Hapo Mwanzo msimamo wa Rais na serikali nzima ulikuwa Tanzania HAKUNA KORONA kwa hiyo hakuna haja ya kuvaa barakoa. Baada ya wananchi, wanaharakati na baadhi ya viongozi wa dini kuonyesha msimamo wao wa kuvaa barakoa, serikali ikaanza kubadilika, tukaanza kusikia Tanzania ina korona chache sana mara hakuna aliyezuia kuvaa barakoa, mwisho wakakubali eti ukitaka kuvaa vaa za Tanzania, kwa wananchi huo ni ushindi.
Hatua inayofuata ni kuishinikiza serikali ikubali kuleta chanjo ya virusi vya korona.
Dalili ni nzuri, kwanza wameanza kusema chanjo ni ghari kitu ambacho hakina msingi wowote kwenye afya ya mtu, halafu wanasema eti hazijajaribiwa kwenye nchi za joto kama yetu sijui hizo taarifa wamezitoa wapi.
Najua mwanzo wataona aibu kukiri kama ilivyokuwa vigumu kukiri uwepo wa Covid 19, watakuja na maneno mengi wakijidai kuchagua aina ya chanjo inayofaa lkn mwisho watakuja kukubali kuileta kwa aibu kubwa.
Aluta continua.