Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,302
- 24,142
Public health
From Wikipedia, the free encyclopediaPublic health has been defined as "the science and art of preventing disease”, prolonging life and improving quality of life through organized efforts and informed choices of society, organizations (public and private), communities and individuals.[1] Analyzing the determinants of health of a population and the threats it faces is the basis for public health.
=======
Afya ina misingi yake, Public Health(Afya ya Jamii) ndio mlinzi wa kwanza wa afya ya binadamu.
Tukizembea misingi ya Afya ya Jamii, kinachofuata ni kutafuta tiba baada ya maambukizi.
Tukianzan kutafuta tiba, ugonjwa ukishampata mtu, basi ujue elimu na mazingira ya kinga yameshindikana.
Sasa hivi suala la Covid-19 linachukuliwa kimzaha mzaha, na ni katika ngazi zote.
Watu na viongozi wanakanzania na masuala ya dawa za kienyeji badala ya kuweka misingi imara ya Public Health.
Tunashangazwa Waziri wa Afya ambaye ni Daktari badala ya kukazania namna bora ya kinga, anaishia kujionyesha namna ya kujifukiza, step ambayo ni ya pili katika kupambanaa gonjwa hili.
Namna Covid inavyo enea tunajua sana kwa sasa hivi lakini kuna hatua kwa kweli zinakera, maana ndugu zetu wengi tumewapoteza hasa hizi wiki nane zilizopita.
Kiongozi anadiriki kuema HAKUNA KUVAA BARAKOA
Sijui tumweleweje?
Kuna kiongozi nafikiri huko Moshi, aliamuru waliokuwa kikao wavue barakoa.
Sijui kama ana akili timamu!
Lakini hatuwezi kumlaumu sana, ni kwa sababau wanasiasa wameamua kuliingilia hili suala la public Health bila hata wao kujua misingi yake.
Wizara ya Afya ianze kampeni mahsusi ya kuendelea kufundisha jamii jinsi ya kujikinga na gonjwa hili.