Tumenyanyaswa na tumepuuzwa vya kutosha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumenyanyaswa na tumepuuzwa vya kutosha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Petu Hapa, May 4, 2009.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka nilipokuwa shule ya msingi nilisoma ngojera ya maneno haya! tumenyanyaswa vya kutosha, tumepuuzwa vya kutosha - sehemu ya maandiko ya mwalimu nyerere.

  Mwenye kumbukumbu juu ya maandiko hayo na maudhui yake tafadhali nifungue macho! Najaribu kukumbuka maneno yenye kauli za kuleta hamasa kwa wananchi yalikuwa yapi!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ni maneno yaliyoko kwenye tangazo la Azimio la Arusha..

  Tumeonewa vya kutosha
  Tumenyanyaswa vya kutosha
  Tumepuuzwa vya kutosha
  Ni unyonge wetu umetufanya tuonewe, tunyanyaswe na tupuuzwe
  Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ambayo yatatufanya tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena!
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Haya maneno ni mazito sana!

  BWT.......Hivi nani katika maneno hayo anawakilisha ''tume'' na nani analalamikiwa hapo? Je, ni wahujumu uchumi au wakoloni vs wananchi wapenda ujamaa?

  Je, maneno haya yanalitusadia vipi kipindi kile na msaada huo ulipotelea wapi? kwa maneno mengine, maneno hayo kwanini hayapo mioyoni mwetu hivi leo?
   
 4. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2009
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Natamani mafisadi wangetuhurumia wasome haya maneno ya mwalimu wakati huo jamani.Tafadhali Rais wetu chukua hatua juu ya hawa mafisadi.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hamjui tu ni kwanini waliliua Azimio la Arusha?
   
 6. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hayo maneno bado yapo katika baadhi ya mioyo ya watu, ila si wengi. Sababu kubwa ni Choyo na tamaa zimezidi. Kibaya zaidi ni utamaduni unaoendelea kujengeka wa kuwa na mali nyingi, tena easy money. Uliza graduates wa hapo mlimani wa karibuni opinion yao juu ya hilo utashangaa. Kila mtu anataka kuwa tajiri, tena bila jasho. Mtu akipata ki slot tu anachonga dili lake, basi watu wamekaa kidilidili tu, wanakera sana. Ukiwa selfish haujali Mtanzania mwenzako, unaiba tu.

  As a long tern strategy, fundisha wanao hayo maneno, national anthem, uzalendo nk, kizazi kijacho kiwe tofauti. Mimi baba yangu aliniambia!
   
 7. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndio washika hatamu hao! Wananchi! Lakini kwa wakati ule haikuwa saitu ya mwananchi wa kawaida tu, ilikuwa ni sauti ya wasomi, viongozi wa chama, na wapigania uhuru wa nchii hii. Walipokuwa wanasema tumeonewa vya kutosha, hakuwa kuhusu madaraka, ilikuwa ni kubadilisha mfumo serikali ya kikoloni.

  Leo hii, ni viongozi wangapi watasema tume!, watu "wakati" wangapi watasema tume zaidi ya kukimbilia ukuwadi kama alivyosema chachage amakuwa kikaragosi kwa maneno ya mwanakiji!

  Ni wanakijiji wamebaki wanalalama tu wenyewe, wengine wamejifunza hakuna jema la kuingojea serikali, ni mpini na nguvu zako zitakulisha!

  Mwelekeo mbaya!
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Miujiza ni michache sana hapa ulimwenguni!
   
 9. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Azimio la Arusha vs Ujamaa! Eti tofauti yao hawakuiona! Walidhani ujamaa umepitwa na wakati!Kama kujitegemee kunaitwa ujamaa, basi wacha niitwe mjamaa.
   
Loading...