Tumeliwa Sisi

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Namkumbuka sana mzee Maganya, mkazi wa Mara wilaya ya Mugumu, mnamo miaka ya 1980 baada ya vita ya Uganda yule Mzee alikuja na wazo la ajabu sana, mzee Maganya aliamua kujitangazia Uhuru wake toka ndani ya Tanzania hii, ila hakuwa na elimu, alipandisha bendera yake ya ngozi ya chui na kujitangazia uhuru wake,akiwa na kikosi chake cha ulinzi kamili. Mwalimu nyerere wakati huo akiwa rais aliamuru akamatwe haraka sana, lakini ilikuwa ni vigumu sana kumpata, hata hivyo vyombo vya dola vilifanya kila njia na kufanikiwa kumtia mbaloni na kisha kumuua kwa lisasi mwaka 1983.

Hadithi hizi zilipowafikia watanzania wengine,watu toka Mara tulionekana kama matahira na wakorofi katika jamii hii ya kitanzania, tulidharaulika na hata kusontwa vidole, ilikiwa vigumu sana hata ndugu zangu wa Mara kwenda kuoa katika makabila mengine katika Tanzania hii.

Mimi nilijiuliza ni kwanini mzee(Maganya) huyu aliamua kufanya hivyo siku zile kweli sikupa jibu kwa kipindi kile, ila sasa ndipo naanza kujua Mzee Maganya alikuwa na Mtizamo mzuri kama msimamo huo angeuanzisha kama leo angeungwa mkono na sisi sote,ila kilichomuhukumu ni wakati na elimu pia.

Kwa kuwa ndugu zangu elimu ilichelewa katika mkoa wetu, kwani katika mkoa mzima shule za sekondari zilikuwa tatu(Tarime sec, Musoma sec na Mara sec) hizo ndizo shule katika miaka hiyo ya 70 – 80 zilizokuwepo, hivyo jamii yangu ikajikuta ikiishia katika majeshi ya Polisi na JWTZ katika taifa hili la Tanzania.

Katika mikoa mengine mambo hayakuwa hivyo, matharani kilimanjaro, Kagera , Arusha na kwingineko mambo yalikuwa shwari, watu walipata elimu ya kutosha na hata leo haushangai kuona mkoa mmoja waweza kuwa wasomi ya kiwango cha uprofessor zaidi ya 100, lakini huko nitokako wakizidi ni kati ya 3 – 6.

Hoja yangu iko hivi, hebu sisi ambao hatukupata elimu ya kutosha kwa maana ya kwamba jamii zetu hazikujitoshereza katika elimu tutaupataje usawa katika gawio la Taifa hili? Wale wasomi wa wakati ule kwa sasa ndiyo wenye nacho, sasa sisi twende wapi? Mnatusukumia ukutani eti? Umoja wetu uko wapi sasa? Hebu kumbe Mzee Maganya alikuwa na mtizamo halisi! Ndugu zangu ninyi ni mashaidi kuwa kile kilichoachwa na Mwalimu Nyerere wameshagawana, wamerasimishana na hata kuingia ubia na Wageni, sisi twende wapi jamani wanyonge wa taifa hili?

Najua wanaforum mwaweza kusema nina jaziba ila siyo hivyo bali huu ndiyo mtizamo wangu, naomba mnisaidie kimawazo sisi tusiyokuwa na fedha za kuwapata elimu bora watoto wetu wana nini siku za usoni? Ama uwiano huu wa tusiokuwanacho utaendelea hivi mpaka lini. Taifa linawajibu wa kusawazisha uwiano huu mapema. AMA NDIYO TUMELIWA SISI TULIYOCHELEWA KUPATA ELIMU

Mwana wa Mwita nimesema.
 
Kuna mwingine pia kule Tarime sikumbuki ni kijiji gani alipandisha pia Bendera ya chui kujitangazia uhuru, tuhabarishe na hiyo.
 
Back
Top Bottom