Tumeshateka mamilioni ya kura, sasa ni wakati wa kuteka mioyo ya wapiga kura

Allan Clement

Verified Member
Aug 14, 2013
1,906
2,000
Nawasalimu ndugu zangu, huku kipekee kabisa nikipongeza ushindi wa JF kwenye baadhi ya kesi zinazoendelea huko! naamini tutashinda zote,

Ni wazi kuwa JamiiForums ni mahali salama kabisa kwasasa, na tuendelee kuomba Mungu sehemu hii iendelee kuwa salama tena! Nikirudi kwenye uzi wangu, mtu mmoja alisema mahali fulani kuwa " kwenye maisha kuna malengo mawili tu! 1. Kupata unachohitaji 2. Kufurahia unachokipata'

Uchaguzi umeisha "salama kabisa" salimini, na chama tawala kimezoa kura nyingi pengine kuliko chaguzi zote za vyama vingi zilizotangulia, sitaki kusema chochote kuhusu uchaguzi ulikuwaje, ninachosema mamilioni ya kura yamepatikana

Kazi kubwa ilioko mbele sasa ni kuvuna MIOYO ya watu ikubali kwa furaha kuwa kura zao hazijaenda bure! Ndio "winning souls" hili ndio jambo la pili la msingi sana, unaonaje unampa mtu mahitaji yote ya msingi lakini hana furaha na wewe? (winning souls) hakuna kitu kikubwa kama kuhakikisha mioyo hii ya wapiga inakuwa pale pale kwenye kura zao!

Hivyo ushindi huu badala ya kuutumika kuwakejeli wengine, utumike kuthibitisha na kuwaonyesha watu wote duniani kuwa "tulistahili kushinda kwa namna hii" (winning souls)

Kupeleka mahitaji pekee hakutoshi, tupeleke upendo na maneno mazuri yasiyo na ubaguzi hata chembe! nilishaona sehemu fulani wananchi walikataa ng'ombe aliyetolewa msibani kwakuwa tu mtoaji wa ile ng'ombe hakuwa na kauli nzuri kwa wafiwa, wafiwa waliamua kuchuma mboga za majani na kuendelea na msiba wao huku dume la ng'ombe likiwa limebaki pale pale kwenye mti.

Winning souls!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom