Tumelamba Garasha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumelamba Garasha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanilo, Feb 1, 2011.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa wale wacheza karata wanajua maana ya kulamba dume kunavyoweza kuathiri mchezo mzima na kupelekea ushindi. Ila Ukilamba magarasha lazima upate maumivu ya kupoteza mchezo mzima wa karata hata kama utakuwa na jockeri moja na magarasha matupu. Nimeanzia mbali nikijaribu kuangalia ahadi na utekelezaji wa kile alichokuwa akikisimamamia Mh Mwenyekiti wa CCM wakati wa uchaguzi uliopita. Ninapata wasi wasi na IQ yake kwa kile alichokuwa akikisema, Nimeongezea ahadi ya 70 ambayo iko wazi lazima ataitekeleza tena kwa mbwe mbwe.

  1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum
  20.chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  21.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  22.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  23.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  24.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  25.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  26.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  27.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  28.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  29.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  30.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na
  31.kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  32.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  33.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  34.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  35.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  36.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  37.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa -Musoma
  38.Kulinda haki za walemavu - Makete
  39.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  40.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  41.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  42.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  43.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  44.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  45.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  46.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  47.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  48.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  49.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  50.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  51.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  52.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  53.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  54.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  55.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  56.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  57.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi - Ifunda
  58.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  59.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  60.Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii – Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  61.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa – Kibandamaiti mjini Zanzibar
  62.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  63.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  64.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  65.Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  66.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  67.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  68.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  69.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  70. Kufuata utawala wa kisheria wa kutii mamlaka za kimataifa hata kama mchakato wa DOWANS umejaa utapeli, lazima tuwalipe ili Rostam asifanye nchi isitawalike.


  Sisiti kukuona wewe Mkwere ni kama garasha kwa hizi ahadi zako.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Karibu Mchungaji, na pole na matatizo, naona umeingia kivingine kabisa

  Mkuu hivi unapoteza muda kuangalia hizo ahadi za huyo jamaa, mbona kuna mambo mengi ya kuyazungumza na kupanga mikakati ya kuchukua nji hii, nadhani ukimdiscus huyo jamaa na wewe utakuwa ni level moja na yeye, mijadala hiyo hiyo ina wenyewe (MS nk)
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  LAZIMA ALIPE HANA UJANJA AKIKATAA MAMBO YATAKUWA MABAYA ZAIDI CCM WANA TELELEZA ILANI YAO KWA ASILIMIA MIA PALE WANAPOWAKUMBATIA MAFISADI NA WEZI ILA KWA ASILIMIA SIFURI KWA WATANZANIA HASA WA MONDULI NA IGUNGa
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Reverend Masanilo welcome home mkuu!

  Kaka hiyo ahadi namba moja inanihusu sana kifamilia na kibiashara/uchumi tatizo langu ni kwamba nilishaondoa matumaini kwa Mkuu wa nchi labda kama unatokea muujiza sawa tutaipokea hiyo reli kwa furaha.

  Mkubwa mwenzio akiamua kukudanganya ujue amekudharau, nami nahesabu alitudharau na anaendelea kufanya hivyo!
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hii nchi haina wenyewe....
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hi dharau kubwa sana! Tunajua cha kufanya Ben Ali nguvu ya Umma ilimwangukia na sasa upepo unaelekea kwa Hussein Mubarak! Natamani na sisi tumtoe mkwere na dharau zake hizi. Sidhani akama anajua kuwa tunajua anatudharau
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  karibu mkuu!
  karibu sana
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kule kwenye messenger umepigwa ban?
   
 9. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ah, Mchungaji umerudi, karrriiiiibbbb sana yhakhe!
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Kiongozi nilikuwa napita tu ndo ghafla nakutana na huu ukumbusho wa mashairi ya Daktari mkuu JK.

  Ntarudi baadae.
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,948
  Likes Received: 23,830
  Trophy Points: 280
  Mchungaji umerudi na hasira mbaya!

  karibu tena.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa anapenda sana kuimba bongo flava hata kwenye mambo yanayohitaji umakini! Umeme ni shida baada ya miaka 50.....hawa jamaa ni yak yak!
   
 13. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mchungaji karibu sana. Tulikumiss sana Mkuu
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tawile baba tumechoka tunasubiria kipenga tu tujae mitaani:clap2:
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nilikuwepo kwa ID mingine mazee! Teh teh teh teh teh
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Karibu Rev..
  akitimiza ahadi hizo zote ruksa kuilipa Dowans na hata kurudi madarakani
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  NGOJA NIRUD MKUU....!
  hahahaha
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ni ahadi pekee iliyomsaidia Daktari mkuu JK kujipatia "kula" kutoka kwa ndugu zangu wa mkoa wa Mara.
  Sasa hizi kelele za wanaharakati wa mazingira zimewapandisha pressure jamaa zangu, nadhani JK atakuwa anatabasamu kwakuwa amepata excuse ya kutotekeleza ahadi yake. Ila asisahau kwamba asipojenga hiyo barabara hasira za raia zitahamia kwenye faru!!
   
 19. Taluma

  Taluma Senior Member

  #19
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ....ama kweli this is H.E.DR......!
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tuna matatizo yanayofanana kama watanzania. Ugumu wa maisha ni kwa kila mtu regardless ya itikadi zake kichama hata kidini. Ni miaka 50 hadi leo tunakosa maji safi ya kunywa wakati fisadis wanakunywa maji sipesheli na matibabu majuu. Misri huyu Husni Mubarak alishinda kwa 95% leo watu wako mtaani hawataki ujinga. Zaidi ya watu Mil 1 wameandamana polisi wameungana nao maana huwezi uwa watu wote hao

  [​IMG]
   
Loading...