Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,761
- 40,974
Licha ya kashfa nyingi ambazo zimeiandama serikali ya CCM inaonekana kana kwamba Watanzania siyo tu tumekuwa wavumilivu bali pia tumekuwa hatusikii tena maumivu kwani tumekuwa kama tuliopigwa ganzi ya ufisadi. Kiwango cha hasira bado hakijafikia mahali ambapo wananchi wanaweza kusema "imetosha" na badala yake tumekuwa kama tuliokubali kushindwa na tunainamisha vichwa vyetu kwa aibu.
Je, tukate tamaa na kusalimu amri na kukubali hali halisi kuwa "mambo ndivyo yalivyo?" Je tukubali kuwa utawala wa CCM ndivyo ulivyo na hivyo jitihada zetu za kuamsha fikra za watu wetu ni za bure? Kuna faida gani ya kupigia kelele ufisadi na uhalifu wa kila aina hasa kama wananchi bado wako pale pale na wanakubali yale yale?
Ni jinsi gani tunaweza kuizibua na kuizimua hii ganzi ya ufisadi ili watu waelewe kuwa mambo mengi mabovu yanayoendelea nchini yanatokana na utawala mbovu wa CCM? Ni jinsi gani tunaweza kushiriki katika ujenzi wa mawazo ya mapya ya kifikra na kuweza kuliamsha Taifa katika ujenzi mpya wa Taifa.
Sikiliza matangazo yangu ya leo nikijaribu kutafuta majibu ya maswali haya.