Tumeshindwa mtihani rahisi saaaana, tutaiweza migumu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeshindwa mtihani rahisi saaaana, tutaiweza migumu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Aug 8, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa wale waliofuatilia habari za Babu wa Loliondo, watakumbuka jinsi ambavyo baadhi yetu tulipaza sauti za kuonya kuwa dawa ya mzee huyo ilikuwa kanyaboya! Hata hivyo tulipuuzwa na kuonekana watu wa ajabu sana kwenye jamii. Kuna baadhi ya marafiki na ndugu zangu walinizuia kabisa kupinga hadharani habari ya uponyaji wa Babu wa Loliondo.

  Sasa imethibitika kuwa hakuna kitu kama uponyaji katika hiyo dawa ya Babu. Binafsi niina ushahidi wa ndugu 3 wa karibu sana, ambao wametumia dawa hiyo na hawana nafuu ya aina yoyote.

  Lawama sasa zinaelekezwa kwa viongozi wetu ambao walijifanya mbao za matangazo kuitangaza dawa ya Babu kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kana kwamba ilikuwa ni mwarobaini wa matatizo yetu ya afya na akili. Babu mwenyewe tayari keshawakana walioshindwa kupona kwa kueleza kuwa ni kutokana na imani yao ndogo.

  Suala la Babu na tiba yake ni zito sana na viongozi wetu wanayo maswali mengi ya kujibu ingawa na sisi pia tuna mzigo mkubwa wa lawama ambao tunastahili kuubeba katika ujumla wetu. Hili ni anguko kubwa la Watanzania kama taifa na linaonesha kuwa hatuko tayari kukabiliana na mambo magumu!
   
 2. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umenikumbusha mbali mkuu, kuna mtu nilimueleza kuusu hili swala kabla, akaniambia bwana usilete usomi wako kwenye mambo ya imani.
  Akaniambia "Kuna mambo mengi ambayo mwanadamu hayajui, kwa hiyo usinishawishi kabisa kutokuamini dawa ya babu".
  Baada ya mwezi, nilumuuliza vipi tiba, jamaa alibaki kulalamika tu kama kawaida ya watz.
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hii tabia tunayozidi kuhalalisha ya kutoa majibu mepesi mepezi kwa maswali mazito ndiyo inayotugharimu sana. Nafurahi sana kwamba pamoja na kunyamazishwa kwa nguvu, ukweli sasa uko hadharani. Ngoja tuwasubiri wadau watupe ushahidi wa imani kama wamepona au la!
   
 4. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tiba ya Loliondo ilishikiwa bango na baadhi ya Maaskofu kisha likabebwa na baadhi ya viongozi wa nchi kisha "vyombo vyetu vya habari" vikapata pa kuuzia magazeti.
  Kazi ndio hiyo. Wewe umia na ulie, mwenzako manufaa na kicheko eeenhhhh??????
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu? Unaongea katika nafsi ya mtu mmoja mmoja au katika mtazamo wa nchi isiyojua lipi la kufanya na lipi la kuacha??
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Polea yako....

  kwa taarifa nilizopata mimi
  watu wa kisukari pamoja na pumu
  wana afadhali sana baada ya kuchukua kikombe
  cha babu ..
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi mwanzoni nilisikia hivyo. Ila kadri ziku zinavyoenda naona kama hiyo tiba ina-expire na exp dates inaonekana tayari zimepita!

  Ngoja tusubiri wenye ma-ushuhuda.

  Mzima lakini wewe?
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmmmhhh
  haya tuzidi kusubiri ..

  Nway mi mzima kabisa Mzee DC
  umeukataa ubabu jumla naona.....

  Vipi we mzima kabisa dear ??
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Safi sana Mjukuu..

  Babu ni mzima na alisharudia jina lake tamu baada ya huyo mtu aliyemkera kuonekana tapeli....

  Kila kitu shwari kabisa...Karibu supu ya pweza pale Chuda!
   
 10. KATIZAJI

  KATIZAJI Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ilikuwa ni kipindi cha sakata la dowans kulipwa bilioni 94! Babu wa loliondo akashika kasi!
  Huku na huku mara tunasikia dowans imekuwa symbion!
  Napenda sana huu muziki wa habari (single ya babu iliuza sana!)
  sasa turudi kwa dowans, hivi iliishia wapi vile?! Wadau tukumbushane!

   
 11. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama hukuwa na iman au imani yako ilikuwa haba huezi pona,ingawa kuna habari kuwa 78% ya walokunywa dawa walipona!
   
 12. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  AD,
  Nina binamu yangu alienda kupata kikombe cha babu kwa ajili ya kisukari, lakini tumemzika kama wiki 3 zilizopita! Binafsi sijapata nafasi ya kumwona aliyepona aliyepata kikombe.............mhhhh!!!!
   
 13. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280

  asante sana Babu
  ilikuwa rahisi sana kukuita
  Babu kuliko Mzee..

  na kuja kuinywa hiyo supu ili unipe
  story za "hapo zamani za kale"
  sante babu...
   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Duhhhh
  Pole sana mami..

  Wachache nilio bahatika kuongea nao
  wanamatumani na wanajisikia vema tu...
   
 15. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Na Babu bado hajaweka wazi hesabu za mshiko mpaka sasa. Jiandaeni kumpokea Texas, Florida au Nevada maana watu wakishatupiga changa la macho na kuzoa mabilioni wanakimbilia U. S. of A. kivulini. Na hilo ni swali zuri Katikazi, hivi Dowans tuliishalipa deni au litaingizwa kwenye gharama za umeme wa Symbion? Tutakoma. Wapiga vita ufisadi Bungeni wako wapi mbona hili limepotea kinyemera?
   
 16. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Tuna-compile ushahidi. Tupatie contacts za hao waliopona ilil tuweze kuwajumuisha katika ushuhuda. So far hatujampata anayesema bila "lakini" kuwa amepona kabisa. Wengine hata kwa macho wanaonekana afya zao bado ni mgogoro.
   
Loading...