Tumfuate Mungu Sio Viongozi wa Dini:Tuguri Zakutwa Kanisani kwa Mchungaji huyu

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
4742613_chaf6_jpg8c8fe1f90736dc67ebba1dd9bd017b40

4742608_chaf1_jpg829af0f93cf03175ee51a7951dca4585

4742609_chaf2_jpg04f2dd4881d75f7d667ac21cfea0c221

Hii imetokea nchini benin baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia kanisa la mchungaji aliyekuwa anatumhumiwa kufanya mapenzi na wake za watu. Waliyoyakuta hawakutegemea ni zaidi ya walichoshutumu.

Tumwabudu Mungu kwa akili na Roho sio kwa kusubiri kuadithiwa na wakuu wetu pale mbele ya kanisa.
 
Imeandikwa "watatokea manabii wa uongo na watafanya ishara kubwa wengine wakisema, Mimi ndiye " Omba upate macho ya rohoni.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, haya ni maneno ya mapema sana ya MUNGU. Na bahati mbaya sana wakristo wengi hatutumii akili tunapokuwa kwenye dini zetu, tumewaabudu watumishi na sio MUNGU, ni kosa kubwa sana kumwangalia mtumisha kama Mungu na ndiyo maana hatupati tunayo yapata. yapo mambo ya msingi ya kungalia unapokuwa kanisani.
1. Utukufu wa jambo lolote linalofanywa hapo linampa utukufu MUNGU au mwanadamu? kama utukufu anapewa mwanadamu kimbia vibaya mnoo hapo hapafai.
2.Je Jina la Yesu, damu ya yesu na neno linatumika kujenga ufalme wa MUNGU au linajenga ufalme wa mtu? kama ni ufalme wa mtu ondoka bila kuaga kama huwezi kubadili mwelekeo.
3.Mnafundishwa kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake kwanzaa? au mnatafuta uponyaji na miujiza na pesa(vitu kwanzaa). Kama vitu kwanza tafakari sanaaaaa
4. Nguvu ya Roho matakatifu inaongezeka hapo ulipo? na unapata mabadiliko yoyote kiroho na kimwili? na mabadiliko hayo unaoujasiri wa kusema ni MUngu kakusaidia na sio figisu zako kama rushwa, uganga na kadhalika? ukiona huwezi kusema asante kwa Mungu kwa chochote ulichopata kwa sababubu huoni mchango wake ondoka hapo unaposali au badilika kama kunanafsi ya mabadiliko.

Kwa mjibu wa MUNGU kanisani ni mahali kukufundishana habari za ufalme wa MUNGU na kushirikisha uzoefu na vipawa, kupeana shuhuda na kusaidiana lakini kwa utukufu wa MUNGU.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Afrika vituko haviishi, yaani anatembea na wake za watu ndio mmuvamie nyumbani kwake, kwani anawabaka? Kwanini msiwafunge kufuli wake zenu? Yote kukosa kazi hii, watu wako busy kwa upuuzi.
 
Afrika vituko haviishi, yaani anatembea na wake za watu ndio mmuvamie nyumbani kwake, kwani anawabaka? Kwanini msiwafunge kufuli wake zenu? Yote kukosa kazi hii, watu wako busy kwa upuuzi.
wanawake wengi wakimuamini mtumishi wako radhi hata kuachika ila kwenye mkesha waende. wao(hao wananchi) ndio maamuzi waliyoona ni sawa japo yanaweza kuwa sio sahihi
 
Back
Top Bottom