G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kwanza sijui kwanini Board ya korosho imetumbuliwa wakati kosa ni la serikali.
Sijui kwanini waziri wa kilimo ametumbuliwa wakati alimlilia Dr. Mpango machozi pale bungeni! Ona sasa Mpango alivyomponza mwenzake.
Twendeni kimahesabu kisha tuangalie mwenye kosa ni nani?
Tayari tumekwapua Tshs bilioni 250 za wakulima wa korosho (Export levy)
Tayari tunaenda kununua tani 210,000 za korosho kama serikali (Najua wafanyabiashara katu hawatonunua wakati hakuna faida)
Sasa kwa bei ya Tshs 3000 kwa kilo maana yake serikali inahitaji kununua korosho kwa Tshs bilioni 630. Ukichukua ile Export Levy waliyokwapua ya Tshs bilioni 250 ambayo kimsingi ni fidia kwa wakulima pale soko linapokuwa baya. Hii ndiyo fedha inayotumika kufidia gharama mbalimbali na huongezwa kwenye manunuzi. Maana yake chukua 630 bilioni - 250 bilioni unabakiwa na 380 bilioni. Hizi 380 bilioni ndiyo fedha halisi ambazo serikali itatoa mfukoni mwake kununua korosho.
Sasa Tani 210000 ni sawa na kilo 210,000,000 za korosho
Ukichukua Tshs 380,000,000,000 ukagawa kwa kilo 210,000,0000 unapata Tshs kadirio la juu 1900 kwa kilo.
Hiyo ndiyo bei halisi serikali inayoenda kununulia korosho. Kisha tutakuwa na mapambio ya kila aina wakati mchawi ni Mpango alipoikwapua ile Export Levy!
Pole sana Tizeba ulilia sana pale bungeni kuhusu sakata la export levy na ukamtahadharisha Mpango kuwa anakuweka pagumu kiutendaji ila Mpango akavaa miwani nyeusi! Pale alikuwa anachimba kaburi lako na jana kakuzika rasmi!