Tumetoka mbali: Unawakumbuka watu hawa na mambo haya?

Mkuu heshima mbele...
Kweli umenikumbusha mbali saaana, lakini inawezekana vipi ukamzungumzia marehemu Momba kisha ukamsahau Hassan Rehani?
Au ukamzungumzia kalala mbwembwe ukawaacha watu kama dr remmy, bushoke, na Cosmas?

Mkuu Gang Chomba,

Nafikiri Balantanda amezungumzia wale ambao tayari ni marehemu. Hao unaowataja wewe bado wako hai!!!

Mkuu Balantanda, heshima mbele mkuu, nimekuvulia kofia, kumbukumbu yako ni kali!!!

Kuna huyu mchezaji wa pamba ambaye alikuwa mzuri sana kwa kupiga penalty. Alikuwa hasogei hata hatua moja nyuma kutoka kwenye mpira lakini hakuna golikipa aliyewahi kudaka penalti yake wala yeye kupiga nje. anayemkumbuka huyu mchezaji atupe jina lake. Nimemkumbuka, alikuwa anaitwa Mao Mkami. Kwa penalti kiki alikuwa mwisho.

Tiba

Tiba
 
Hahaaaaaa,umenikumbusha kuhusu mkulu OLE..Mzee MAYUKU unamkumbuka lakini???..R.I.P John Kaduma

Mkuu,

John Kaduma (Marehemu) alikuwa msanii mzuri sana wa kuchora katuni lakini bahati mbaya alikuwa anavuta sana bangi ambayo nafikiri ilichangia kifo chake. RIP John Kaduma

Tiba
 
Aisee..hili sikulijua kabisa..Kumbe John Kaduma alikuwa ni muendelezaji tu wa vitu vitamu vya marehemu Peter Ndunguru.Nashukuru sana kwa kunijuza hili mkuu

Mku
ndunguru.jpg
Philip Ndunguru (RIP)
lu umenikumbusha ya akina Chakubanga na Apollo......

lodilofa1.jpg

madenge.gif
 
Miaka hiyo mie sijui nilikuwa na enterest zipi sidhani hata kama kwetu tulikuwa na redio au santuri

asante sana mtoa mada ya kale ni dhahabu
 
daah mkuu kama ulikuwepo,basi kuna jamaa alikua mbabe wa darasa akaja kwangu nikamchapa,basi bifu lake kaandika barua ya mapenzi na jina langu kama mimi ndo nimeandika namtaka demu kwenye desk ninalokaa,halafu kaidondosha karibu na mlango wa mwalimu mkuu,halafu maza nae alikua anafundisha same shule,barua ikaokotwa ikapelekwa ofisini,baada ya adhabu ya shule maza akaipeleka tena homu ikafanyiwe remix na mdingi babu kibano cha siku hiyo sitasahau maisha.

Dah na midingi ya enzi zile ilikuwa ikishupalia kitu basi ni nongwa ama ndalilo...

Halafu zamani bwana yaani ilikuiwa ukifanya kosa nje ya home basi shua lolote hata usilolijua linakukamata na kukupa stick za kutosha,
Ila cku hizi ukimpiga mtoto wa mtu mama yake anakuja na kanga begani anakuchambaaaaaa.

Zamanii kukiwa na msiba basi mta mzima kimyaaaaaa.

Zamani demu akipata mimba basi hata kutembea mtaani aibu.
 
hahahah maadili siku hizi yamemomonyoka kwa asilimia 75 we huoni hata vitoto vikikosea shuleni vikachapwa wazazi tunafunga vibwebwe na kuelekea skuli kuporomosha mvua ya maneno
Vitoto kubeba mimba ni ufahari
Misiba imekuwa jambo la kawaida kabisa
 
Dah, mkuu mtoa mada na wote mliochangia, hakika mmenitoa machozi kwa kadri nilivyokuwa nikipitia michango na mawazo yenu. Nimekubali kuwa ya kale ni dhahabu na ujana ni maji ya moto. Nimekubali kuwa ardhi ni kiboko tena huwa haishibi kwa kadri ilivyomeza wapendwa wetu. Kwa kweli waliotajwa humu pamoja na kazi zao bado watakumbukwa na vizazi vijavyo hata baada ya miongo kumi. Vijana na watoto wa sasa watakumbukwa kwa lipi? Ni changamoto kweli kweli. Aksanteni sana wadau kwa kunirudishia ujana wangu japo kwa kufikiria.
 
kwa mfano kipindi kile kwenye msiba hakuna kuchekacheka watu kama wehu.

Kwenye msiba mavazi ni meusi, na mkishazika wote mtanyoa vipara.

