Tumezidisha porojo, Tunajenga nchi kwa maneno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumezidisha porojo, Tunajenga nchi kwa maneno

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Oct 3, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kungekua na mashindano ya kuzungumza maneno, basi Tanzania ingekua kinara na pengine ingekuwa ikifanikiwa kutwaa medari zote za dhahabu hasa katika mashindano ya dunia.
  Tumekua hodari wa kuzungumza kubwabwaja kuliko kutenda, il hali kazi haziendi hivyo kurudisha nyuma maendeleo yetu. lakini pia tumekua wepesi wa kulalamika ama kulaumu.
  Angalia Tanzania imekua nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili, wanyama, milima, mito na maziwa ambavyo vinatosha kuwa vivutio vikubwa kwa upande wa utalii hapa nchini.
  Lakini licha ya kuwa na mlima mkubwa; mlima kilimanjaro bado Tanzania imekua hainufaiki na mlima huo kama kenya. Waziri kagasheki amesema ni aibu kwa tanzania kupata watalii wachache wakati kenya wakienda wengi, ni aibu Tanzania kuendelea kuwa na idadi ya watalii wachache wanaingia ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.
  Alisema Tanzania yenye ardhi kubwa na rasilimali nyingi inaingiza watalii wachache ikizidiwa mbali na nchi kama kenya na zimbabwe, lakini ikifuatiwa kwa karibu na rwanda yenye ardhi ndogo.
  Kagasheki kama ilivyo kawaida kwa Watanzania anarudia maneno ya watangulizi wake, anaendelea kupiga porojo, lakini anasahau kwamba Tanzania inazidi nchi hizo jambo moja pia, porojo.
  yeye kama waziri anatakiwa afanyie kazi mambo haya na sio kuyazugumza tuu alafu hamna kazi yeyote. wenzetu wanajitahidi kufanya kazi kuliko porojo.
   
Loading...