Tumewawakilisha wote kwenye MSIBA WA BB YAKE PAKAJIMMY

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.

UPDATE;

PAKAJIMMY na familia yao walifika salama na kumpumzisha mzee wetu mida 7:45 mchana tarehe 28/01. Baada ya siku 3/4 tutakuwa tena na Pakajimmy hapa Jamvini.
 
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.
Mmefanya jambo zuri la kusifiwa. Naamini kwa hili hazina yetu pale juu itaongezeka. Mmbarikiwe sana wakuu.
 
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.
Asante sana Mungu awabariki kwa moyo mliouonyesha.

PakaJimmy Mungu akufariji kwenye kipindi hiki kigumu.
 
Nguli na wengine, mbarikiwe. Mungu amlaze pema mzee wetu na kuwapa faraja wafiwa, AMEN.
 
Nguli,Chrispin,bht,Binti Sayuni(Ziondaughter),Geof na Kaizer,nimefarijika sana kusikia kwamba mlituwakilisha wana JF katika msiba wa baba ya rafiki/ndugu yetu PJ,ninawashukuru sana wa hilo na ninawaomba muendelee na moyo huu wa upendo na mshikamano mliouonesha katika kipindi hiki kigumu kwa rafiki/ndugu yetu PJ na familia yake...Mungu awabariki sana wakuu
 
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.

Asanteni sana kwa uwakilishi mliotufanyia.
 
Binafsi nashkuru sana,hope atakaporudi sisi wengine tulioshindwa kwenda tutaenda kumwona,Aanteni sana Mungu awabariki na zaidi ampe faraja PJ
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.
 
Wote mliohudhuria msiba kwa Dar asanteni sana kwa uwakilishi wenu, ningeomba kwa sisi tuliopo Arusha tuwasiliane (PM) ili tuweze kwenda kumpa pole pale atakaporudi. Mungu akutie nguvu PJ
 
Kazi nzuri sana hiyo....charity begins at home.........kwa sisi hapa our home is JF! So hopeful if we can show this love and solidarity here, hope we can replicate the same all over the country to our beloved brothers & sisters........!

Pamoja sana!
 
mungu awabariki na awaongezee moyo wa upendo hili mlilofanya si dogo ..
asanteni sana
 
Mimi, Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer tumewawakilisha wana JF wote kwenye msiba wa baba yake Pakajimmy maeneo ya kitunda na safari ilianza mida ya saa 8 kulekea Mbeya ambako mzee wetu atapumzishwa. Na tulivyowasiliana mida ya saa 11 walikuwa wamepita maeneo ya morogoro mjini.

Pakajimmy kafarijika na anawashukuru wana JF wote kwa support mliompa kipindi hichi kigumu.

Ahsanteni sana, kwa undugu wa kweli, may godbless you All.
Amen.
 
Wote mliohudhuria msiba kwa Dar asanteni sana kwa uwakilishi wenu, ningeomba kwa sisi tuliopo Arusha tuwasiliane (PM) ili tuweze kwenda kumpa pole pale atakaporudi. Mungu akutie nguvu PJ

Tunawashukuru sana wan JF mlioko Dar,na sisi wa-Arusha tutajitahidi atakaporudi tutaenda kumwona,niliongea nae juzi na jana nikamwahidi atakaporudi tu nitamtafuta,Preta wazo lako nalikubali kwa 100% nitaku-PM
 
Mungu awabariki sana wa JF wa Dar,mmeonyesha moyo wa upendo sana na kujali kwa rafiki yetu PJ,tuendelee na moyo huu,nimeifurahia sana hii familia ya JF jinsi ambavyo tunabeba mambo kwa umakini mkubwa,Nguli,Chrispini, BHT, Geof, Ziondaughter na Kaizer Mungu awabariki saaaana.
 
Kwanza kabisa nampa pole ndgugu PJ kwa msiba mkubwa uliomfika wa kumpoteza Baba yake mpendwa. Ni msiba mkubwa sana na baada ya kuongea naye kwenye simu niliona ni kwa jinsi gani ndugu yetu huyu alikuwa kwenye majonzi makubwa.

Pili napenda kuwapongeza wote mlioenda kwenye kuaga mwili wa Mzee wetu mkiongozwa na Mhe. Nguli binafsi nawashukuru sana. Hakika nimefarijika sana kutokana na nyie kuwa hapo na hakika faraja aliyoipata ndg. PJ itakuwa kubwa sana. Kwa mimi ambae niko nje ya jiji la DSM kwa sasa ambaye nilitamani kushiriki nimefarijika sana na kwenda kwenu hapo.
Labda niseme wazi tu kuwa PJ alihudhuria msiba wa Babu yangu uko Arusha na hakika ni mtu wa watu na amekuwa mtu wa watu siku zote.
Bwana alitoa Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amen
 
Back
Top Bottom