Tumempeleka Rais Magufuli Mahakamani kwa malengo maalum

Well and fine! You are absolutely right! My worry, Tuna Judges wa ku handle kesi kama hiyo? Kuna Judge kwenye high court wa kuwa na guts za kutoa hukumu ya HAKI dhidi ya Rais? Hawa majaji wa "UPE"?
Ukisoma Judgements za akina Lugakingira, Katiti, Mwalusanya na wengine wachache sana ambao sijawataja, these had guts to dispense justice, hawa wa leo hakuna anayeweza kusoma, kwenda library, personal intuition (judicial intuition) akatoa maamuzi yenye high power mental faculty reasoning within the confines of law! Akina Wilbard Mashauri?? Mashauri, yuko High Court??? Shame! Shame on Judiciary, Aibu Ibrahim Juma, CJ!

Nisamee kwa comment yangu inaweza isipendeze, lakini ngoja niiseme!
Judge Mashauri mwenyewe kapewa ujaji kwa hisani ya kuwaweka ndani Mbowe na Esther wakati anatakiwa kustaafu. Kwa hiyo kateuriwa ili astaafu akiwa juji na kula pensheni ya ujaji
 
Tunamshtaki Rais Magufuli Mahakamani kwa Malengo Maalum.

Tangu mwaka jana nilipokata shauri kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia kwa Mwanasheria wangu Wakili Fatma Karume kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Kilangi, kumekuwepo na mjadala kuhusu maeneo kadha wa kadha ya shauri hilo.

Sehemu yenye mjadala zaidi ni uamuzi wetu wa kumjumuisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kama sehemu ya Wajibu Maombi (Respondents). Imezoeleka, kiutamaduni kuwa "Rais hashtakiwi". Tumeaminishwa na tukaamini hivyo. Ndio maana hakuna mtu, kwa kumbukumbu zangu, tangu uhuru aliyemshtaki Rais Mahakamani hapa nchini.

Mjadala wenyewe umeongezwa na kitendo cha Rais Mwenyewe, siku ya sheria nchini kugusia suala la yeye kustakiwa. Rais aliweka bayana mshangao wake kwa watu tunaomshataki wakati ipo ibara ya 46 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayompa kinga.

Ni muhimu kufahamu kwa nini tunamshtaki Rais? Tunajifurahisha tuu ama tunayo malengo?
Mbali na sababu mbalimbali, tumelazimika kumfanya Rais kuwa Respondent kwa sababu yeye ndiye aliyemteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali asiyekidhi sifa za kikatiba za kuwa na sifa za kuwa wakili na mtumishi wa umma kwa miaka 15. Kwa kumbukumbu zilizopo Dk. Kilangi amepata uwakili mwaka 2011 hivyo hakidhi sifa hizo zilizowekwa na Katiba.

Swali linakuja kwa nini tuendelee kumshtaki Rais wakati anayo kinga? Sisi tumesoma ibara ya 46 ya Katiba (nimeiambatanisha). Hatujaona popote kwenye ibara hiyo kuwa Rais ana kinga ya kutoguswa moja kwa moja. Tulichoona;

1. Kwenye masuala ya jinai kinga ya Rais ni absolute. Hagusiki kabisa Mahakamani

2. Kwenye masuala ya madai anayoyafanya kama Raia, kinga yake ina mipaka. Anaweza kushtakiwa lakini sharti apewe notisi kwanza.

3. Kwa makosa anayoyafanya kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama hili la kumteua Mwanasheria Mkuu asiye na sifa, hatujaona kikwazo cha kikatiba.

Hivyo basi, suala hili kuletwa mbele ya Mahakama, linaipa Mahakama nafasi ya kutoa tafsiri juu ya kinga ya Rais. Mahakama itatueleza kama kinga ya Rais ni ya kutoguswa moja kwa moja ama ina mipaka. Hii ni fursa kwa Mahakama kuimarisha jurisprudence ya eneo la kinga ya Rais specifically na uwajibishwaji wa Rais kwa ujumla.
Mahakama isingeweza kutoa ufafanuzi wake yenyewe bila kupelekewa suala hilo.

Sisi tumejitolea kulipeleka jambo hilo ili Mahakama itekeleze wajibu wake wa kutafsiri sheria.

Tunaliachia jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Kiongozi Feleshi, Masoud na Luvanda linaloendesha kesi hii lifanye kazi yake.

Ado Shaibu, Katibu Mwenezi, ACT Wazalendo.View attachment 1019393

Sent using Jamii Forums mobile app
Shauri liko mahakamani. Hivyo halistahili kuzungumziwa nje ya mahakama. Kama unaona una ushahidi wa kutosha kushinda kesi, bana hoja zako usiziweke hadharani mpaka utakapoziwasilisha mahakamani. Ama sivyo itachukuliwa unaingilia uhuru wa mahakama. Hufaidiki cho chote kwa kueleza mitandaoni hoja zako kuhusu shitaka lako.
 
Judge Mashauri mwenyewe kapewa ujaji kwa hisani ya kuwaweka ndani Mbowe na Esther wakati anatakiwa kustaafu. Kwa hiyo kateuriwa ili astaafu akiwa juji na kula pensheni ya ujaji
Hivi how old is he? Nilidhani labda ni kijana hivi middle aged
 
Shitaka Lako Ni Kupinga Uteuzi Wa Dr. D. Kilangi Kuwa AG au Shitaka Lako Ni Kinga Ya Rais Kutoshitakiwa Mahakamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Napinga uteuzi wa AG. Lakini kwa kumjumisha Rais, inalileta suala la immunity ya Rais kwenye mjadala. Bila shaka upande wa Serikali utaleta pingamizi ya kwamba Rais hashtakiwi. Hapo, Mahakama itailazimu Mahakama kwanza kushughulikia suala hilo kabla ya kushughulikia kesi ya msingi.
 
Hahaha kila siku nasema humu wenzenu wanafuata ILANI ya chama chao nyie mnafuata katiba na hapo ndio mnapishana nao.

Kila siku mnasema kavunja katiba kwa hili au lile na sijawahi kusikia mmeshinda kesi, au na huko mahakamani hawafuati sheria na katiba?!
 
Well and fine! You are absolutely right! My worry, Tuna Judges wa ku handle kesi kama hiyo? Kuna Judge kwenye high court wa kuwa na guts za kutoa hukumu ya HAKI dhidi ya Rais? Hawa majaji wa "UPE"?
Ukisoma Judgements za akina Lugakingira, Katiti, Mwalusanya na wengine wachache sana ambao sijawataja, these had guts to dispense justice, hawa wa leo hakuna anayeweza kusoma, kwenda library, personal intuition (judicial intuition) akatoa maamuzi yenye high power mental faculty reasoning within the confines of law! Akina Wilbard Mashauri?? Mashauri, yuko High Court??? Shame! Shame on Judiciary, Aibu Ibrahim Juma, CJ!

Nisamee kwa comment yangu inaweza isipendeze, lakini ngoja niiseme!

acha matusi
 
Una kifua kijana mwenzangu? Usije ukataitiwa kidogo ukapotea maboya. Mambo mazito hayo kumshtaki Mkuu
 
Back
Top Bottom