Tumeshindwa, tuombe msaada kwa wazungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeshindwa, tuombe msaada kwa wazungu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 20, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati Rais Kikwete amepokea maandamano ya kupinga mauaji ya Albino kwa kupiga mkwara wa kunyonga watu... habari ndiyo hii..

  Mtoto mmoja Albino auawa kikatili mkoani Shinyanga

  2008-10-20 18:21:20
  Na Radio One Habari

  Wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi -Albino limeingia mkoani Shinyanga kufuatia mauji ya mtoto mmoja Albino katika kijiji cha Shilela, Kata ya Segese wilayani humo.

  Mtoto huyo wa kike aitwaye Esther Charles, mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika shule ya msingi kijiji hapo ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

  Diwani wa Kata ya Segese Bwana Joseph Mayala amesema watu wasiojulikana wakiwa na mapanga usiku wa manane walivamia nyumba ya Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Mzolewa Mashili ambaye ni baba wa mtoto huyo kwa kuvunja mlago wa nyumba yake kwa kutumia jiwe kubwa.

  Amesema watu hao waliwaweka chini ya ulinzi wazazi wa mtoto huyo na kuanza kumchuna sehemu za usoni, kichwa hadi ngozi ya kisogoni na kumkata miguu yake kuanzia sehemu za nyonga na kuondoka nayo.

  Diwani huyo amewataka wananchi wakiwemo walinzi wa jadi Sungusungu Wilayani Kahama kuhakikisha watu wanaojihusisha na mauaji hayo wanafichuliwa.

  My Take:
  Tuombe msaada kwa wazungu kutusaidia kukomesha mauaji haya? Lakini zaidi siyo tu kwenye suala la mauaji haya bali usimamizi mzima wa sheria zetu kuna aina fulani ya kigugumizi au kusita kuchukua hatua za dhati.

  Leo nimeona picha ya jinsi gani mgambo wa jiji wakiwasweka kwenye makarandinga (mafuso) wamachinga maeneo ya Posta (Dar) katika kile ambacho bila ya shaka wanaamini ni kulisafisha jiji. Lakini hadi sasa hatujaona jinsi gani waliochafua nchi kwa ufisadi wao hawajasweka kwenye makarandinga zaidi ya kusubiri maelezo ya kuwa "very soon, watachukuliwa hatua".

  Ni wazi tumeshindwea kusimamia sheria zetu wenyewe hasa zinapokuja kwenye masuala yanayohusu mambo makubwa zaidi; tumeshindwa kufanya mambo mengi ambayo jamii yoyote inapaswa kufanya yenyewe. Vile vilivyo msingi tumeviweka pembeni na tumeng'angania vya sekondari.

  Je kuna ubaya gani tukiomba timu ya waendesha mashtaka toka Commonwealth, kuna ubaya gani tukiomba timu ya wahandishi kutoka Japani au Ujerumani kusimmamia infrastructure development? Kuna ubaya gani tukakubaliana na vyuo vikuu mahiri duniani vikatuendeshea UDSM au Mzumbe n.k na kugeuza vyuo vyetu kuwa World Class Higher Education institution?

  Kama hatuwezi kufanya kitu na tunajua hatuwezi (licha ya kujibaraguza) kwanini tusiombe msaada kwa wale wanaoweza? Hata Nyerere wakati wa maasi ya 1964 aligundua kuwa pamoja na uzalendo wake wote asingeweza kuzima uasi bila msaada wa Waingereza. Je tuwaombe tena wazime uasi unaochochewa na ufisadi?
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama tungeamua kuwa serious, report ileya Vick ilikuwa sehemu nzuri ya kuanzia vita hii na kwa keli kama tungekuwa tumeamua kupambana, tungekuwa tumefika mbali sana.
  Nadhani hatujashindwa kiasi cha kufikia kuomba msaada kwa wazungu katika hili; tatizo ni kuwa hatujaamua kulishughulikia ipasavyo
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mimi nadhani tumeamua kulishughulikia na uwezo wetu umefikia kikomo. JK alilizungumzia suala hili mapema mwaka huu na limerudiwa mara nyingi, tumeona juhudi zao (kama alivyoelezea kwenye hotuba) lakini at the end, hatuna uwezo wa kulishughulikia vinginevyo kwanini watu wanafanya mambo haya with impunity?
   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  JK ana uwezo wa kushughulikia chochote? Maneno mengi, utendaji sifuri.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Oct 20, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Oh no, sisi Sivyo Tulivyo kwa hiyo hamna haja ya kuomba msaada kutoka kwa wazungu....
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji! JK na Said Mwema wake hawajashindwa... ila hawataki au hawaoni umuhimu wowote wa kufanya hivyo.. kwao huu ni wakati wa ku-relax na kutesa...
  OMBI LANGU KWA WANA JAMII FORUM.... Tuwasadie ma-albino wote wa Tanzania kupata hifadhi ya ukimbizi nchi za nje hasa Ulaya na USA. Najua wengi wa ma-albino hawajui wafanye nini ili wapate hadhi ya ukimbizi ambako wataishi maisha ya raha bila hofu. Hili ndilo lililobaki.
   
 7. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siku zote nimekuwa nasema watu wanapoua vibaka wa simu, lazima wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ASAP sababu Human Life is Sacred. watu wengi wamepinga na kusema ni sawa tu acha vibaka wauawe sababu polisi hawafanyi kitu. viongozi wa serikali nao wamekaa kimya sababu hawaoni thamani ya maisha ya hawa vibaka.

  Serikali inasahau kuwa binadamu mkishaanza kuua vibaka na kuona powa tu, mmomonyoko huo unaslide mpaka kuua mtu sio issue tena. Wameamia kwa albino, soon itakuwa kwa watu wa aina nyingine.

  Nakumbuka wakati tuko wadogo ilikuwa vigumu sana kusikia mtu ameuawa Tanzania, lakini siku hizi hata watu hawashtuki. Tunakoenda kubaya
   
 8. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kuna miaka nadhani katikati ya 80's kulikuwa na tatizo la watu
  wenye "upara" kwani walionekana dili sana na kulikuwa na
  fununu mitaani kwamba walikuwa wanauawa. je hili lilikabiliwaje?

  aidha lile suala la watu kuchunwa ngozi mkoani mbeya
  nalo lilikabiliwaje?

  je mikakati iliyotumika katika suala la vipara na ngozi haiwezi
  kutumika kwenye suala la albino?
   
 9. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ile ya kuuza vichwa vyenye upara ilikuwa utapeli wenye msingi wa kishirikina, na ilikufa yenyewe baada ya "wafanyabiashara" wa bidhaa hiyo kutapeliwa sana. Utapeli huu ulianza nchi za west Africa hasa Nigeria na Cameroun, lakini walioileta Kigoma hii kitu walikuwa wasenegali kwa kupitia Burundi (hasa kwa sababu ya urahisi wa maelewano kwa lugha ya kifaransa). Ilikuwa hivi:

  Matapeli wawili wanaoshirikiana wanaingia mjini, na kuishi vitongoji tofauti huku wakionekana mbele ya jamii kama hawana uhusiano wowote wala hawafamiani. Katika wawili hao, mmoja atajifanya anatafuta kichwa chenye kipara na atatangaza tenda hiyo kwa njia za chinichini iwafikie wenye tamaa ya hela. Yule tapeli mwingine atasubiri habari ya biashara hiyo ienee, kisha ataanza kujinadi hivyohivyo kichinichini kuwa ana kichwa cha binadamu lakini hajui pa kukiuza (na ni kweli anacho). Sasa ukiwa na tamaa ya fedha utaenda kwa yule anaetafuta kichwa utamuuliza atanunua kwa bei gani? Anaweza kukutajia hata milioni 10. Ukienda kwa muuzaji ukimuuliza anauzaje, anakuambia milioni 5 (kwa tamaa unaona hapo iko faida!). Kama unayo hiyo milioni 5 ukinunua hicho kichwa ili ukipeleke kwa "mteja", jamaa wanawasiliana kuwa umeshalipa hela, wanatokomea! Ukifika kwa aliyekuagiza unakuta alishatambaa zamani! Na hivyo hivyo ukifanya ujinga ukaenda kuua mtu, unapomjulisha "mteja" wako kuwa unaleta kichwa, wanawasiliana kuhakikisha kama kichwa hicho ni kile walicho nacho. Wakijua ni kipya pia wanatoroka, kwa hiyo muuaji unabaki na "mzigo" wako wa kichawi! Kwa hiyo kwa vyovyote mwenye tamaa atatapeliwa tu, akinunua kichwa anabaki nacho, na akiua mtu bado pia anabaki nacho, hela hakuna! Na anayeachiwa kichwa kwa mtindo huo alikuwa hathubutu kusema, kwa hiyo matapeli waliweza kuendelea na kazi hiyo kwenye mitaa na miji mingi. Sasa baada ya watu wengi kutapeliwa na kubaki na vichwa vya watu visivyokuwa na mnunuzi, ile biashara ilikufa.

