Tumeshindwa Kupambana na UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI, na sasa wameongezeka Maadui watatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeshindwa Kupambana na UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI, na sasa wameongezeka Maadui watatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Sep 3, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huku vita ikiwa mbichi ya Kupambana na maadui watatu, ambayo tunazidi kushindwa kadiri ziku zinavyosonga, sasa wameongezeka maadui wengine wabaya watatu. Maadui hao ni CCM, UFISADI na POLISI.

  CCM wanajua siku zao zimekaribia ukingoni, kwa maovu waliowafanyia watanzania, na wanayoendelea kuwafanyia watanzani, wanaamini kuwa siku wakitoka madarakani hawatakuwa na kwa kukimbilia. Kutokana na hili sasa wameamua kuonyesha sura yao kamili. Wamegeuka sasa kutoka kutangaza sera na kuwahudumia wananchi na kuanza kupambana na wananchi na kuhakikisha kwamba wananchi hawana nchi tena, hawana pa kukimbilia. Wananchi hawana haki ya kuandamana, hawana haki ya kuonyesha hisia zao, hawana haki ya kukutana kuzungumza matatizo yao. Kama CCM wanafikiri wataweza kuzuia hili vugu vugu la mabadiliko wajue wamechelewa mno.

  Huu woga wa CCM umewafanya kuzalisha maadui wengine wawili wakubwa wa wananchi. Kwanza wamezalisha ufisadi, kila aliyeko kwenye serikali hii dhalimu ya CCM anahakikisha kwamba anajilimbikizia mali za kutosha ili mambo yakiharibika aweze kukimbilia popote duniani anapotaka. Wakumbuke dunia hii ni ndogo sana, hizo pesa wanazoficha huko uswisi na kwingineko zitajulikana tu na hivyo wasijidanganye kwamba zitawasaidia chochote.

  Pili wamezalisha adui Polisi. Hii ni mbinu ambayo wameamua kuitumia ili kutisha wananchi wasishiriki vugu vugu la mabadiliko. Polisi badala ya kuamriwa kulinda raia na mali zao, sasa wameamriwa kuua raia na kuharibu mali zao. Hawana hata chemba ya huruma, wameua watu wasio na hatia, wameharibu na kupora mali za raia, wamejivika ujambazi huku wakilindwa na wakubwa zao, na ole wake atakaesema askari fulani ni jambazi, asubuhi atajikuta kajinyonga - ukistaajabu ya Musa utakutana na ya Firauni. Polisi wamekuwa walinzi wa mafisadi na wezi wa mali za nchi hii. Wameua watu migoni kulinda maslahi ya watu wanaotuibia rasilimali zetu. Sasa wamegeuka kuua raia wanaotaka kuonyesha hisia zao kwa jamii. Nchi yangu Tanzania unakwenda wapi.

  Tutakimbilia wapi sisi. Bahati mbaya sana Dunia yote sasa imetugeuka. Mafuta yetu na gas yetu imewafanya Jumuiya ya Ulaya na hata Marekani kuvaa miwani myeusi na kuweka pamba masikioni wasisikie kilio cha watanzania, wasione mateso wanayoyapata watanzania kutokana na utawala huu dhalimu wa CCM. Serikali ya CCM inaingia mikataba ya kitapeli na hawa watu ili waendelee kuchukua rasilimali zetu zinazozidi kuongeza siku hadi siku, wasingependa nchi hii ichukuliwe na watu wenye uchungu na rasilimali zao. Nchi hizi zinajua mikataba hii ya kilaghai ikiisha hawatakuwa na sehemu ya kukimbilia kupata rasilimali hizi bure, kwani ni Tanzania tu ndio inazigawa kwa ujira wa 10% zinazofichwa Uswisi. Kwa hiyo wanajifanya hawaoni, hawasikii na wala hawaguswi na mauaji haya ya raia wasio na hatia. Nchi hizi za Ulaya hutasikia zikikemea hii dhuluma na ubakaji wa demokrasia, badala yake wataendelea kusifu viongozi hawa walevi wa madaraka na kutupa misaada feki inayozidi kutuangamiza kila siku. Misaada wanayolipa Jeshi la Polisi ni ya kuhakikisha hakuna mabadiliko nchi hii ili waendelee kuiba. Tutakimbilia wapi sisi. Nadhani Mungu yupo nae atatupigania, Ni yeye tu amebaki kimbilio letu. Bado sijaacha kuamini kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

  Mimi naamini damu za wote waliokufa kutetea rasilimali za nchi hii, zitaibadilisha nchi hii na kurudisha rasilimali za nchi hii mikononi mwa wengi, zitarudisha haki na kuondoa udhalimu, zitafanya tupambane vilivyo na wale maadui watatu wa mwanzo. AMEN.
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakuunga mkono asilimia zote. Polisi wameanza kutembea na mabomu mpaka yanawaumiza na wao wakati wakina Mwema wamekaa ofisini wanazunguka na viti Kama santuri
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Well articulated. Tukiamua tunawaangamiza hawa maadui wapya kwa kuwachoma moto.
   
 4. N

  Ndogue Ndogue Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli maadui hawa watatu wameongezeka,ila watajimaliza wenyewe.USHAHIDI:
  1.ADUI CCM ANAJIMALIZA MWENYEWE-Angalia kisa cha bashe na kigwangala na minyukano mingine ndani yao.
  2.POLISI WANAJIMALIZA-Angalia silaha ilivyowageuka walipokuwa wakimuua DAUD MWANGOSI
  3.MAFISADI WANAJIMALIZA.Angalia kesi ya mramba anavyomshukia mkapa,au rostam anapokimbia 'siasa uchwara za ccm ili atengeneze mtandao wa kuwashughulikia mafisadi wenzie waliomshughulikia'
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Policcm are above the law.
  Mtasikia wakisema "taarifa za KIITELIJENSIA zilizotufikia zinaonyesha marehemu hajapigwa risasi, ila CHADEMA wamemtumia radi ya kichawi kutoka Sumbawanga."
  Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu.
   
 6. data

  data JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,787
  Likes Received: 6,559
  Trophy Points: 280
  Tuongeze maombi na sala
   
 7. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakati UVCCM Kinondoni wamefanya mkutano uliozua vurugu Essacs Sec, na huku Makamu wa Rais kuzindua kampeni za uwakilishi BUBUBU, Chadema wameambiwa wasubiri sensa iishe ndipo waendelee na M4C......! This is not fair
   
 8. t

  tenende JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Lini mkuu?
   
 9. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  jana.......
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  CHANZO
  kitendo cha polisi kurusha risasi katika kundi kubwa la raia wasiokuwa na hatia wakiwemo wakina mama na watoto ni tendo la kigaidi na limepitiliza criminal act. in my opinion what police did yesterday is not a criminal act bali ni terrorism au war act nia ikiwa ni kutisha wananchi kuhudhuria mikutano ya chadema. Kitendo cha polisi kutungua watu wanaokwenda kwenye mikutano ya chadema maana yake wameshatangaza hilo eneo kuwa ni eneo la hatari.

  SABABU ZA KUBEBA SILAHA.
  jawabu letu linatakiwa kuwa wazungu wanasema never bring knife in gunfight. nasi sasa tuna kila sababu za kubeba silaha for selfdefense tu tunapokwenda kwenye mikutano kwa ajili ya usalama wetu au wa mtu binafsi kwani hatuwezi kuendelea ku dis armed/ kutokubeba silaha za kujitetea kwani wenzetu wanazo na wanazitumia kwahiyo kutokubeba silaha ni kuweka maisha yako hatarini. polisi yeyote atakayenyanyua silaha yake kukulenga basi akikisha unammaliza yeye kwanza kabla ya yeye kukumaliza wewe. utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kuendelea kwenda kwenye gunfight ya polisi waliyoitangaza Ukiwa mikono mitupu. amini msiamini polisi wakishajua kuwa wananchi wako na silaha za kujikinga dhidi ya uhuni wao hakuna polisi atakayethubutu kurusha risasi kwenye kundi la raia kwani hana uhakika risasi itakayoingia kichwani kwake itatokea angle gani kwani polisi atakayethubutu kufanya hivyo atakuwa ametangaza vita na umati uliyombele vita ambayo hawezi kushinda.
   
 11. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unyama huu unaofanywa na kuratibiwa na viongozi na wafuasi wa Cdm mpaka lini? Angalia walivyomfanya mwandishi wa Channel ten Iringa. Nimeona walivyomwaga utumbo wake sijaamini nikionacho"..........
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Mwema must go!
   
 13. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Nasikiliza Wapo radio..aisee ni hatari
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mi nasubiri radio iman,
  msemaj wa polisi ameshakanusha,kasema ni kitu kilichorushwa na watu,,,,,sosi magazeti ya leo
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inabidi tuamue kweli Father of All
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  unadhan nani akija atafaa,,,,UMEMSAHAU MAHITA WEWEE???AU ULIKUA HUJAZALIWA???ALIKUJA NA MAJAMBIA AKASEMA YA CUF,,,,,,,MAUAJI YA MWEMBE CHAI?????MAUAJI YA ZANZIBA?????,HATA AJE NANI POLIS WATAENDELEA KUUA TU
   
 17. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni jambo la kusikitisha kuwa raia wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha yao.Hii ni kutokana na kiburi cha CHADEMA kutotaka kutii amri halali za dola.
  Hivi,CHADEMA mtaanza lini kuona uchungu kwa raia hawa kupoteza maisha yao bila sababu?
  Mliambiwa sensa inaendelea,msimamishe M4C yenu hamkusikia.
  Angalieni msije geuka chama cha mauaji.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ar u msemaj wa polis nini,,,maana magazet ya leo yamemnukuu msemaj wa polis kwa maneno hayahaya uloyaandika
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Join Date : 1st September 2012, Nape kwanini usitumie ID yako ya siku zoote unatuchanganya sasa.
   
 20. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  zanzibar sensa inaendelea au wamemaliza maana jana kule kulikuwa na mkutano pale bububu
   
Loading...