Tumeshinda kwenye Operation “Vaa Barakoa” sasa tuhamie kwenye Chanjo

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,858
2,000
Wakati waliozitengeneza chanjo wananchi wao wanazikimbia, Waafrika wanalilia. Huku mnachomwa na jua mwaka mzima na kupata vitamin D ya kutosha, mnakula vyakula vulivojaa vitamin C, bado mnalilia chanjo.

 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,012
2,000
Mfano babako anatoka asubuhi kwenda ktk mihangaiko,,unampa condition aje na nyama akitoka job,ataleta?..
Mfano wa ajabu sana huo.., (Baba yake anatoka kazini kutafuta) Wakati viongozi wanakusanya kodi ambayo huyu unayemdharau ndiyo anayetafuta hio pesa na kuwalipa hao ambao kazi yao ni kuhakikisha anapata value for money....
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,012
2,000
Wakati waliozitengeneza chanjo wananchi wao wanazikimbia, Waafrika wanalilia chanjo. Huku mna chomwa na jua mwaka mzima na kupata vitamin D ya kutosha, mnakula vyakula vulivojaa vitamin C, bado wanalilia chanjo.

Unajua maana ya chanjo ?
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
12,341
2,000
Mjifunze basi kuomba kistaarabu,,kwani mkiomba kwa unyenyekevu kitaharibika kitu?,,sio lazima kutunishiana msuli,,nna hakika mkiomba kwa staha,hizo chanjo zitakuja tu...
Hakuna anayeweza kutamba kama hana afya, hatuwezi kumchekea mtu anayefurahi sisi tukiugua huku yeye akiendelea kufanya majaribio ya kichawi. Yeye kama kazuiwa kuvaa Barakoa na Waganga wake asitushirikishe sisi hadi kutamba kwamba walio karibu naye hawatakiwi kuvaa.
 

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
584
1,000
Ushawahi tongoza demu halafu anapigabkelele na vijembe kuwa hakutaki halafu kadiri muda unavyokwenda analainika kama ute
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,422
2,000
Wakati waliozitengeneza chanjo wananchi wao wanazikimbia, Waafrika wanalilia chanjo. Huku mna chomwa na jua mwaka mzima na kupata vitamin D ya kutosha, mnakula vyakula vulivojaa vitamin C, bado wanalilia chanjo.

Wewe na Dorothy endeleeni kupiga nyungu na kubugia maji ya tangawizi sisi wengine tunataka chanjo.

852EB373-233D-445E-BB1F-215800267A43.jpeg
 

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
2,839
2,000
Hapo Mwanzo msimamo wa Rais na serikali nzima ulikuwa Tanzania HAKUNA KORONA kwa hiyo hakuna haja ya kuvaa barakoa. Baada ya wananchi, wanaharakati na baadhi ya viongozi wa dini kuonyesha msimamo wao wa kuvaa barakoa, serikali ikaanza kubadilika, tukaanza kusikia Tanzania ina korona chache sana mara hakuna aliyezuia kuvaa barakoa, mwisho wakakubali eti ukitaka kuvaa vaa za Tanzania, kwa wananchi huo ni ushindi.

Hatua inayofuata ni kuishinikiza serikali ikubali kuleta chanjo ya virusi vya korona.

Dalili ni nzuri, kwanza wameanza kusema chanjo ni ghari kitu ambacho hakina msingi wowote kwenye afya ya mtu, halafu wanasema eti hazijajaribiwa kwenye nchi za joto kama yetu sijui hizo taarifa wamezitoa wapi.

Najua mwanzo wataona aibu kukiri kama ilivyokuwa vigumu kukiri uwepo wa Covid 19, watakuja na maneno mengi wakijidai kuchagua aina ya chanjo inayofaa lkn mwisho watakuja kukubali kuileta kwa aibu kubwa.

Aluta continua.
1. mlikuwa mnashindana na nani?
2. Chanjo ziko nyingi zingine zimekataliwa Afrika Kusini nayo imizikabidhi CDC ya Afrika zigawiwe
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,422
2,000
1. mlikuwa mnashindana na nani?
2. Chanjo ziko nyingi zingine zimekataliwa Afrika Kusini nayo imizikabidhi CDC ya Afrika zigawiwe
Mabeberu, kwani hujui tuna vita ya kiuchumi, ila sisi tumezikataa chanjo zote tunazo zetu zilizoidhinishwa na wizara ya afya.
 

Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,351
2,000
Upo sahihi. Tuzidi kuwasihi viongozi wa dini, wazidi kuihimiza Serikali kuutimiza wajibu wake.

Kwa kuwa hoja ya msingi ya Serikali ni ughali wa chanjo (ule utopolo wa Mwigulu kuwa eti Dar kuna joto Ni upuuzi), tupiganie hospitali binafsi na taasisi binafsi zinazojihusisha na masuala ya afya kupewa uhuru wa kuagiza na kutoa chanjo.

Kauli ya viongozi wa dini imeonekana kuwa na nguvu kwa serikali kuweza kubaeili fikra zile zisizo sahihi dhidi ya corona, basi hawa hawa watuongoze katika kulipigania hili la chanjo. Lakini chanjo iambatane na upimaji.
Duh wewe ni mwoga hakuna mfano. Unaonekana kuwa na nakisi kubwa ya elimu ya uraia. Hao viongozi wa dini hawadai haki kwa niaba ya waumini bali wanadai haki wakiwa sehemu ya raia; wakiwakilisha kundi kubwa la wananchi.

Ujitokeze kuungana na wenzako kudai haki ya kupata chanjo bila kusubiri maaskofu. Aidha, chanjo haipaswi kutolewa kwa kila mtu kujigharimia mwenyewe.

Serikali inawajibika kutumia rasilimali za wananchi kugharimia chanjo ya Covid 19 na kisha kuisambaza na kuhakikisha wananchi wanapata chanjo hiyo kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa wananchi wote wa taifa hili. Jiongoze ndugu.
 

IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
2,971
2,000
Mlishindwa kumpigania Lisu apate japo 20% sembuse huu ujinga wenu?

Corona itapita huku mkiendelea kuwa wajinga hivi hivi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom