IslamTZ
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 309
- 182
Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya Demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika.
Baada ya kutangazwa matokeo, viongozi wa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA na ACT, walijitokeza hadharani kutangaza kutoyatambua matokeo. Hili ni jambo sahihi kwani hakuna namna unaweza kuukubali uchafuzi ule uliobatizwa jina la uchaguzi.
Shida ipo katika hatua zilizotangazwa za kupambana na udhalimu na ujambazi uliofanyika dhidi ya demokrasia.
Vyama vya upinzani vimetangaza maandamano yasiyo na ukomo yatakayoanza kesho Jumatatu Novemba 2.
Tujiulize maswali mawili: Kwanza: je maandamano ni muhimu? Pili: Je maandamano yanawezekana na yataleta tija inayotegemewa katika muktadha wa Tanzania?
Nikianza na swali la kwanza, hakika maandamano ni muhimu, tena ni muhimu sana. Maandamao ni moja ya njia muhimu za kujieleza katika siasa za kidemokrasia, haki ambayo inatajwa hata kwenye katiba ya nchi (rejea uhuru wa kujieleza na kutoa maoni).
Kwahiyo, katika hali ya kawaida, ilikuwa ni muhimu kuandamana kuelezea kutoridhishwa na uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika.
Hata hivyo, kuhusu swali la pili, kwamba, je maandamano yanawezekana na je yataleta tija? Jibu, bila shaka, ni hapana. Nina hoja tatu za msingi za kuamini maandamano hayataleta tija.
Hoja ya kwanza ni ukatili wa vyombo vya dola utakaopelekea watu wengi kuumizwa, iwapo watajitokeza. Uzoefu wa Zanzibar na maandamano yaliyowahi kuitishwa huko nyuma dhidi ya utawala wa awamu ya tano, yakiwemo yale ya UKUTA na yale ya Mange Kimambi, unaonesha kuwa hii ni serikali ya kikatili isiyojali kabisa utu na haki za binadamu.
Katika utawala wa serikali ya awamu hii, uhai wa binadamu hauna thamani hata kidogo. Watakuua na hawatajali. Kwa nini viongozi wa upinzani muwapeleke watu kwenye kifo hali mnaelewa kiwango cha ukatili wa serikali hii?
Tuseme, watu wameandamana na baadhi kadhaa wamekamatwa na kuwekwa ndani. Je, vyama hivi vilivyoitisha maandamano vina uwezo wa kwenda kuwatoa ndani kwa kuwawekea dhamana au itakuwa kila mtu na lwake? Naelewa kiuhakika kabisa kuwa wengi kati ya watakaojitokeza (kama kweli watajitokeza) ni vijana wadogo, maskini ambao huenda familia zao hazina mbele wala nyuma na zinawategemea katika kutafuta riziki. Je mmewafikiria hao wategemezi?
Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa ya Watanzania wasioridhishwa na ukandamizaji wa demokrasia., lakini changamoto za kimaisha wanazokabiliana nazo ni kubwa mno kuwafanya wajali. Hivyo, ni wazi kuwa, watakaojitokeza kwa maandamano ni watu wachache sana, jambo ambalo litarahisha kazi ya vyombo vya dola ya kuwashughulikia.
Na baada ya kushughulikiwa kikatili, naamini vijana hao hawatarudia tena kuandamana. Jambo hili likitokea litaipa serikali dhalimu ya CCM ushindi wa kisaikolojia. Watasema na kutangaza duniani kote, ‘Aagh ni wakorofi wachache tu waliokuwa wakileta ukorofi.’
Ndugu viongozi wa upinzani kutoka vyama vya ACT na Chadema, jaribuni kuwalelewa watu mnaowaongoza, na tafadhalini msiwapitishe katika njia wasiyoimudu kwani wafuasi huenda wakaamua kuacha hata kuunga mkono mapambano ya kidemokrasia. Kuwafanya watu waandamane hivi sasa ni sawa na kukamua jipu lisiloiva.
Nini kifanyike? Mambo mawili ni muhimu sana. Kwanza, vyama viendelee kupaza sauti za kupinga uchafuzi wa demokrasia uliofanyika kwa kutumia vyombo mbalimbali ili kunyanyua uelewa miongoni mwa wananchi na hivyo kupata uungwaji mkono. Hoja isiwe chama kipi ni mahiri zaidi katika kuleta maendeleo bali ulinzi wa demokrasia yetu.
Pili, viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine wajaribu kushawishi jamii ya kimataifa kwanza kutotambua uchaguzi na matokeo yake na kisha kuibana serikali ya Magufuli irudie uchaguzi baada ya kufanya mabadiliko ya kisheria yanayokandamiza demokrasia.
Kwa kumalizia, ni vyema kwa vyama vya upinzani kujitathmini. Baada ya kufanyiwa dhulma walizofanyiwa, Je nini wanaweza kufanya ili vyama hivi viendelee kuheshimika na kukubalika mbele za wananchi?