Tumhukumu kwa matendo yake na sio maneno ya wapambe wake

TUTABAMS

Member
Sep 10, 2019
55
50
Habari za jioni wana Jf. Poleni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa letu pendwa(Mama Tanzania).

Nimekuwa mfuatiliajia wa tarifa nyingi zinazotufikia hapa jamvini. Kilichonivutia zaidi hadi na mimi kuamua kujibanza nyuma ya keyboard yangu na kupandisha huu uzi hapa jamvini,ni kile nachokiona /soma kama mvutano baina ya makundi makuu matatu ya kisiasa kwenye swala la usukumwaji wa gurudumu la maendeleo ndani ya nchi yetu.

Baadhi ya watu ndani ya chama tawala wanadai maendeleo makubwa yameletwa na yanaendelea kuletwa na Rais wa wamu ya 5.Watangulizi wake wa awamu 4 zilozopita hawakufanya lolote.

Wengine ndani ya chama walikairiwa wakisema hakuna,hakuna jipya lilolo/linalofanyika na awamu ya 5,yote ni mmuendelezo kama sio kunalizia yale makubwa aliyo kwishaanzishwa na watangizi wake wa awami ya 1,2,3&4.


Na wale wasiokuwa ndani ya chama wanaona hakuna kubwa la kimaendeleo alilofanya zaidi ya kuimashisha propaganda na kubomoa Yale mazuri yote ya watangulizi wake.

Hoja yangu hapa kama kicha cha habari kinavyojieleza hapo juu, nawaomba wadau tuorozeshe miradii iliyokamilika au viporo, au maendeleo aliyoyafanya Dereva wetu kwa kipindi hiki cha miaka mi4 ya awamu wa tano. Ili tuweze kulinganisha na awamu zilizopita ili tujue hayo yasemwayo na hayo makundi matatu hapo juu kama yanaukweli wowote.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo.Matusi ruksa kwa atakayejisikia kufanya hivyo,ndio Uhuru wenyewe wa maoni.
 
Unatenganishaje awamu ya tano na awamu zilizotangulia?

Unataka kusema ameipigania nchi ikapata uhuru, akaanza kuijenga nchi kila kitu kuanzia mwanzo bila kukuta chochote toka kwa watangulizi wake?

Miradi, pesa, madeni, rasirimali watu, miundo mbinu, mipango, siasa safi, utawala bora, mipango, sera, katiba n.k zote amezikuta kutoka awamu zilizomtangulia.
 
Back
Top Bottom