MpigaFilimbi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,169
- 182
Mchungaji umenena vyema kabisa. Ifike mahali tuamue kuacha visingizio tukae na tujadili mustakabali wa taifa letu, na tuamue kuchukua hatua inayofaa na mwelekeo unaostahili ili vizazi vijavyo visije kututupia tena lawama. Tumepumbazwa na tumepumbazika kiasi kwamba tumeuza hata uhuru wetu wa kufikiri. Wapo ambao huwa hawaamini hata kile wanachokifikiria kuhusu familia zao. Hatufundishi watoto wetu fikra za maendeleo, kujitegemea na utu, wanachoweza ni kuiga wizi na kuombaomba.
Ni kweli tunaweza kuamua kurudisha uhuru wetu na kujithamini kama binadamu tunaostahili heshima na kuthaminiwa kwa kuanza kuthamini utu wetu na urithi wa taifa letu. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuacha kuwa kibaraka wa mtu yoyote.