Pindi kiongozi wa dini atakapoamuru udongo utumbukizwe ndani ya kaburi basi vilio vitatawala hapo mpk watu watazimia.
Lakini siku hizi thuubutuuuuu

Watu makaburini hawazimi cmu, mpk wafiwa unakuta wako Bar wanagida, yaani misiba imekuwa ni kama yani komunio au kipaimara...

Je mnahisi ni nini?
 
Hivi kuna yule jamaa alikuwa akiitwa Saleh Jabir yuko wapi???,jamaa nakumbuka ndo alianza kurap kiswahili kwa kuiga/kukopi nyimbo za Vanilla Ice

Mkuu nimekukubali, una kumbukumbu kama computer! Napenda sana kumsikiliza Zomboko na Kufi pale RFA kumbe kuna wataalamu wengine hapa.

Huyu jamaa kweli alikuja na mambo yake nakumbuka alirap ule wimbo wa ice ice baby wa Vanilla, Now that we found love what we gonna do with it na nyingine kadhaa.

Nasikia Saleh Jabir yupo UK na Salama huyu wa EATV ni mdogo wake.
 
Nikianza na Muziki,kwa kipindi cha nyuma muziki wa Dansi(ya ukweli) ulikuwa umeshamiri sana nchini kwetu kiasi kwamba enzi hizo redioni ilikuwa ni mwendo wa muziki wa Dansi tu.Kuna baadhi ya wanamuziki ambao kwangu mimi huwa ni vigumu sana kuwasahau kutokana na mchango wao katika kuufanya muziki wetu(enzi hizo) uwe maarufu.Binafsi siwazungumzii wanamuziki wa miaka ya 60 na 70 bali nawazungumzia wanamuziki wa miaka ya 80 mwanzoni mpaka miaka ya 90 ambao daima walinivutia na abado wananivutia kutokana na uzuri wa miziki yao,wanamuziki hawa kwa sasa ni marehemu,hivyo nimeona ni bora niitumie nafasi hii japo kwa uchache kuwashirikisha katika kuwakumbuka mashujaa wangu hawa wa muziki.Kila mtu anajua kwamba kuna wanamuziki ambao huwezi kuacha kuwataja mara tu uanzapo kuuzungumzia muziki wa Tanzania,wanamuziki hawa ni kama akina Salum Abdallah,Mbaraka Mwinyshehe Mwaruka,Marijani Rajabu n.k(Mungu awarehemu). Mimi leo nimeguswa kuwakumbuka wanamuziki hawa wafuatao:-

1.Hemed Maneti Ulaya:-Mzee mzima mwenyewe wa Vijana Jazz Air Pambamoto ,huyu
mkulu kwa kweli alikuwa ananikosha mnoo kwa utunzi na uimbaji wake kiasi kwamba
alipachikwa jina la Chiriku.Baadhi ya nyimbo(ninazozijua) ninazozipenda mpaka leo ni
kama Maria,Tambiko la Pambamoto,Bujumbura,Penzi haligawanyiki sehemu ya 1 na
ya 2 na nyingine nyingi tu.Huyu bwana alikuwa na kipaji kwa kweli.

2.Eddy Sheggy:- Huyu bwana naye alikuwa na kipaji,ukisikiliza nyimbo zake kama
Milima ya kwetu(akiwa na Super Rainbow),Penzi haligawanyiki,Ogopa Tapeli,Mwisho
wa mwezi nk(akiwa na Vijana Jazz),Nelson Mandela,Shakaza(akiwa na Washirika
Tanzania Stars,wimbo wa Shakaza aliurudia pia alipohamia Bima Lee Orchestra) au
Nyimbo za Baba Jenny na Gondoigwe(akiwa na Bantu Group) uatona ni jinsi gani naye
Alikuwa na kipaji cha kuimba.

3.Jerry Nashon Dudumizi:- Mtaalamu mwingine wa Vijana Jazz ambaye daima mimi
namkumbuka kwa nyimbo zake tamu alizotunga na kuimba akiwa na Vijana Jazz,
nyimbo kama VIP,Shoga,Theresa na nyingine nyingi tu…..

4.Suleiman Mbwembwe:- Huyu namkumbuka kwa nyimbo yake tamu ya Mama Chichi
(akiwa Vijana Jazz) na nyingine nyingi akiwa na Juwata/Ottu Jazz/Msondo Ngoma.

5.Francis(Nassir) Lubua,mtaalamu mwenyewe wa Nginde Ngoma ya Ukae

6.Tino Masinge “Arawa”….Sina la kusema hapa jamani…R.I.P

7.Ali Kishiwa Mhoja “TX Moshi William”…Aaargh,kifo jamani.Ukisikia mtu ana
kipaji TX alijaliwa hasa,sina haja ya kutaja kazi yake,inajulikana.

8.Athuman Momba:-Kifaa kingine hiki cha Vijana Jazz na Msondo Ngoma…R.I.P

9.Le supreme Fredy Ndala Kasheba:- Mzee wa ZAITA MUSICA wana ZUKE ZUKE
Muselebende,nani atavishau vibao vyake vitamu kama Marashi ya Pemba,Dezodezo
(Tshala Muana aliununua huu wimbo) ama ule wimbo mtamu wa Kesi ya Khanga
(mama nipe nauli nikamfuate Monica,amekimbilia Zambia na Treni ya mizigo,kisa cha
kukimbia madeni yamemzidi,Doti kumi za Khanga alizokopa hajalipa)….dah

10.Suleiman Mwanyiro “Computer”: Mtaalamu huy wa gitaa zito(besi) wa Nginde

11.Kalala Mbwembwe:-Huyu bwana alikuwa Tancut Almas baadaye akaanzisha bendi
ya Ruaha International,namkumbuka kwa nyimbo zake kama Lutandila,Safari n.k

12.Kyanga Songa:-Huyu bwana alikuwa na pacha wake tangu Sambulumaa,Tancut na
baadae Ruaha International

Wakuu kwangu mimi hizi ni Hazina zilizotoweka ghafla tukiwa bado twazihitaji.Tuendelee kuwataja wengine ambao nimewasahau…Sasa hivi muziki wa Dansi Bongo ni kama umejifia tu,hakuna kitu,kila kitu vijana wanakopi muziki wa Kikongo tuuuuuuuuu…..Pa1

Namkumbuka Marijani Rajabu na wimbo wake niupendao saaana aliimba..

....Mama watoto muogope Mungu wako, kwa huyo mwana asiye na baba yeye hakupenda hiyo kazi ya mola....... Kazi ya Mungu haina makosaaaaa...............
 
Halafu kipindi hicho hakukuwa na cha Kwa Fujo DJs wala Nyuki DJs..Disko lilikuwa lapigwa na maDJ wataalamu(mabitozi wa enzi hizo)baadhi yao ni kama DJ Chriss Phaby,
Young Millionaire(Jacob Usungu wa RFA),Nigger J(Masoud Masoud),DJ Joe Kusaga,DJ
Kalikali,DJ Kim,Choggy Sly,Hayati Deo Kiduduye(Super Deo???) na wengine ambao nimewasahau…Ilikuwa raha iliyoje kwa kweli wakuu

Hivi Usungu yupo wapi jamani? ............ Kipindi chake cha enzi hizo kinapwaya sana pale RFA siku hizi
 
wakati huo bwana mnanitamanisha wish na mie ningechungulia kipindi kile hata kidogo
 
wakati huo bwana mnanitamanisha wish na mie ningechungulia kipindi kile hata kidogo

Yaani ilikuwa raha hasa,hebu sikiliza maneno kama haya kutoka kwenye mojawapo ya nyimbo za miaka hiyo:-

"Oooh mume wangu eeh,ulinitaka radhi eeh,nataka oa mke mwingine wa pili,uwezo huo wa kumtunza ninao....aaah aaah matokeo ya penzi limezidi elemea kwa mke mwenzangu eeh"

"Hunijali kwa chumvi,hunijali kwa sukari,tabu nyingi ninapata na watoto heeh"

"Hunijali kwa mavazi,hunijali kwa malazi,kweli penzi haliwezi gawanyika heeh"

"Nakuomba sana mume wangu,ukumbuke japo na watoto,nakuomba sana mume wanguu ukumbuke japo na watoto"

"Hunijali kwa chumvi,hunijali kwa sukari tabu nyingi ninapata na watoto ooooh"

Huyu alikuwa ni Hayati Eddy Sheggy na Vijana Jazz katika kibao kitamu cha Penzi haligawanyiki No. 1...Yaani we acha tu
 
Ama maneno haya:

"Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo"

"Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe Viaipiii(VIP),si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,viaipiiii"

"Binadamu hanunuliwi kama nguoo viaipii,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako utanitorokaa"

"Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwakooo,kwa uzuri ulionao viaipii,natamani penzi letu liwe penzi la ndotoni,tafadhali nakusihi viaipii,nakuomba uwe wangu viaipii,ili niondokane na ndoto za mapenzi"

"Binadamu hanunuliwi kama nguooo viaipii,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako utanitorokaaa"

"Ukinikubali viaipii,mimi niko tayari,kubadili dini,ukinikubaliii viaipii mimi niko tayariiii,kubadili dini,hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipando niwe na wewe smbamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa"

"Binadamu hanunuliwi kama nguooo viaipii,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako utanitorokaaa"

"Ukinikubalii viaipii,nitatoa mahali ya mbuzi saba,ukinikubalii viaipi,nitatoa mahaliii ya mbuzi saba......"

Dah...bwana wee...Natokwa na machozi hapa jamani..Kwa kweli nilikuwa napendezwa sana na uimbaji wa Hayati Jerry Nashon Dudumizi,hasa katika wimbo wake hapo juu wa VIP akiwa na Vijana Jazz,mojawapo ya nyimbo zake za mwishomwisho kabla hajafariki..Jamaa alikuwa na sauti ya kutetemesha fulani hivi
 
Yaani live barantanda wewe ni fan wa pambamoto...
Toka ulipoanzia mpk hapa nimepata picha kamili.
 
Ila ukweli ni kuwa Tanzania hakutatokea bendi kama Nginde...
Na ntakuwa nawabwagia mistari michache ya nyimbo zao zilizopata kutikisa taifa miaka hiyo nikianzia na Telegram...

Bushoke;
Sasa naijibu telegraam nilioipata kutoka kwa mkeo oooh oooh oooh anaomba ushauri wangu, kwa kuwa maelewano yenu ndani ya nyumbaa yamekuwa madogo...
Ktk majibu niliyotuma nimemhusia mkeo ooh ooh kama ameadhimia kutorudi nyuma kimapenzi avumilie na kuomba kheri itawale shari, mkumbushane hisani msameheanee kama wazazi...

Halafu huko mbele anaimba fresh jumbe kisha Chidumule anamalizia...

Amini usiamini mke ndani ya nyumba hapigwi kwa fimbo au makofi, hupigwa kwa upande wa kanga kwani mkeo ni pambo la nyumba.....

aaaah jamani sikinde ni noma.
Ntarudi baadae kwa ajili ya kuwakumbusha vibao kama ubaya, pata potea, conjesta, christina bundara, hiba, mv mapenzi, mfaume, crala, editha, mume wangu jerry nk nk nk nk
 
Hujakosea kaka,mimi nilikuwa pambmoto damu(kama Arsenali vile)..Pia Nginde ndo usiseme nilikua mnazi mkubwa pia
 
Ila ukweli ni kuwa Tanzania hakutatokea bendi kama Nginde...
Na ntakuwa nawabwagia mistari michache ya nyimbo zao zilizopata kutikisa taifa miaka hiyo nikianzia na Telegram...

Bushoke;
Sasa naijibu telegraam nilioipata kutoka kwa mkeo oooh oooh oooh anaomba ushauri wangu, kwa kuwa maelewano yenu ndani ya nyumbaa yamekuwa madogo...
Ktk majibu niliyotuma nimemhusia mkeo ooh ooh kama ameadhimia kutorudi nyuma kimapenzi avumilie na kuomba kheri itawale shari, mkumbushane hisani msameheanee kama wazazi...

Halafu huko mbele anaimba fresh jumbe kisha Chidumule anamalizia...

Amini usiamini mke ndani ya nyumba hapigwi kwa fimbo au makofi, hupigwa kwa upande wa kanga kwani mkeo ni pambo la nyumba.....

aaaah jamani sikinde ni noma.
Ntarudi baadae kwa ajili ya kuwakumbusha vibao kama ubaya, pata potea, conjesta, christina bundara, hiba, mv mapenzi, mfaume, crala, editha, mume wangu jerry nk nk nk nk

"Najua mwenzangu karibuni utatoka hospitalii,utokapo tafadhali,fika mjini mtafute mpaka umuonee mchumba wangu Clara mchumba wangu Clara"............

"Nyumbani anakoishiii ni Msimbazi Kota ukimkuta mweleze mchumba wako Kitwana anakusalimu"

"Kama atasikiaa ee,kaama atasikaa mweleze,ajali iliyonipata nimekuwa kilema,na hicho kilema kisiwe kisingizio cha kutokuja kuniona"

"Tafadhali ukimuona.......

Kaka umeutaja wimbo wa Clara hapo juu umenifanya kwa haraka niyakumbuke maneno haya(hata sijui kama nimeyaandika sawa)...Il Nginde walikuwa kiboko aisee..Huku unamkuta Cosma(Cosmas Chidumule),King Michael Enock,Hassan Rehan Bitchuka,Max Bushoke.....Nginde walikuwa wanatisha bwana

"
 
Halafu walikuwepo Orchestra Safari Sound wana Ndekule(baadae wakabadilisha mtindo wakawa wanajiita wana Power Iranda)..Hawa jamaa walikuwa kiboko nao..Sikiliza kibao kama Christina Moshi.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom