Tumeumbuka! Shilole na Vanessa wameonyesha Watanzania tulivyo wambea!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ukinitoa Mimi tu humu na baadhi wawili watatu hatumo kabisa katika huo mkumbo wa " UMBEA " ambao umewakumba members wengi humu juu ya SAKATA zima lililokuwepo hapo kabla.

Ni kwamba wiki mbili zilizopita members humu walikuwa WAKIJADILI na KUKUZA sakata la Wasanii wa Muziki wawili ambao ni MAARUFU hapa nchini Tanzania Shilole na mwenzie Vanessa ambapo kila Mtu humu alikuwa " akitiririka " anavyojua huku wengi wetu ( wenu ) mkiwa MNASHADADIA tu pasipo hata kujua nini kilichopo na wapo wale wenzangu na Mimi ambao na wao walikuwa wakijifanya KUCHANGIA wakati hata hao Wasanii wenyewe HAWAWAJUI.

Kuna waliokuwa wakiponda huku wengine wakisifia ilimradi tu kuchochea BIFU la hawa Wasanii lizidi kuwepo.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ni kama vile WAMBEA, WAPASHKUNA na WANAFIKI wote mmeumbuliwa ambapo juzi hawa WASANII walijitokeza hadharani na kusema kiuwazi kabiasa kuwa nawanukuu " KIUKWELI WALA HATUKUWA NA BIFU LOLOTE LILE NA TUNAHESHIMIANA NA KUPENDANA SANA ILA TULIAMUA TU KUFANYA HIKI KITU TUKIWA TUNA PROJECT AMBAYO LEO TUNAILETA KWENU LAKINI PIA TULITAKA KUJUA NI JINSI GANI WATANZANIA NI MASHABIKI WA KUPENDA BIFU KULIKO HATA KUNUNUA CD's ZETU " mwisho wa kuwanukuu.

Na kwa mujibu wa akina SHILOLE na VANESSA wamegundua yafutayo kutoka kwa Watanzania na ni mambo ambayo kiukweli inabidi Wewe UNAYEJIJUA ni MBEA, MFITINI na MNAFIKI wa KUTUKUKA uyaache kwani yatazidi tu kukuumbua. Wamegundua kuwa:

  1. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA ni WAMBEA.
  2. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA ni wapenda MAJUNGU.
  3. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA ni WACHOCHEZI wa UHASAMA.
  4. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA ni WANAFIKI.
  5. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA ni WAKOROFI wa KUTUKUKA.
  6. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA hawana HOFU ya MUNGU.
  7. % kubwa ya Vijana / Mabinti wa TANZANIA wana WIVU na CHUKI.
Mwisho naomba kuuliza wale MEMBERS ambao walikuwa WAKIKESHA humu " kutiririka " juu ya hawa akina SHILOLE na VANESAA bila kumsahau yule muanzisha UZI je hizo sababu zao KUU saba ( 7 ) hapo juu ZINAWAHUSU au WAMEWAONEA tu kama siyo KUWASINGIZIA?

Naomba kuwasilisha na karibuni.
 
Wambea si wao wenyewe kwan clip za video zilizokuwa zikitembea hapa mitandaoni tuliwaomba wazitengeneze ..??
au hawakujua nn kitatokea kwa wabongo.

Pleease..!! Tunawaomba wasanii wetu wasitufanye sisi wajinga.
 
kwa tulioukua tukijua kwamba wanatafuta kiki tokea mwanzo.. na kiingereza sio ishu ya kugombana labda uwe zezeta au punguani tunasema "yeeeeeh" #mixiology
 
Back
Top Bottom