Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 159
Heshima Mbele,
Mchana huu nimetafakari sana maneno ambayo nimeulizwa na Ndugu Msimbe.Sanctus kaniuliza mpaka sasa nimelifanyia nini Taifa,Inawezekana likawa swali langu ila ni swali ambalo tunapaswa kujiuliza kila mmoja wetu(hata yeye kama yeye amelifanyia nini taifa?).
Ili swali si geni sababu hta wapinzani wamekuwa wakiulizwa wamelifanyia nini taifa na viongozi wa CCM na imekuwa ni swali la kawaida kuulizwa kwa mtu yeyote ambaye anaonekana ni mpinzani au anshabikia jambo flani lenye maslahi.
Ila hii si hoja ya leo ili ki-ukweli kila mtu amelisaidia taifa kwa njia moja ama nyingine na kwa wapinzania wanatakiwa wapewe nafasi(pindi wakiwa tayari )ili waoneshe wanweza kufanya nini
Wana Jamii wenzangu,
Tumekuwa wachangiaji wakubwa sana hapa, tumekuwa waandishi mahiri hapa, tumeweza kujenga hoja nzuri,nyingine zenye mbembwe na kejeli,zingine zenye mistari ilipangwa kwa sanaa ambayo inavutia ila sasa kila mmoja ajiulize amelifayia nini taifa,na tutanatikiwa tufanye nini kwa taifa hivi sasa.
Mie binafsi michango yangu humu imeweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika taifa hili,na hii ni mifano michache tu
1.Nilikuwa mtu na kama risasi kali ambayo ilieleza umma kuhusu mikataba ya Buzwagi iliyosainiwa visivyo huko UK.
2.Nilisababisha Bunge likamng'oa Mamvi na kashfa yake ya RDC
3.Nilimwambia Mkulu kuhusu kuchukizwa kwangu na Masuala ya EPA,na nikamweleza atenganishe siasa na sheria.
MY TAKE
Mambo ambayo tuanatakiwa kujiuliza kwa sasa ni nini tufanye ili kulisadia taifa
1.Tufute yote na tuanze upya kabisa,tuwasamehe wale wote waliotufikisha hapa,ndiyo kesi za IPTL,RDC na za EPA na za kina Mramba zifutwe kuanzia mwaka huu
ili mwaka 2010 tuanze upya kabisa kujenga taifa jipya lenye misingi ya utu,lenye kujali wananchi wake,lenye viongozi wanaojua wananchi wanahitaji nini kwanza,lenye wansiasa wanaojali maendeleo ya majimbo yao.
2.Tufute ile kadhia kwamba mtu anaweza kutupa maisha Bora,hivyo tuangalie ni nani anaweza akatuongoza na siyo kutawala
Mie uwezo wangu ni kuandika,na michango yangu hapa JF imeweza kulisaidia Taifa kuondokana na wizi,ufisadi na utawala mbovu,nimeweza pia kujenga ujasiri kwa watu wengi hivyo taifa limefadika na mawazo yangu.
Last edited: