Tumepata pancha mikumi na nje kuna wazee wa nyika, konda na dereva wamegoma kushuka kubadili tairi

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu natoka Iringa narudi Dar ila kwa sasa nipo hapa Mikumi mbugani tumepata pancha na basi la upendo lakini nje kuna simba wa 3 wamelala kwenye nyasi, cha ajabu konda na dereva wamegoma kushuka kwenda kubadili tairi wanaogopa wazee wa nyika simba.

Sasa abiria wote tumebaki tumejikunyata ndani ya basi tunasubiria labda tutapata msaada wa kuwatimua simba halafu wanaonekana wana njaa sana maana wanavyotuangalia.

Hawa wadudu wanatisha sana
 
Sio kweli aisee, K 4 LIFE ww ni.muongo...mm nipo hapa Mikumi mbugani nambie ni sehemu gani nije kuwaona na wazungu wangu, tuna siku ya3 mbugani tunatafuta simba hatuoni then nyie bus lije liharibikie miguuni mwa simba???

sasa mkuu kweli nyie muna gundu na hao wazungu wako yaani siku 3 hamjaona simba? sasa mnafanya nini hapo mikumi na hao wazungu? ona sisi simba wamejileta wenyewe hapa tunawafaidi bila ya kulipia, njooni hapa darajani tujumuike
 
Ulivosema 'mna siku 3 hapo' imenifanya nielewe kuwa haupo Mikumi, ungesema hapa Mikumi sawa ningeweza kujishughulisha na ww
 
Ulivosema 'mna siku 3 hapo' imenifanya nielewe kuwa haupo Mikumi, ungesema hapa Mikumi sawa ningeweza kujishughulisha na ww

mkuu mikumi kubwa sana nimeandika hivyo kwa maana sijui mpo angle gani
 
mkuu mikumi kubwa sana nimeandika hivyo kwa maana sijui mpo angle gani

Mikumi sio kubwa aisee, naifahamu vizuri sana maana nimefanya kazi ndanj ya hifadhi kwa miaka mitano....ukiniambia alama ya mahali mlipo najua haraka sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom