Tumeshatafakari kabla ya kuwahukumu ya Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA?

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
5,211
4,170
Asalaam ndugu WanaJF wenzangu. Katika tafakari zangu na kujiuliza mambo kadha wa kadha nimeona niwaze kwa sauti na kuishirikisha sauti ya mawazo yangu kwa wanachadema na wali wasio wa CHADEMA.

Mimi sio mtu wa kukurupuka kabla ya kuandika au kuzungumza. Ni MTU wa kutafakari kwanza ndio naweze kuzungumza.

Katika chama cha CHADEMA hakuna Mtu asiyejua Mchango wa bi Mdee katika kukijenga chama hiki ndani ya bunge na nje ya Bunge.

Hatuwezi kudharau Mchango wake hata kidogo. Ni mwenda wazimu tu Atakaye udharau Mchango wa bi Mdee.

Tuje kwenye hoja ya kuapishwa kwao. Kwamba wamekisaliti chama chao kwa kukubali Akubariki uo unaoitwa uharamia wa CCM kwenye Uchaguzi wa October 28

Mimi nilipowaona mabinti hawa wakiapishwa nilifarijika sana na kikawapongeza CHADEMA kwa uamuzi huo wa kutimiza matakwa ya katiba ya kupeleka wabunge wao bungeni.

Ila nilishangaa sana taharifa kutoka kwa katibu wa chadema Bw John John Mnyika ikisema wao hawahusiki na kilichofanyika na wakina bi Mdee.

Sasa nikajiuliza hivi chadema imemwacha mbunge 1 wa nkasi na kuwahukumu wakina Ni Mdee? Mbona haikumkataza yule mbunge wa nkasi na kumtolea vitisho kama hawa wakina Bi Mdee kuna nini nyuma ya pazia?

Hivi Bi halima anaweza kwenda na wenzake tena hawa ni watu wenye wadhifa mkubwa sana ndani ya chama bila kupata BARAKA za Mwenyekiti wao?

Hapa nikagundua kuna kitu kinaendelea ndani ya chadema ila hawataki kutamka hadarani na hawa wakina mama wamekataa kufanywa Rube stamp ya wenye maslai ndani ya chadema.

Mtakumbuka kuna uvumi ulitoka kwamba baadhi ya wakubwa walitaka kupelekea tume majina ya wake zao ili waende bungeni. Nadhani hili linaweza likawa sababu ya wamama haya kukataa kupelekea pelekwa na wa kubwa hawa.

Pili hivi wakina mnyika wange shida nafasi hata 10 za ubunge wange susia kwenda Mjengoni? Au nongwa ni kwa sababu hakuna nafasi za wanaume kwenye horodha ya viti maalum?

Hapa nilazima wafuasi wa chadema wagundue umagumashi uliopo ndani ya chadema. Kwamba kuna baadhi ya Viongozi ndani ya chama ndio wakisema neno lao lifuatwe hata kama halina maslai kwa taifa.

Nilazima vyama hivi vikajitathimini ni wapi vulianguka vikajirekebisha. Lakini vikingangania kujiona kwamba wao ni wenye haki na kudharau yanayofanywa na Serikali katika kuleta Maendeleo basi vitambue mwisho wao kisiasa ndio umewadia.

Wakati chama cha Democratic Kyle marekani kilipo anguka na kushindwa Uchaguzi miaka 4 na Bw Trump kilijipanga na kujisahihisha wapi kilipikosea na Leo wameungwa mkono na wamarekani hapa chadema hawana lakujifunza?

Nimalizie kwa kusema Asiye kubaki kujisahihisha siku zote uangukia kushindwa kazi kwenu chadema.
 
kama kweli hizi sarakasi ni kwa ajili ya pesa za EU za kuendesha bunge ina maana hawaoni kinachoendelea kweli?huu upendo umetoka wapi wa ghafla hivi?
 
Hahaha huyu huyu Halima Mdee aliyekuwa anafukuzwa bungeni kila siku na ndugai tena kwa kashfa leo mnasema alikuwa na mchango mkubwa bungeni?!

Chama cha Chadema akiwemo huyo huyo Halima Mdee waliongoza kuuonyesha umma kwa kuonyesha kura feki za ccm zilizokuwa zimeshajazwa kuingia vituoni, hilo lilituonyesha uchaguzi haukuwa huru na haki, leo huyo huyo anapokubali haram anaonekana shujaa?!

Chadema haitambui uchaguzi uliopita kwanini ikubali viti maalum?!

ACT wakiwa CUF hawakukubali kushiriki serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwanini leo?!

Usaliti ni dhambi kama kuua, na nidhambi kama kuiba, hakuna dhambi kubwa kushinda nyingine, kwa walilolifanya ni usaliti wa wananchi kwa maslahi binafsi siyo ya taifa wala wananchi.

Wako 19 hawana tofauti na COVID-19, wame saliti umma wameamua kujinufaisha ni nje na malengo ya chama.

Hivyo COVID-19 hawatufai wacha waende, tuta recruit wengine wanawake hawajaisha.
 
Back
Top Bottom