  Inawezekana hili suala la albino ni hivyo hivyo, huenda ni matapeli wamewekea "price tags" kwenye viungo vya albino. Na kama kuna aliyeua albino akaishia kukosa "soko" au kuachwa solemba na bidhaa, hawatathubutu kujitokeza maana ni siri. Lakini kikubwa wanaouvaa mkenge hapo ni "madalali", ananunua jicho la albino kwa milioni 2 ili akaliuze milioni 5, kumbe "mteja" aliyemtuma na "muuzaji" wa awali wako pamoja! Akifika kwa mteja anakuta alishatoweka, anabaki na jicho la albino ambalo hajui pa kulipeleka, anaanza kutafuta mwingine wa kumtapeli nalo.

  Serikali ikitaka kutokomeza hili jambo inaweza, na pa kuanzia ni kwa wanunuzi wa hivyo viungo ambao wako mitaani kwetu, tunaishi nao. Polisi wa upelelezi na hata watu wa usalama wakitaka kutumia mbinu za kiintelligensia kuwasaka na kuwakamata wote hao wanaweza, unless mtu aniambie jeshi letu la polisi na watu wa TISS hawana mbinu hizo! Zile nguvu kazi walizopeleka Chunya kuwasaka waliomrushia mawe Mwankupili, zingetosha kabisa kuwasaka na kuwatia nguvuni wanaoua albino!
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama Vicky Mtetema aliweza kufanya attempt hii ...sidhani kama TISS na Polisi upelelezi (CID) hii kazi inawashinda....ni kuwa hawajaamua au wanasubiri waambiwe na wakubwa ndio waone kuna tatizo.
   
 11. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nikushangaze! Hata hao polisi upelelezi na TISS ukiwawekea dau la milioni 2 kwa kichwa wakuletee watu wanaouza viungo vya albino, nakuhakikishia utaletewa watuhumiwa, exhibits na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani. Ni njaa tu zinatesa watu. Hii mbinu ya kutangaza dau mbona hata nchi za wazungu (huko tunakoiga mambo mengi) huwa zinatumia kukamatia wahalifu sugu au korofi.
   
 12. k

  kaiyurankuba Member

  #12
  Oct 20, 2008
  Joined: May 16, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafasi ya uchawi na ushirikina katika tanzania bado ni kubwa. Walioenda shule wamo na wasioenda shule wamo pia, walio na dini wamo na wasio na dini wamo pia! ni vigumu kwa askari/hakimu/mtawala anaye amini katika kutoa kafara ili 'afanikiwe kikazi/kibiashara' kuchukua hatua dhidi ya uhalifu wa aina hii! ni vigumu kwa watu walio enda mlingotini' ili washinde uchaguzi kuweza kuchukua hatua zinazostahili kukomesha mauaji ya albino!!nani atamfunga paka kengele?

  unyanyasaji wa maalbino ( i actually mean persecution!) tanzania haujaanza leo. look at ukerewe. kisiwa cha ukerewe kinajulikana dunia nzima kwa kuwa na 'highest concentration of african albinos in the world'. how come? because it was 'the dumping ground' of unwanted albinos from all over the great lakes region of africa! kuwapeleka maalbino kuishi uhamishoni ulaya na marekani maana yake nini? manake tumeshindwa kuishi kwa upendo na hawa ndugu zetu? it means we have failed to provide a secure environment in which they can live and realize their full potential and contribute to the development of our country?

  Hatujashindwa bado! na hatuwezi ku export hili tatizo kwa wazungu it will be an admission that indeed we are worst than animals! may be thats who we are Mr JK? Where are you?
   
 13. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kithuku
  Nimependa ulivyofafanua, ila para ya mwisho ningetaka kuelewa kama nimeelewa vyema. Unamaanisha Chifu Mwangupili a.k.a Chakubimbi ametumia madaraka yake vibaya kwa kupeleka vikosi kusweka rumande waliorushia magari mawe badala ya kutumia nguvu hiyo kukusanya wanaoua Watanzania wenzetu? Je unamaanisha ufinyu wa kufikiri wa huyo mkubwa ndio unasababisha yanayotokea kwa Watanzania wenzetu albino? Kama majibu ya moja na mbili ni ndiyo... mkuu kula kumi zooote
   
 14. N

  Nsunza Member

  #14
  Oct 21, 2008
  Joined: Jan 21, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio dau tu, watu hao wakamatwe washitakiwe ikiwezana wapatiwe "capital punishment" Na jeshi letu la polisi linaitaji kusafishwa maana utendaji wake wa kazi ni mbovu na linaongozwa na watu wengi ambao hawajasoma. Ndio maana ukiangalia ramani ya Tanzania, Dar ni ndogo sana lakini hata amani hakuna!Majambazi wana vunja benki kilasiku. Halafu unazungumza maendeleo! Sijaona raisi mwenye mtazamo mdogo kiasi hiki! Anajiita mchumi! Huu ni upuuzi! Kikwete asafishe na kuwapromot watu walio soma kwenye ngazi zote and stop this seniority BShit!!!
   
 15. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #15
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukiaona nchi imefikia hapa ujue kuna tatizo kubwa sana. Kwanza lazima tujiulize inakuwaje watu badala ya kutafuta pesa kwa njia ambazo ni halali na kwa kufanya kazi kwa bidii iweje leo wanatumia njia za ushirikina ili waweze kuwa matajiri?
  Kwa mtizamo wangu kama watu waliopewa madaraka wanafanya ufisadi wa kupindukia na wanatoka unafikiri huyu mtu wa kwaida ili na yeye aweze kuwa mtu katika jamii atapitia njia gani ya mkato?
  Ikiwa Proffessa, Daktari, Mwalimu na wanataaluma wanaacha kazi zao na kuingia kwenye siasa ili waweze kufaidika na shortcut ya ufisadi sembuse Masanja kule kijijini shinyanga ili naye atoke kwa haraka na kupata pesa ili naye siku moja awe kigogo the only shortcut atakayouitumia ni kama hizi za kuua maalbino.

  Jamani hili swala la mauji ya maalbino is more than ushirikina . Watu wamekataa tamaa hata kufikiri kunawashinda na kuamua kutafuta mkato wa ushirikina. Jamani wale wataalam wa sayansi ya jamii na wachumi naoomba umtupe perspective yenu!!
   
 16. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #16
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuongelea dau sawa lakini itakuwa ni temp. solution! Tatizo ni la kiuchumi zaidi!
   
 17. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160


  Kithuku;
  Nashukuru sana kwa mchango wako na pia umenigusa sana kwa maelezo yako ya ufafanuzi mzuri kabisa kuhusiana na biashara ya vichwa, na namna ulivyoweza ku-hypothesize kujaribu kui-link na hii ya sasa hivi, ambayo ndiyo the worst case ever.
  Mimi najaribu kufikiria kuwa: kwa nini tusi-assume kuwacase ya sasa ya alibinos ni sawa na ile ya mwanzo ya watu wenye vichwa vyenye vipara, halafu tuziombe media (Television, Radio, Magazeti) ku-air hizi information kuwa kuna utapeli tu unafanyika kujaribu kuwaibia watu kijanja? Kwa sababu kama hypothesis hii itakuwa true, then tutakuwa tumesolve problem. Au hata serikali iitishe hata press conference kupitia wizara husika, ieleze haya kwa waandishi wa habari ili hizi taarifa ziweze kusambazwa nchi nzima. Watau wengi najua hatukuwa tunaelewa hata kilichokuwa kinaendelea kuhusiana na hii biashara ya watu wenye vipara, km alivyoeleza kithuku, mimi mwenyewe nikiwa mmojawapo. Tusipofanya hivyo, keshokutwa lazima zitakuja kuzuka biashara nyingine katika mtindo huu huu, labda ya wanawake wenye udevu, wanaume wenye mwanya, wasichana wenye shingo ndefu, nk. nk. nk.
  Capacity ya nchi yetu ina uwezo wa kushughulikia mamtatizo makubwa sasa, ukilinganisha na hili amabalo ni dogo sana kiutendaji, lakini very sensitive and touching. Jamani tatizo hili liko ndani ya uwezo wetu kabisa, tunachotakiwa ni kushirikiana just one day, the next day litakuwa limekwisha kabisa!
   
 18. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii habari niya kusikitisha sana...naona kuna haja ya kumpeleka JK kule
  THE HAGUE kama ataendelea kupuuzia mauaji ya ndugu zetu hawa.

  Wembe.
   
 19. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi huyo mganga aliyekuwa exposed na Vicky Mtetema amekamatwa? Inabidi tuanzie hapa...Ifanyike operesheni ya kuwakamata na kuwaweka ndani waganga wote wa kienyeji wanaodai viungo vya albino, ngozi ya binadamu nk...hawa ndio chanzo cha vitendo hivi kwa hiyo tukianza na hawa tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana.
   
 20. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kwamba wachawi wamevishinda vyombo vya dola? shame on us!
   
Loading...