Tumepata funzo gani kutokana na uchaguzi wa Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumepata funzo gani kutokana na uchaguzi wa Ghana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhache, Jan 7, 2009.

 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Uchaguzi wa Ghana umemalizika kwa wapinzani kuchukua madaraka ya kuiongoza dola ya Ghana. Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki kutokana na maelezo ya wanasiasa na vyombo vingi vya habari.

  Je wanaona umekuwa huru na wa haki kwa wapinzani kushinda au kuna mambo mengine. Wengi walitegemea pawepo na vurugu kama uchaguzi wa Kenya na Zambia. Au ina maana Ghana wameiva kisiasa zaidi ya Kenya na Zambia. Kihistoria Ghana ni moja ya nchi za kwanza kupata uhuru barani Afrika.

  Ninachoweza kusema ni kwamba tuna kitu tumejifunza. Tusitegemee chama kimoja kiwepo madarakani maisha. Chama kitakachoshinda tukubali matokeo. Wachaguaji ni wapiga kura. Tutoe matokea ya haki na kwa wakati.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Funzo ni kuwa na katiba nzuri inayoipa Tume ya Uchaguzi uhuru wa kutokuingiliwa na viongozi waliopo madarakani. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi TZ anateuliwa na Rais, wajumbe nao. Sasa kweli kesi ya Nyani ukawape Tumbili, kushinda labda kama itatokea Tumbili wamezidiwa na Nyani kuvuna mahindi...
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Tujifunze kuaminiana. Viongozi wengi wa Africa wanaamini ni wao tu ndio wanaweza kuongoza na si mtu mwengine. Hawatizami maslahi ya kitaifa kwanza bali yao na vyama vyao. Kama viongozi wengi wangeacha ubinafsi, naamini matatizo mengi yanalolikabili bara la Africa yangepungua san au yasingekuwapo kabisa.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Hii hoja sijui ni mwanzishaji wake kaiweka huku au ni modereta kaihamisha. Hii ni hoja ya kisiasa. Ilibidi ikae kule kwenye moto. Haitendewi haki hapa madongokuinama.

  Kama ilivyosemwa, Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya Black Africa kupata Uhuru (Ethopia haikuwahi kuwa koloni). Sisi tulikuwa wa pili. Unlike Ghana, sisi hatujapata misukosuko ya utawala wa kimabavu wa kijeshi. Ilibidi tuwe tumewatangulia kidemokrasia na hata kimaendeleo.

  Tatizo la katiba lililotajwa na mwenzetu hapo juu ni la kweli sana. Katiba ya Tanzania iliundwa na viongozi wa CCM, kwa faida ya CCM. Walihakisha wanaiunda kwa namna itakayowawezesha kuhodhi madaraka.
   
 5. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nawiwa kusema nashukuru kwa wote waliotoa mchango wao kuhusiana na tuliyojifunza kutokana na uchaguzi wa Ghana. Katiba nzuri na tume inayojiamini na kujitegema ni moja ya sababu za kufanya chaguzi zetu ziwe nzuri na bila migongano ya hapa na pale.
   
Loading...