Tumeshindwa Tunalazimisha kukubalika kwa Nguvu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Yawezekana Watanzania tuna "Mind Crisis Syndrome Disease(MCSD)" na hii hutupelekea kushangilia kila jambo, kuunga mkono kila jambo na kutofanya tathmini ya kile tunachokiunga mkono na kushangilia!
-----------------------------------
Hii inajidhihirisha pia hata kwenye matamko yetu ya kuhama vyama nayo yana Crisis na lack of authority! Mwakilishi wa wananchi anasema anahama chama kwa sababu "fulani" anatekeleza ahadi zilizokuwa ndio agenda yake, nonsense! Ulitegemea atekeleze nini? Huo si ndiyo wajibu wake na wako?

Kutekekeleza ahadi ni wajibu wa msingi wa kimkataba kati ya Kiongozi(Serikali) na Mlipa kodi(Umma- Wananchi). Ni ujinga kabisa tena wa kiwango duni kabisa kuwahi kutokea kudhani kwamba kuna mtu mmoja anatekeleza ahadi kama hisani na kama vile financing ya utekelezaji wa ahadi hizo unatoka kwenye mfuko wake! Huu ni uzwazwa wa hali ya juu sana!.

Governance ni coordinated and integrated duty. Na kwa msingi huo huwezi kuona matokeo chanya ya uwajibikaji huo kama mtu mmoja anafilisi akili za watu wengine!

Ninachokiona kwa karibu ni kwamba, hama hama na jitihada kubwa za kuwarubuni wapinzani wasio na fikra pevu ni kutaka kutengeneza justification ya kukubalika hasa pale uchaguzi wa marudio utafanyika na kama ilivyo ada uporaji wa matokeo nje ya [HASHTAG]#ballotpapers[/HASHTAG] ndiyo umekuwa mtindo mpya wa demokrasia katika taifa letu!

Kimsingi tuseme ukweli kwamba utawala huu unalazimisha kukubalika pasipo kuonesha dhati ya utendaji na uwajibikaji unaoweza kuleta ustawi wa maisha ya watanzania.

Kuwarubuni wanasiasa kuhamia chama chako tena kwa gharama kubwa hakuondoi ugumu wa maisha ya mtanzania, sana sana kunazidi kumuongezea adha na taabu kubwa!

Kwanza, ni muhimu nikaeleweka kwamba mtu kuhamia chama kingine ni HAKI yake ya MSINGI kabisa na hahitaji mjadala. Hoja TATA ni namna gani huyo mtu kahama toka sehemu moja kwenda nyingine! Ameshawishiwa? Amerubuniwa? Au amehama kwa hiari yake mwenyewe kwa kuchoshwa na aina fulani ya ghiriba za watawala wasioishi kwa kile wanachokihubiri?

Pili, ijulikane kuwa kwa mwakilishi wa jimbo ambaye kimsingi anahama chama kwa sababu za kijinga kabisa na hasa kwa kununuliwa au kwa njia yoyote ya hovyo huyo mtu ni [HASHTAG]#LAANA[/HASHTAG] na [HASHTAG]#MKOSI[/HASHTAG] kwa jamii ya watanzania wote ikiwemo waliomchagua kuwawakilisha kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa nini nasema hivyo? Ni ukweli usiotia shaka kwamba mzigo wa fedha za kugharamia uchaguzi mpya wa marudio utatokana na fedha za mlipa kodi mtanzania! Huu ni mzigo unaobebeshwa watanzania bila sababu yoyote! Alaaniwe anayewarubuni wawakilishi hawa na alaaniwe pia mwakilishi huyu mwenye akili ya Kikunguni!

Kwa mfano; unahamaje kwa kuhongwa na/au ahadi ya kulipiwa madeni yako unayodaiwa? Ni jambo lisilokuwa na fikra pevu hata kidogo!

Watanzania tudai KATIBA mpya! Tuamke tudai Katiba na Tume huru ya Uchaguzi!

[HASHTAG]#AmkeniTuaamke[/HASHTAG]!
[HASHTAG]#Tusinyamaze[/HASHTAG] [HASHTAG]#Tusiogope[/HASHTAG]!
 
Mtanyooka tu.
Mmeshaingizwa kichinjioni, naona mko bize kujihami! Mko kwenye defensive mode kilankukicha.
 
Kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi nipo na nyie ila Hili la kuwatetea Mafisadi na kuwapa front seat kwenye Chama sipo na nyie
 
kinachouma ni yule fisadi kipara anaedhulumu kwa kigezo cha kodi..
halafu senti hizo alizonyang'anya anaenda kuhongea eti ionekana anakubalika
limbukeni..
kwanza ni kiongozi batili maana alisukumizwa kwa bao la mkono..
 
Hao wanaohama vyama, siyo kweli wanahama kwa sababu wanazozisema kwa sababu hazina maana. Kujiunga na vyana vya upinzani hakumaanishi tu kwamba chama kilichopo madarakani hakitimizi majukumu yake. Kwa kuwa hata ukiyaona yanayofanykika kinyume upinzanini, bado huna uwezo wakuyarekebisha badala yake utabakia kukosoa.

Pamoja na yote, kwa mauaji na chuki dhidi ya viongozi wa upinzani kwa sasa, ninapata ujasiri kusema hawa wanaorudi ccm, wanarudi kule kwa unafiki ii wasiuawe.

Wameshajua, ukiwa ccm wewe unaweza kufanay lolote hala baya, na hakuna mtu wa kukuchulia hatua. Lakini pia, unapendelewa na pia unalindwa na huitwi adui.

Mungu aichunguzaye mioyo, anajua nia za wote hawa. Laini pia yawezekana Mungu anaona UKaWA ni jeshi kubwa kuliko analohitaji kwa ukombozi wa taifa. Wait and see!
 
Fisadi yupi? Mafisadi wote wapo CCM pesa za Umma zinatumika kuwanunua Wapinzani huo ni Ufisadi pesa za walipa kodi badala ya kufanya maendeleo zinatumika kuwanunua Wapinzani.
 
Hao wanaohama vyama, siyo kweli wanahama kwa sababu wanazozisema kwa sababu hazina maana. Kujiunga na vyana vya upinzani hakumaanishi tu kwamba chama kilichopo madarakani hakitimizi majukumu yake. Kwa kuwa hata ukiyaona yanayofanykika kinyume upinzanini, bado huna uwezo wakuyarekebisha badala yake utabakia kukosoa.

Pamoja na yote, kwa mauaji na chuki dhidi ya viongozi wa upinzani kwa sasa, ninapata ujasiri kusema hawa wanaorudi ccm, wanarudi kule kwa unafiki ii wasiuawe.

Wameshajua, ukiwa ccm wewe unaweza kufanay lolote hala baya, na hakuna mtu wa kukuchulia hatua. Lakini pia, unapendelewa na pia unalindwa na huitwi adui.

Mungu aichunguzaye mioyo, anajua nia za wote hawa. Laini pia yawezekana Mungu anaona UKaWA ni jeshi kubwa kuliko analohitaji kwa ukombozi wa taifa. Wait and see!
Pesa inayotumika kuwanunua Wapinzani, pesa inayotumika kurudia uchaguzi ni pesa za walipa kodi huo ni Ufisadi mkubwa pesa za Umma inayotumika kwa mambo yasiyo na Tija na kama CCM wangezitumia hizo pesa kwenye kupeleka maendeleo majimboni wangevuna kura pasipo uchakachuaji wala kutumia nguvu kudhoofisha upinzani, Huo mladi wa Maliyamungu Bashite, Lipumba, le mutuz na Jerry muro kula 10% kwenye pesa za kuwanunua Wapinzani ni Mladi haramu na huenda ikaja kuwa Skendo baadae endapo Lengo walilomdanganya Mtukufu malaika toka chato halitatimia.
 
Kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi nipo na nyie ila Hili la kuwatetea Mafisadi na kuwapa front seat kwenye Chama sipo na nyie
Mafisadi wapo CCM, ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli, ujenzi Dsm Airport na chato Airport, bomba la mafuta na Gesi kote Huko Maliyamungu Bashite na wana CCM wamekula 10% kufanikisha Dili zote, Escrow, kivuko feki, mabehewa chakavu, pesa NIDA, NSSF, TTCL , ATC , kuuza nyumba za serikali, chenji ya Rada, chenji bunge la katiba vyote vimepigwa na CCM wenzako hata zile bilion 251 zilipotea kwa kuwalipa makandarasi hewa wizara ya ujenzi zimeliwa na CCM, mafisadi wote wapo CCM.
 
Wanakimbia mapigo hatari ya gizani
Acha tu hizo nafsi zao zina siri nzito
Afadhali ya mchana wanapata mwanga usiku kuna mazito
 
Mtanyooka tu.
Mmeshaingizwa kichinjioni, naona mko bize kujihami! Mko kwenye defensive mode kilankukicha.
Wewe kichinjio kinakukosa vipi? Gharama za maisha ziko juu kwa wote. Sikushangai. Mtu ukiwa ccm unawaza kwa kutumia makalio.
 
Back
Top Bottom