Guru Master
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 224
- 591
Siasa siku zote ndo imekuwa ni njia ya kweli ya kuongoza mabadiliko na mapambano ya dhati kuelekea ukuaji wa uchumi. Misimamo mitizamo,mikakati,maono na mwongozo kuelekea uchumi fulani katika dunia yote.
Hapa utanzia kwenye miundo mbinu imara ya kukuza uchumi kuanzia kwa mwananchi wa kawaidaa halafu kwenda kwa serikali yenyewe na tena kurudi kwa mwananchi wa kawaida. Miundo mbinu imara kama ukusanyaji halali na sahihi wa kodi bila kuwabebesha mzigo mkubwa maskini, ujenzi wa shule ,hospital,barabara, viwanda n.k
Upatikanaji wa kipato halali kwa wananchi na malipo sahihi. Kupunguza gap la wenye nacho na wasio nacho na kujenga umoja na upendo kati yao ili wasio nacho waone haja ya kusaidia wasio nacho na hivyo kuisaidia serikali kwa namna nyingine.
Siasa za maji taka,ubabe, udikteta, urubuni,umangi meza, fitna na kifisadi siku zote zimekuwa chanzo cha kuanguka uchumi wa nchi nying za kiafrika.
Wanasiasa wetu wa nchi nyingi za Afrika wamekuwa ni wenye kuangalia maslahi yao binafsi kabla ya kuangalia maslah ya taifa. Wametengenza namna ambayo wananchi wanawachagua wao ili waje kuwa maboss wao.Na ndo maana hali hii imejenga na mna ya kutengeneza wanasiasa wenye kiburi,ujivuni,majidai na nyodo mbele za wananchi.
Kiongozi anasemaje kuwa yeye amewekwa na Mungu hapo alipo? unajiuliza huyo mungu ni nani?
1. Aliyemteua/ aliyemchagua
2. Mungu aliye sehemu fulani hivyo hata aliye mteua hana nafasi ya kumwajibisha?
Unawezaje kuwaambia wananchi kuwa wapende wasipende kitu flan kitafanyika hata kama itabidi wale nyasi? Unawezaje kuwambia wananchi kuwa hujali na kama watakunyima kura zao wakunyime hamna shida wewe haikusumbui?
Katika hali hii ya kuwanyanyasa wananchi unagundua kuwa ni ngumu kusimama katika uchumi sahihi wa kututoa katika hatua moja kwenda nyingine kwa sababu ya ukosefu wa utashi wa mambo muhimu. Tuna matukio ambayo yatabaki kuwa kovu katika maisha yetu. Kuna vifo ambavyo wananchi wenyewe walipaswa kuvisimamia kidede na kuwaenzi wahusika ili wengine wasikate tamaa.
Ni wa ngapi wanamkumbuka stan katabalo na ile kashfa ya loliondo? Mwandishi wa habari huyu aliuawa akiandika kitu chenye maslha kwa taifa mabalo mpaka leo halijaweza kumkumbuka na kuona ushujaa wake. Ni nani anamkumbuka daud mwangosi? Mwandishi ambaye aliuawa akiwa katika kutimiza majukumu yake. Ameiacha familia yake yatima mpaka leo haifahamiki wanaishi vipi na je walilipwa angalau kifuta machozi kwa kuondokewa na baba wa familia?
Ben Saanane amepotelea wapi? Mtu aliye na zaidi ya miaka 18 anapoteaje na watu wakanyamaza kuacha kama ilivyo?
Mnamkumbuka dr. Ulimboka? madktari wenyewe ambao alikuwa akiwatetea mmemsahau kama ganda la mua ambalo lilishanyonywa utamu wake na hivyo kuwa halina faida tena. Siasa za hovyo husababisha kujengwa kwa taifa la hovyo. Siasa za kimatukio husababisha taifa la kimatukio.
Uchumi wetu hauwezi kuwa imara ikiwa tunaongozwa na siasa za maji taka, vumbi, bora liende na msenenge unenge yaani liwalo na liwe ili langu liwe.
Haya ni mambo ambayo kama taifa tunapaswa kuyaangalia. Bila hivyo hata miaka 200 ijayo nchi zetu zitakuwa kama zimesimama maana katika miaka hiyo tutafikia hatua mbayo wenzetu ndo wapo sasa. Kwamaana ya kuwa nao watakuwa wamesogea mbali sana.
Tukiweka mbele maslah ya vyama na kusahau utaifa hatuwez kuendelea kamwe. Uchumi wetu utategemea sana an aina ya siasa tunayofanya. Je, tunakubali kukosolewa? Tunayafanyia kazi makosa tuyafanyayo?
Tunaruhusu watu huru watupe changamoto au tunataka kuitwa watukufu na watakatifu? hayo ndo maono tuliyo nayo. siasa za kibabe,udhaifu na kukosa uelekeo.
Katika mambo yote tufanyayo tusisahau dunia inazunguka. palipo na usiku leo baadaye patakuwa na mchana. Kuna mvua na jua. Kuna masika na kiangazi. ukilijua hili siku zote utaishi ukitunza maji na pia utaishi ukiweka eneo kavu kwa kujua kuna kipindi cha masika bonde halitakufaa kama ambavyo kipindi cha kuangazi bonde ni sehemu nzuri kwa kupata maji na unyevu. Milima na mabonde hutegemeana kwa maana ya kuwa bila mlima hakuna bonde na bila bonde hakuna mlima.