Tumewajua mapema: Miezi 6 uwanja Chato, miaka 24 uwanja Butiama no!

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,333
72,796
Kuna kauli nyingi kuwa serikali ya sasa inaangalia vipaumbele na kumjali mwananchi.

Ajabu bajeti ya kwanza tuu miezi 6 baada ya kuingia madarakani zinatengwa zaidi ya Bil2 kujenga uwanja wa ndege Chato.

Hicho ni kipaumbele? Kama ni umuhimu wa Rais aendapo "kutembea" kwao kwa nini wasipanue uwanja wa Geita ili uweze kutumika pia na ndege za usafiri wa RAIA naye akitumia uwanja huo kisha Gari kwenda Chato?

Mbona Nyerere hakuwahi kuwaza kujenga Airport Butiama? Au Mkapa Nanyumbu?
Hapa iko namna, mpaka inani kumbusha kitendo cha kwenda kuweka Traffic Lights kwenye barabara Kule Chato zisizo na matumizi yeyote.

Huwa wanaanza hivi hivi, kidogo kidogo kisha inakuwa tabia na mazoea na kuhoji inageuka kuwa dhambi
 
Subiri mtaisoma namba vizuri, na nilazima mtambuwe tunahitaji Ikulu mpya Chato Rais wetu mtukufu akiwa anakwenda mapumzikoni, tena tunahitaji ifanane na ile ya kijijini kwa Jacob Zuma maana hawa hadhi yao na uchumi wa nchi zao ni sawasawa.

1465618991456.jpg
 
Huyo asemaye ni rafiki wa masikini HARAKA SANA anaonyesha ajipendavyo.
Kwa waliowahi kupita Chato, wanaweza kusema wakati akiwa waziri wa ujenzi aliagiza ziwekwe traffic light pale kwa ajili ya nini hasa? Kama sio kutaka ufahari tuu?
 
I
Kuna kauli nyingi kuwa serikali ya sasa inaangalia vipaumbele na kumjali mwananchi. Ajabu bajeti ya kwanza tuu miezi 6 baada ya kuingia madarakani zinatengwa zaidi ya Bil2 kujenga uwanja wa ndege Chato. Hicho ni kipaumbele? Kama ni umuhimu wa Rais aendapo "kutembea" kwao kwa nini wasipanue uwanja wa Geita ili uweze kutumika pia na ndege za usafiri wa RAIA naye akitumia uwanja huo kisha Gari kwenda Chato?
Mbona Nyerere hakuwahi kuwaza kujenga Airport Butiama? Au Mkapa Nanyumbu?
Hapa iko namna, mpaka inani kumbusha kitendo cha kwenda kuweka Traffic Lights kwenye barabara Kule Chato zisizo na matumizi yeyote.
Huwa wanaanza hivi hivi, kidogo kidogo kisha inakuwa tabia na mazoea na kuhoji inageuka kuwa dhambi
INASIKITISHA SANA
 
Nyie mbona mmeiba mkajenga kwenu hatusemi?.

Halaf hilo suala mbona ni uongo wa mchana kweupe....mimi niko bungeni nyaraka zote ninazo za bajeti hayo mambo hayapo.

UKAWA wamebaki kutapatapa kuwa mawakala wa mafisadi.
 
Magufuli ana hasira Fulani kwa watu fulani kutoka mikoa Fulani akiwa na imani kwamba hawa watu na mikoa yao imeendelea kwa ajili fulani lkn labda haelewi hili lilianzia wapi na mantiki ya Nyerere kuunganisha waTZ kuwa kitu kimoja bado haelewi.

Hii ni sawa na kumjengea mtu choo lkn anaenda kujisaidia ziwani kwa sababu ustaarabu huo hana wala hajafundishwa.

Tafakari kwa makini utanielewa, Nyerere alielewa hili vizuri so alitaka to equalize kwa busara na akili
 
Back
Top Bottom