Tumeumia, lakini chonde chonde tusiandamane...

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya Demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika.

Baada ya kutangazwa matokeo, viongozi wa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA na ACT, walijitokeza hadharani kutangaza kutoyatambua matokeo. Hili ni jambo sahihi kwani hakuna namna unaweza kuukubali uchafuzi ule uliobatizwa jina la uchaguzi.

Shida ipo katika hatua zilizotangazwa za kupambana na udhalimu na ujambazi uliofanyika dhidi ya demokrasia.

Vyama vya upinzani vimetangaza maandamano yasiyo na ukomo yatakayoanza kesho Jumatatu Novemba 2.

Tujiulize maswali mawili: Kwanza: je maandamano ni muhimu? Pili: Je maandamano yanawezekana na yataleta tija inayotegemewa katika muktadha wa Tanzania?

Nikianza na swali la kwanza, hakika maandamano ni muhimu, tena ni muhimu sana. Maandamao ni moja ya njia muhimu za kujieleza katika siasa za kidemokrasia, haki ambayo inatajwa hata kwenye katiba ya nchi (rejea uhuru wa kujieleza na kutoa maoni).

Kwahiyo, katika hali ya kawaida, ilikuwa ni muhimu kuandamana kuelezea kutoridhishwa na uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika.

Hata hivyo, kuhusu swali la pili, kwamba, je maandamano yanawezekana na je yataleta tija? Jibu, bila shaka, ni hapana. Nina hoja tatu za msingi za kuamini maandamano hayataleta tija.

Hoja ya kwanza ni ukatili wa vyombo vya dola utakaopelekea watu wengi kuumizwa, iwapo watajitokeza. Uzoefu wa Zanzibar na maandamano yaliyowahi kuitishwa huko nyuma dhidi ya utawala wa awamu ya tano, yakiwemo yale ya UKUTA na yale ya Mange Kimambi, unaonesha kuwa hii ni serikali ya kikatili isiyojali kabisa utu na haki za binadamu.

Katika utawala wa serikali ya awamu hii, uhai wa binadamu hauna thamani hata kidogo. Watakuua na hawatajali. Kwa nini viongozi wa upinzani muwapeleke watu kwenye kifo hali mnaelewa kiwango cha ukatili wa serikali hii?

Tuseme, watu wameandamana na baadhi kadhaa wamekamatwa na kuwekwa ndani. Je, vyama hivi vilivyoitisha maandamano vina uwezo wa kwenda kuwatoa ndani kwa kuwawekea dhamana au itakuwa kila mtu na lwake? Naelewa kiuhakika kabisa kuwa wengi kati ya watakaojitokeza (kama kweli watajitokeza) ni vijana wadogo, maskini ambao huenda familia zao hazina mbele wala nyuma na zinawategemea katika kutafuta riziki. Je mmewafikiria hao wategemezi?

Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa ya Watanzania wasioridhishwa na ukandamizaji wa demokrasia., lakini changamoto za kimaisha wanazokabiliana nazo ni kubwa mno kuwafanya wajali. Hivyo, ni wazi kuwa, watakaojitokeza kwa maandamano ni watu wachache sana, jambo ambalo litarahisha kazi ya vyombo vya dola ya kuwashughulikia.

Na baada ya kushughulikiwa kikatili, naamini vijana hao hawatarudia tena kuandamana. Jambo hili likitokea litaipa serikali dhalimu ya CCM ushindi wa kisaikolojia. Watasema na kutangaza duniani kote, ‘Aagh ni wakorofi wachache tu waliokuwa wakileta ukorofi.’

Ndugu viongozi wa upinzani kutoka vyama vya ACT na Chadema, jaribuni kuwalelewa watu mnaowaongoza, na tafadhalini msiwapitishe katika njia wasiyoimudu kwani wafuasi huenda wakaamua kuacha hata kuunga mkono mapambano ya kidemokrasia. Kuwafanya watu waandamane hivi sasa ni sawa na kukamua jipu lisiloiva.

Nini kifanyike? Mambo mawili ni muhimu sana. Kwanza, vyama viendelee kupaza sauti za kupinga uchafuzi wa demokrasia uliofanyika kwa kutumia vyombo mbalimbali ili kunyanyua uelewa miongoni mwa wananchi na hivyo kupata uungwaji mkono. Hoja isiwe chama kipi ni mahiri zaidi katika kuleta maendeleo bali ulinzi wa demokrasia yetu.

Pili, viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine wajaribu kushawishi jamii ya kimataifa kwanza kutotambua uchaguzi na matokeo yake na kisha kuibana serikali ya Magufuli irudie uchaguzi baada ya kufanya mabadiliko ya kisheria yanayokandamiza demokrasia.

Kwa kumalizia, ni vyema kwa vyama vya upinzani kujitathmini. Baada ya kufanyiwa dhulma walizofanyiwa, Je nini wanaweza kufanya ili vyama hivi viendelee kuheshimika na kukubalika mbele za wananchi?
 
Zitto kama ana vidhibiti vya kuchezewa rafu anaweza kwenda mahakamani.

Kabla hujaandamana jiulize;

1. Je, lengo lako ni kupindua serikali iliyoko madarakani? Kama ndio, je uko tayari kupambana na vyombo vilivyowekwa kisheria kuilinda serikali isipinduliwe? Je, uko tayari kukabiliana na kesi ya uhaini?

2. Nini unategemea kitatokea baada ya hayo maandamano? Kama ni uchaguzi mpya, je nani ataitisha huo uchaguzi na kwa mujibu wa sheria ipi? Kama ni tume mpya, je nani ataiunda na kwa kutumia sheria gani?

3. Je, una uhakika watu wote wanaokuja kuandamana wana lengo lilelile unalofikiria wewe kichwani? Hakuna mtu anayetaka kutumia maandamano hayo kufanya uhalifu? Iwapo watakuwepo wahalifu, je uko tayari kuwa sehemu ya watakaochukuliwa hatua ya uhalifu?
 
ni maandamano yasiyo na kikomo, hawawezi kuweka nyomi za watu magerezani wala kuua nyomi za watu, matokeo yake ni muafaka wa tume huru na uchaguzi kurudiwa.
Ni rahisi kuiweka kinadharia...wait until people are gunned down.
 
Ni rahisi kuiweka kinadharia...wait until people are gunned down.
Bila ya kufanya maandamano ya amani, nakuhakikishia watu wataumizwa na kupotea sana kipindi hiki pengine kuliko nyakati zote zilizowahi kutokea. Madikteta wana tabia ya kupima upepo kwanza..
 
Lolote unalofanya hapa duniani lina pande mbili positive na Negative,Ukitaka kuandamana andamana tu wala usijiulize, sana, ila jikumbushe swala moja tu je kwani wao wataishi miaka 200? Mkapa kawaua wapemba wengi 2001 Leo hii yuko wapi?2/11/2020 na kuendelea
 
Zitto kama ana vidhibiti vya kuchezewa rafu anaweza kwenda mahakamani.

Kabla hujaandamana jiulize;

1. Je, lengo lako ni kupindua serikali iliyoko madarakani? Kama ndio, je uko tayari kupambana na vyombo vilivyowekwa kisheria kuilinda serikali isipinduliwe? Je uko tayari kukabiliana na kesi ya uhaini?...
Hahaha unaakili wewe?! Mahakama ya ccm upeleke kesi kuilalamikia CCM!

Mtawala hakuingia madarakani kisheria, sasa vyombo vya kisheria vinamlindaje mvamizi?!

Ukiwa juu ya sheria, wewe ndiye unatunga sheria, wewe ndiye unaadhibu wavunja sheria uluzowatungia.

Wailo juu ya sheria hata huwa hawaapi, unaapa kwa nani na ili iweje?! Labda kama ni kuzuga tu.

Mungu hawezi kuapa
Kuwatumikia malaika na viumbe aliowaumba na kuwatawala, ni kinyume chake ndiyo iawezekana, yani malaika, binadamu na viumbe wote wanaweza kuapa kuwa watiifu kwa Mungu.
 
Siku Lisu alipotua nchini kulikuwa na tishio la Serikali kuwa ole wao watakaoandamana. Maelfu walijitokeza, waliandamana. Hakuna cha taarifa wala kibali cha Polisi. Serikali/polisi waliwafanya nini?

Pamoja na ukatili wa serikali hii, hawana ubavu wa kuzuia maandamano kwa sababu jamii ya kimataifa ipo na wananchi. Na wanajua ninj kitatokea kama wakiwaua au kuwajeruhi wananchi.

Tuache woga, tuandamane kwa maelfu. Na tayari wamekwishaonywa ole wao wapige mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali na tume ya uchaguzi imeziba Sana masikio TUNASEMA FUTEN UCHAGUZI HAMSIKII SASA NASEMA NA NAUNGA MKO MAANDAMANO YA AMANI YASIOKUA NA KIKOMO

kiongonzi mwenye uchungu na nchi yake lazima kutii bila shurti hisia za watu wake na Kama hawezi basi sio kiongonzi sahii,Sasa tz tuna kata ngapi na mtawezaje yazuia,ngoja tuone ,NARUDIA NAUNGA MAANDAMANO MKONO ,Kama kulia hacha tulie wote labda tutaheshimiana vizuri
 
Me nadhan kabla ya kuandaman angalia kwanza wategemez wako unawaachaje then uende kwenye maandamano
 
Uchaguzi kurudiwa ni ndoto ya mchana. Kwanza hatuna pesa za kuchezea hivyo. Tumeshachaguzi viongozi sasa ni kuchapakazi tu.
 
Ni rahisi kuiweka kinadharia...wait until people are gunned down.
Usitutishe jombi na hii ID yako nyingine. Wewe siyo huyu hapa: YEHODAYA?

Kuandamana ni haki yetu. Kwamba ni wakatili ndiyo tuwaachie mafisi bucha? Looh! Kwani u coward ni nini basi?

Mbona mnataka kututisha tisha sana huku mkijua wazi kuwa uchaguzi mmekwiba?
 
Hahaha kwani maandamano yanaanzia wapi na kuishia wapi, na nini theme ya maandamano?!
 
Uchaguzi kurudiwa ni ndoto ya mchana. Kwanza hatuna pesa za kuchezea hivyo. Tumeshachaguzi viongozi sasa ni kuchapakazi tu.

Kwa hiyo mlipanga mkwibe haraka haraka ili mseme pesa za kurudia uchaguzi hamna Ila wanufaika muwe nyie?

Akili ya kuku kweli kweli.

Ila, hili litawatokea puani inshallah.
 
Back
Top Bottom