Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,382
- 38,653
Kutokana na Historia yao Wamarekani hupima marais wao angalau kwa siku 100 tangu kuingia kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani ni zaid ya mwaka sasa umepita. Kuna watu wanaona kama taifa tumekwama na nchi yetu haipati yale maendeleo yaliyokusudiwa kiuchumi wala kijamii.
Lakini kuna kundi jingine ambalo wao husema kwa kila hali mambo yapo shwari na tunasonga mbele na tupo kwenye njia sahihi. Lakini hatupewi uchambuzi wa kina na vigezo vilivyo wazi kuonesha kama tumekwama tumekwamaje na kama tunasonga mbele tunasongaje. Hivi tangu uchaguzi wa Mwaka 2015 nchi yetu ya Tanzania inasonga mbele ama imekwama pale alipotuacha Jakaya Mrisho Kikwete, au tumerudi nyuma mpaka enzi za Mwalimu Nyerere ama ndiyo tumeselelea kabisa hadi enzi za Ukoloni?