Tumewaona, Joji na Mkewe - Tuwachambue

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,617
8,754
Tumewaona Joji Kichaka na mkewe Laura Kichaka katika ziara hii iliyofanyika hapa nchini kwetu; na wananchi wengi wameweza kuwaona kupitia luninga na hata kwenye picha magazetini.

Pia tumeweza kuona jinsi walivyojionyesha wakati walipojumuika nasi katika ghafla na shamrashamra mbalimbali, ikiwa ni kwenye ngoma au katika sherehe na kuwekeana sahihi katika mikataba, au katika kugawa vyandalua au kutembelea wagonjwa katika hospitali zetu.

Je, nafasi hii inaweza kutupa mwanga hawa watu ni wa namna gani?
Ni watu wanaowajali binaadam wenzao bila kujali rangi zao? Je, tabia waliyoionyesha hapa, na hasa ukiangalia picha mbalimbali unaweza ukakubali kwamba hawa ni watu wanaowajali wenzao?

Wakati tukiyafikiri hayo, ni bora pia tukiwalinganisha na wengine (nina maana ya wazungu wengine wanaoonyesha unyanyapaa au dharau na kujiona wao ni bora zaidi.

Je, kweli huyu ndie Joji mwenyewe, au alikuwa ni wa kuigiza? Na yule aliyekuwa na majipu makwapani alipotelea wapi?

Laura yeye sina shaka naye. Yeye ni huyo huyo tuliyemwona hapa.
Wasiwasi wangu ni kwa Joji. Sehemu moja inanishawishi kumkubali kuwa ndie, lakini sehemu nyingine inaniacha na mashaka.
 
Back
Top Bottom