Tumetoka mbali: waliowahi kulipishwa kupiga picha daraja la Manzese ni wakati wa Kudai Chao

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Miaka hiyo sisi tuliozaliwa mjini tulikuwa tunapata shida sana na watu wa mkoani. Wakifika Dar Kuna maeneo Matatu itabidi uwapeleke.
1. Uwapeleke soko la Kariakoo
2. Uwapeleke Ferry wakashangae meli
3. Usisahau kuwapeleka daraja la Manzese wakapige picha.

Ilikuwa ni usumbufu sana. Maana mgeni akija kama ni umri wako au kakuzidi kidogo wewe ndo unachaguliwa kumpa hizo tours.kwa sisi ambao tulikuwa hatupend kutembea tembea tulikuwa tunakwazika sana.

Ndo wajasiliamali wakagundua kuwa pale manzese mtu akitaka kupiga picha kwa camera yake basi analipia lile daraja na ama sivyo apige picha kwao maana wao ndo wameidhinishwa na serikal kupiga picha raia.

Aisee... Watu walikuwa wanalizwa sana kwa mtindo huu. Walikuwa wanalipa tsh 200-500 kwa kutumia daraja lile. Ilikuwa mida flan ukipita unakuta kumejaa sana watu kule juu wakiweka pozi mbalimbal wakipiga picha.

Nawashaur sasa ni wakati wa kuenda kudai hizo pesa kwa wahusika... Maana kuna siku nlimwona jamaa mmoja alitekuwa akipenda kuulamba na tai na kofia zile za ki cow boy umri umeenda bado yupo pale na camera yake. Waswas wangu na haya madaraja ya mwendokasi yanaweza tumika kijasiriamali.

Wakumbuke jamaw zako mbalimbali ambao sasa wanatamba mjini ila walipofika chuo miaka ile lazima waliomba ukawape tour maeneo hayo.wape hi tu kishkaj.
 
Nashukuru sana... Nadhan ntafika huko siku moja. Maana dodoma,singida,tabora,shinyanga na mwanza nimefika sana. Sijajua hiyo maswa ipo mkoa gani ila huwa nahisi ni kanda ya ziwa kama sijakosea.

Karibu Maswa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom