Tumepita zama nyingi

Japhet zani

Member
May 9, 2011
83
76
Habari za leo ndugu zangu humu ndani. Mimi nisingependa kuwachosha sana na mastori marefu sana kwani najua Watu wengi humu ni watafutaji.

Jamani nadhani hatuna ubishi kuwa dhama tulizofikia hivi sasa ni za science na Technologia ambazo zinaitaji ,Elimu ,Maarifa vipaji na ujuzi. Ila kuna watu bado wanataka mpaka zama hizi wanataka waishi kama zama za kale za mawe.

Tunajua wote kwa sasa maisha ya kijanja janja hayana nafasi kabisa hata huko kwenye shule za msingi sikuhizi Watu wa mazingaombwe hawaji tena hii inamaanisha mambo ya kuzugana na viini macho havina nafasi tena ktk karne hizi.

Je, nini ambacho nataka kusema kwenu. Nikwamba Elimu ni kitu cha kwanza ambacho kinaweza kukukomboa ktk karne hizi usiwaone Watu kama wakina Dimond au Harmonize ukadhani ni Watu wa mchezo mchezo. Pamoja na kuwa na Talent ya muziki ila wamejibidisha sana ktk kuongeza maarifa na ujuzi ,hivi sasa Dimond au Harmonize anaweza kuwasiliana na mtu yoyote ktk Lugha ya Kiingereza kwa ufasaha na wakaingia mikataba bila utata wowote. Hivyo basi tayari wana Elimu ya kiwango kikubwa sana hata maprofesa na madaktari wanaenda kwao kupata Elimu.

Ushauri wangu kwa watu wote.

Hakuna kazi ya kukuingizia kipato kwa sasa ambayo ni lelemama. Ili ufanikiwe unapaswa ujizatiti kilivyo pamoja na kuwa na misingi mizuri ya hicho unachotaka kukifanya. Usidanganywe na mtu kwamba utafanikiwa kwa kuroga ,never ever ,utaangaika kwa waganga wote hamna utakacho pata zaidi ya kuzidi kuingia kwenye Laana tu.

Mimi kwa leo nikomee hapa ,ukitaka mafanikio jibidiishe ktk kazi na Elimu hata kama unataka kuwa Jangili usiende kizembe zembe tu mwituni magemu watakuchapa shaba siku hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom