Tumeuza Uhuru Wetu....na Hazina yetu tumeifuja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeuza Uhuru Wetu....na Hazina yetu tumeifuja!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jul 31, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa hiari yetu wenyewe, kwa kutumia nguvu zetu wenyewe, kwa akili zetu na utashi wetu ulioambatana na upofu uliojaa tamaa, uvivu, usengenyaji na uroho, Tumeuza Uhuru wetu na hazina yetu tumeifuja.

  Sisi ni koloni lililo na Uhuru wa Bendera, tumejitakia kwa ujuvi wetu kuwa masikini wa kudumu, wanyonge ndani ya nchi yao na kuburuzwa kila siku kama majuha.

  Angalieni jinsi neema tulizopewa na Mola tulivyoziharibu kutokana na tamaa, majaribu, ujinga na kiburi kilichojaa uvivu na utegemezi.

  Zi wapi zile ndoto za Kujitegemea, Siasa safi, Uongozi Bora kwa kutumia Juhudi na Maarifa kuupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi?

  Kila siku kukicha ni baragumu za ufujaji na uhujumu. Leo ni Benki Kuu, mara ni ATCL, TRL, Tanesco, Misitu, Utalii, ardhi, madini, uvuvi na hata kujiingiza katika kuatakia shari jirani zetu na kuneemesha maangamizi ndani ya ardhi yao.

  Siwalaumu viongozi pekee, bali lawama za kwanza ni kwangu mimi (na wewe), niliye mjinga ambaye kwa upumbavu nimekimbia majukumu yangu na wajibu wangu niliopewa na Mola na kulindwa na Katiba ya Nchi yangu, kwa kuuza haki yangu ya kupiga kura kwa kukubali kuburuzwa kwa kulishwa andazi na chai.

  Laiti ningekuwa mjasiri na kuitafuta kweli na haki na hata kuamua dira ya Taifa langu kwa kutumia umakini na busara, leo hii nisingekuwa hapa nikiangua kilio na kujitwisha mavumbi nikiwa nimevaa kaniki, nikihangaika kwa tabu na mateso, njaa na magonjwa yakiniwinda kwa urahisi nami nikawa mkimbizi wa ardhi niliyopewa na muumba.

  Ni aibu ya kutisha, utajiri wote nimeutapanya kwa manufaa ya wageni na si ya ukoo na jamaa zangu. Nimeendelea kuwa mpumbavu kwa kulewa mvinyo na asusa za bure, nilizovimbiwa huku nikisifiwa kuwa nimejaaliwa neema na ni mpole.

  Tumeuza nchi yetu, sasa tuamue tuendelee na maombolezo huku tukinyanyaswa na kusulubiwa na njaa na umasikini au tuamke tupukute vumbi, majivu na kufuta machozi na kuanza upya kwa kujitutumua na kutumia busara katika kutafuta haki.

  Haki na hadhi yetu itarudi pale tutakapoamua kwa sauti moja iliyo kubwa na kishindo kuwa tumechoka kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa.

  Tuikimbilie haki yetu kwa nguvu bila woga, tutumie dhamana yetu kwa ufasihi, ili hazina na rasilimali zetu ziwe kwa manufaa yetu, kama Muumba alivyotupangia.

  Jiulize, mpaka lini utaendelea kuamini ahadi hewa, ukiwa umelewa togwa ya ukwaju na kupewa leso kufuta jasho, huku maji na kuku wa karamu ni yule uliyemtoa zaka?

  Kuwang'oa mafisadi na kuushinda umasikini utaanzia na nafsi yako, kisha familia yako, ndipo cheche zitakaposambaa katika mtaa, kaya, kijiji, kata, tarafa, wilaya, jimbo, mkoa na Taifa.

  Kuushinda Unyonge, Umasikini na Maradhi utaanzia kwako binafsi na kwa nguvu zako na majirani zako utaweza kuushinda utumwa.

  Ni hiari yako kuendelea kuwa mtumwa au kuurudisha Uhuru wako na kulinda hazina yetu!
   
 2. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Deep, Rev, deep!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  safi sana, narudia tena safi sana Rev!!!

  ujumbe mzuri kabisa.

  naomba hili liwe somo la wiki kwetu wana jf
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mchungaji Umeongea kwa Uchungu Mkuu, Hakika wapita huko na huko wakinisifu kwa UPOLE MFANO WA KUIGWA
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Inagusa na Inagusa kwelikweli SO? Nisingependa niwe mchoyo kwa waraka huu. Nautuma kwa Rais wa jamhuri ya muungano Wa Tanzania kwa niaba ya serekali yake. Ninahakika ameupata na atausoma tena na tena ...na tena ....Ninahakika isiyopimika atakuja hadharani na kunukuu kifungu hiki na kusema atakachosema ...Nina hakika He will do it and we will all be very happy! Kusikia maoni yake kwa niaba ya serekali nzima. ... wanyonge tunasubiri!!
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hapana ,hebu msikilizeni mwasisi wetu wa Taifa letu.
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=W2UlKYNPYIE&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=OUsmuG_9mhQ&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=_S-nYyq6nDY&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=vkQrfuAgVOk&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Siwalaumu viongozi pekee, bali lawama za kwanza ni kwangu mimi (na wewe), niliye mjinga ambaye kwa upumbavu nimekimbia majukumu yangu na wajibu wangu niliopewa na Mola na kulindwa na Katiba ya Nchi yangu, kwa kuuza haki yangu ya kupiga kura kwa kukubali kuburuzwa kwa kulishwa andazi na chai.

  Laiti ningekuwa mjasiri na kuitafuta kweli na haki na hata kuamua dira ya Taifa langu kwa kutumia umakini na busara, leo hii nisingekuwa hapa nikiangua kilio na kujitwisha mavumbi nikiwa nimevaa kaniki, nikihangaika kwa tabu na mateso, njaa na magonjwa yakiniwinda kwa urahisi nami nikawa mkimbizi wa ardhi niliyopewa na muumba


  Kwa kweli Rev umesema kweli Laiti ningekuwa na uchungu wa kweli kama mwanamwali aliyewekwa ndani nikaanganza jua linalochomoja juu ya uso wa bahari nikatafakari jinsi mababu zetu walivyolinda rasimali ya nchi nika na nguvu na ujasiri wa kukemea eeh Mungu wangu ibariki Tanzania
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jiulizeni ni lini tuliuuza Uhuru wetu? Je hamjioni kama ni koloni linalotawaliwa kwa hiari mithili ya Malaya Mchovu anayekubali kila bwana na hata thumuni?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Huu ni ujumbe unaotakiwa kuchapwa katika mashati na kuwekwa kwenye mabango barabarani; ni ujumbe unaotakiwa kutangazwa juu ya paa na kuimbwa kama kibwagizo katika ngoma; ni ujumbe ambao watoto wanatakiwa wajifunze pale wanapoanza kujifunza a e i o u ! Ni ujumbe ambao wakati wake umefika!

  Ni HIARI YETU KUENDELEA KUWA WATUMWA AU KUURUDISHA UHURU WETU!

  Ndiyo!! na kuilinda hazina yetu ni hiari yetu pia!

  Kudos mchungaji!
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Wazo zuri sana hilo, Shukrani sana!
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hata Tisheti au Kanga yenye haya maneno hapa chini itafaa.

  "Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni, na nyumba zetu kuwa mali za makafiri"
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Ningeikatishia hapo pa mwanzo..
   
 13. U

  Ulusungu Member

  #13
  Aug 1, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Mchungaji kwa ujumbe mzito kwa watanzania binafsi na waafrika wote kwa ujumla,ni ujumbe mzito sana na wa maana sana kwa kizazi hiki tatizo kubwa kwa watanzania tulio wengi ni uvivu wa kufikiri na kutafakari hata mambo yaliyo muhimu si kwa taifa na jamii bali hata kwa mtu binafsi.lau kama watanzania tungeweza kutafakari japo kwa secunde 10 kila tunalofanya na kuweka bayana manufaa yake kwetu binafsi na taifa kwa ujumla na kujua athari zake si kwa kipindi husuka bali kwa karne nyingi zijazo tunaweza kuwa na msingi mzuri wa mapambano na kujitoa katika utumwa wa kushinikizwa kwa kauli na zawadi sisizo na faida hata kidogo.
  Mchungaji amezungumzia mambo manne ambayo yamezungumzwa kwa kipindi kirefu sana,nadhani tunalo jambo moja kubwa ambalo tukiweza kulishinda tutakuwa tumerahisisha ushindi kwa hayo mengine...Nalo si jingine bali ni UJINGA,tukiuondoa ujinga miongoni mwetu tutakuwa tumeshinda kwa asilimia kubwa matatizo mengine.
  Ujinga uko ndani ya Maprofesa,Madaktari na wale ambao tunawaona kana kwamba wameelimika lakini kwa kiasi kikubwa wameneemeka na Ujinga. Ujinga hauondolewi kwa tuition (Tution kwa mtazamo wangu ni moja ya matanuru ya kukomoza ujinga,kwa sbabau mtoto huenda tuition kufundishwa yale ambayo anafundishwa darasani bali hana mda wa kuyasoma na kuyatafakari,msisitizo ungekuwa kusoma,kusoma,kusoma,taitizo la wanafunzi wa kitanzania na waafrika kwa ujumla ni kutafakari,mwanafunzi wa kitanzania hata akiulizwa maswali kwenye mtihani yale yanayohusu vitu anavyotumia kila siku kama Muhogo,Matembele,Mchele,Mahindi n.k.anauwezekano mkubwa kushindwa kwa sababu anavitumia bila kutafakari)
  Ombi langu kwa wana JF kila mmoja wetu katika mazingira tunayoishi aanze yeye mwenyewe kujijengea utamaduni wa kusoma na kutafakari kwa kila akifanyacho na kukitumia ili kuongeza kiwango cha ufahamu.mfano mdogo,ni wa mtu mzima kabisa ambaye ana mafua na kikohozi anakwenda duka la dawa, anaomba dawa inayohusika mhudumu anampa dawa na maelezo ya kutumia (kama 10mls *3 @ day) mtu mzima huyo huyo nafakia nyumbani au pale pale anamimina dawa kwenye kichupa 10mls na kubugia bila hata kujisumbua kujua hiyo dawa imetokana na nini na kunaangalizo gani katika maandishi yaliyotapaa kwenye chupa na kwenye box lake,matokeo anakunywa dwa iletayo usingizi huku anaendesha chombo cha moto na kusababisha ajali mwisho SHETANI kupewa utukufu kwa ajali ya huyu MJINGA.
   
 14. S

  Sebere Member

  #14
  Aug 1, 2009
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev,maoni yako ni mazuri sana, watanzania angalau 20% wangeweza kuyasoma kungekuwa na mabadiliko lakini sasa yanaishia kwa watanzania 0.1%.pole sana.
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Si kweli kuwa Watanzania hawajui yanayowasibu au kufahamu umuhimu wa kutatua yanayowapa shida, bali ni Upumbavu ndio unaotufanya tueendelee kuangamia.

  Ujinga tulikuwa nao baada ya kupata uhuru, tukasomeshana, tukasemezeshana, tukatiana shime, tukaimba, nasi tukaanza kazi tukidai tuko huru na mwelekeo wetu ni wa kujiongoza na kujijenga tujitegemee na kushinda Ujinga, Umasikini na Maradhi.

  Lakini Watanzania si Ujinga uliokithiri tena, bali ni Upumbavu kutokana na hiari, wala si kulazimishwa.

  Wananchi wanaiga Upumbavu wa Viongozi, na hivyo Taifa zima linakosa mwelekeo.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Aug 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Ebana eeeh hapo umemkoma Nyani kweli kweli
   
 17. S

  Shamu JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Shamu,

  Lini tutaacha kutoa visingizio na kutafuta wa kulaumu?

  Tulianza na Utumwa, tukaja mkoloni, kisha Kenya, Uganda, Kaburu, Mhujumu, Nyerere, Mwinyi, Mkapa CCM na sasa Kikwete na hata Upinzani!

  Lakini katika mtiririko wote huu, hakuna mahali tuliposema kwa umoja kama Taifa "Sasa basi, visingizio tuviache" ili kuanza kujijenga upya?

  Mkoloni aliondoka miaka 50 iliyopita, Nyerere katutoka miaka 10 iliyopita, Utumwa tuliuacha miaka 200 iliyopita, vita vya majimaji vilikwisha karibu miaka 100 iliyopita, ni Lini Mtanzania ataamka na kujipukuta vumbi na kulia kobisi ya kale na kung'ang'ania visingizio bila kuamua kwenda mbele?

  Ni hiari yetu tunaburuzwa, ni Utashi wetu tunanyanyaswa ni Upumbavu wetu tunaibiwa, je tuendelee kumlaumu Mkoloni na Nyerere au Karume na hata CCM?

  Kwa nini basi tusiamke na kutumia hiari na wajibu kusahihisha makosa yetu na kuachana na Upumbavu wetu?
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WEWE SHAMU!muacheni huyu mzee apumzike kwa amani!tumezoea sana SPOON-FEEDING WASWAHILI!haikuwa rahisi kwa mwalimu kufanya kila kitu kwa ajili yetu

  Aliyoyafanya mengi yametufikisha mahala pazuri sana.kwa sasa ninaona kwamba NI JUKUMU LETU SASA.........!mimi na wewe ambao kwakweli TUMEUZA UHURU WETU..............
   
 20. S

  Shamu JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninazungumzia mizizi ya Ufisadi na Rushwa zilipoanzia. Kama Nyerere angekuwa kama Mandela tungekuwa mbali sana. Mandela hakutaka kutawala sana ktk chama chake ndiyo maana akawaachia vijana wake. Mizizi ya rushwa na ufisadi ambayo Nyerere kaipandikiza ktk CCM na Serikali yake haitoweza kuondelewa kwa muda mrefu. Nyerere kaiongoza CCM; lakini kwa nini hakupandikiza mizizi ya viongozi bora ktk CCM? kwanini CCM haina utawala wa haki? Wananchi wa TZ bado ni maskini; kwa sababu ya CCM na sera zake za rushwa na ufisadi. Kwa nini Nyerere hakuwapa demokrasia, elimu bora WTZ ktk muda wote? Mpaka sasa hatuna hata viongozi bora wa upinzani; kwa sababu viongozi wote hao wa upinzani wanatoka CCM.
   
Loading...