TUMESAHAU VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.

Free ideas

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
3,490
2,017
Natumaini mko salama kabisa,

Miaka kama mitatu sasa imepita binafsi naona ile kasi ya vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI imekua ikipooza siku hadi siki.Nakumbuka miaka ya 2010 kurudi nyuma TVs, RADIO na hata mabango ya njiani yalisisitiza sana na kuonya kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Kulikua na kampeni nyingi na mashirika mengi yalipiha kelele na kutoa elimu kuhusu maambukizi na pia njia za kuepuka uhonjwa huu mbaya.Wakagi uli ilikua Radio na Tv nyingi zina matangazo haya katika vipindi vyao.Lakini miaka ya hivi karibuni naona kama mwamko wa vita dhidi ya Ukimwi unaanza kufifia tena kwa kasi kubwa sana.

Sitaki kuamini kwamba inatokana na kuwepo kwa dawa za ARV zinazopunguza makali mwilini.Najaribu kuwaza labda vifo pia vimepungu lakini pia inawezekana watu wameuzoea ugonjwa wenyewe na kuona ni ugonjwa wa kawaida kabisa kama vile malaria.Lakini kwa tathimini yangu mdogo naona kama hili janga bado ni kubwa sana na linamaliza nguvu kazi ya taifa kwa kiwango kikubwa.

Nafikiri ni wakati sasa jamii ikumbuke kutoa elimu kuhusu jinsi ya kujiepusha na janga hili ambalo ni kubwa lakini limefumbiwa macho na kuonekana kama vile ni kitu cha kawaida.Tunatakiwa hatu ili kulinda vizazi vyetu na taifa la kesho kwa ujumla.

Ukimwi na maambukizi yake pamoja na athali zake ni zaidi kabisa ya madawa ya kulevya, ni zaidi ya watumishi hewa, ni zaidi ya vyeti feki, ni zaidi ya rushwa, ni zaidi wapiga dili.Nadhani tunatakiwa kurudisha nguvu ile ile ya miaka ile kupambana na maambukizi ya ugonjwa huu.So pamoja na mambo mengine, mapambano haya ni muhimu pi.Nashauri elimu itolewe mashuleni na iweke hata kweny mitaala ili kuvinusuru vizazi vijavyo.

Itakua ajabu sana kua na nchi nzuri isiyo na rushwa, isiyo na watumishi hewa, isiyo na vyeti feki, lakini ikawa na wagonjwa wengi wa HIV.Nadhani kama taifa tutakua hatujafanya kitu.

Nawasilisha..

...........Free ideas........
 
Back
Top Bottom