Tumekusikia Steve Mkapa!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
Tumekusikia Steve Mkapa!

Mpayukaji wa Msemahovyo
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KATIKA jitihada zake mfu za kuwasafisha na kuwatetea wazazi wake, kijana Steven Merinyo Mkapa alijikuta akiuwasha moto asioweza kuuzima.

Wapo wanaoshangaa busara ya Benjamin Mkapa na mkewe Anna, kushindwa kujitetea hadi wakamruhusu mtoto wao awajibie kihuni na kwa lugha za mitaani! Hebu soma nukuu ya kijana huyu tuliyetegemea awe msomi na mwelewa wa mambo. "Najua na wewe ni miongoni mwao kati ya wale wanaotumiwa kumchafua baba, lakini hamtaweza kitu, hizi ni namba zingine," alisema Steve .

Kuchora na hizi ni namba zingine, maana yake nini zaidi ya kuwa lugha ya mitaani? Au ni yale yale ya mtoto wa nyoka ni nyoka? Maana baba yake alisifika kwa kutumia salamu ya kihuni ya ‘Mambo'? .

Maskini kama ni kuchorwa, basi Steve ndiye alimchora baba yake huku naye akijichoresha. Unafikiri unafanya kazi Kiwira si kujichoresha kweli?

Mkapa mdogo alikuja na hadithi za jogoo na dume asijue watu wanajua kuliko anavyodhani. Angekuwa amewahi kuonja adha za Watanzania wanayoipata kutokana na madudu yaliyofanywa na baba na mama yake, hakika asingeropoka na kutisha kama alivyofanya

Kwanza inapaswa bwana mdogo huyu aambiwe kuwa wakati wa watoto wa wakubwa nao kuwa watawala wadogo kiasi cha kutisha umekwisha. Aigize watoto wa marehemu Mwalimu Julius Nyerere, ambao walijitenga na jina la baba yao na kujitafutia maisha.

Kinachozidi kumuonyesha mtoto huyu kama mwenye ufisadi wa kimawazo kutokana na kulelewa na fedha za ufisadi, kwanza ni kudhani kila mtu anahongwa na pia kudandia jina la baba yake. Yeye kama Mtanzania, tena aliyelelewa kwa pesa ya bure ameishaifanyia nini Tanzania? Hana anachojua wala alichofanya zaidi ya kuendelea kufugwa na wazazi wake.

Hata alipoulizwa wapi anapata riziki yake ya kila siku, bila aibu alijibu Kiwira, asijue Kiwira ni chumo la wizi wa baba yake! Hebu soma nukuu hii. "Najua unataka niseme nini…nenda kaseme, nafanya kazi Kiwira…kwa sababu nadhani nyie bila Kiwira na Mkapa hamna cha kuandika," alisema Merinyo huku akinyanyua glasi yake tayari kwa kunywa.

Haya si majibu ya msomi na mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa nchi. Maneno ya kijana huyu anayeonyesha kutokuwa na nidhamu yanamuonyesha kama mbumbumbu asiyeandaliwa kitaaluma.

Juzi tulisikia utetezi wa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete. Alijibu maswali kiutu uzima na kisomi. Alijitetea kuwa analima kijishamba chake licha ya kufanya kazi za kisheria. Lakini angalia huyu wa Mkapa. Yeye anaonea fahari kufanya kazi kwenye mgodi wa baba yake unaosemekana umepatikana kwa wizi na ufisadi.

Watu walitegemea Steve aongelee anachojua kuhusiana na baba yake na mama yake hata kaka yake, kujineemesha kwa mgogoro wa ikulu. Walitarajia angekanusha kuwapo kwa ANBEN, Fosnik, Tanpower na madudu mengine.

Mkapa mdogo alilenga kuwaonyesha waandishi wa habari kama wenye unywanywa na ngoa. Lakini hata hivyo alishindwa.

Anaona wanaoandika mabaya ya wazazi wake wametumwa na wanahongwa. Hivi nani alimhonga Mbunge Aloyce Kimaro? Wanaosema wazazi wake waliibia taifa ni Watanzania, si waandishi wa habari, na isitoshe kwa umri wake hajui kuwa waandishi wa habari ni sauti ya umma! Kama kuna kitu alichothibitisha Steve, si kingine bali kuwa na malezi mabaya. Tunaojua maisha ya familia yake walipokuwa Sea View kabla ya baba yake kuwa rais, hatuyashangai maneno ya Steve. Watoto wa kina Nyang'anyi, marehemu Chiduo na wengine waliokuwa wakiishi karibu na kwa Mkapa miaka ya 80 hadi 90 wanajua tatizo la Steve ni nini .

Inatisha kama hawa ndio watoto wa watawala wetu. Yaani Steve hajui ni kwa nini Watanzania wanamtaka baba na mama yake wajieleze! Anakimbilia vitisho asijue watu hawamuogopi mtu. Hajui kuwa Watanzania wamebadilika na kuanza kuchukua hatua za kujikomboa kifikra! Huyu ni wa kuhurumiwa sana.

Maskini Steve angekuwa anajihangaisha kusoma alama za nyakati na historia ya matukio na tawala za dunia asingesema aliyosema. Asingepayuka wala kuropoka. Angeogopa kile kilichowapata watoto wa majambazi kama Causescu, Surhato, Augusto Pinochet, Sani Abacha na wengine wengi ambao baba zao walikuwa vibaka walioko madarakani.

Wataalamu wa tabia husema kuwa tabia ya mtoto mara nyingine huonyesha aina ya wazazi alio nao. Na hii kwa Steve siyo chuku. Mkapa alisifika kwa ubabe na urushi. Sasa tazama anawarithisha wanawe udhaifu huu. Hivi Steve hajui kuwa watanzania wakiamua wazazi wake wanaweza kusema hata kama hawataki? Asiwachokoze watu waliokwishapigika kutokana na siasa na sera mbovu za baba yake. Hajui Watanzania wanajua kuwa baba yake alipata mali nyingi alipokuwa madarakani. Hata hiyo Kiwira inayompa riziki Steve kuna siku itarejea mikononi mwa umma. Asijidanganye kuwa kinga ya baba yake ni kinga yake, hata kaka yake na mama yake .

Atake asitake kuna siku haki itatendeka na wahusika watalipia. Hili ni suala la wakati. Laiti angesoma ufunuo wangu juu ya maiti inayolindwa huku ikinuka pamoja na ukoo wake! Hakuna kitu kinaweza kuisaidia familia ya Mkapa kama kukubali ukweli kuwa walitenda ndivyo sivyo. Hili halina ubishi. Laiti Mkapa angeeleza alivyopata mali anazomilki kama mgodi wa Kiwira, ANBEN, Tanpower, mahekalu ya Mkuzi Lushoto na lile la Sea View bila kusahau M Bank .

Juzi juzi Mkapa alikaririwa akisema wanaosema aliiba ni waongo. Bahati nzuri Watanzania walishtukia uongo wake wakaja juu na hajajibu zaidi ya kujibaraguza.

Na hii si mara ya kwanza kwa Mkapa kutumia njia mbovu na watu wabovu kujitetea. Walianza wachumia tumbo kina Tambwe Hiza. Tulipowaandama wakaachia ngazi na kujifungia kwenye chama wanakoganga njaa zao.

Sasa anamtuma mwanawe asiye na adabu wala ujuzi. Bado mambo mazito. Mkapa ajitokeze ajibu maswali ya umma juu ya jinsi alivyoongoza nchi na alivyopata ukwasi. Tunamtaka atueleze mafanikio ya uwekezaji aliyotuahidi.

Maskini Steve haoni hatari inayowakabili wazazi wake. Amekuwa kama mke wa mfalme wakati umma ulipokuwa ukiandamana kwa kukosa mkate, akasema kama hawana mikate si wale keki. Maneno haya yalijirudia nchini Romania ambapo imla wa nchi ile Nicolae Causescue alipinduliwa na kuuawa yeye na mkewe.

Maskini Steve angejua Watanzania wanavyohangaishwa na ufisadi uliosimikwa na baba yake asingefunua kinywa chake na kukufuru. Angekuwa amesoma shule za mwembeni akitembea kwa miguu au kuumizwa na wahuni wa daladala, hakika asingetapika aliyotapika.

Maneno ya Steve hata hivyo yana faida moja kwa Watanzania. Nayo ni kuwaonyesha shibe ilivyowalevya watawala wao na watoto wao kiasi cha kukufuru na kuwatishia Watanzania hao hao.

Mbona Mwalimu Nyerere alivyoshutumiwa kuwa alikuwa kajiwekea pesa nyingi nje alijibu tena kwa unyenyekevu. Hatukumsikia Makongoro wala Emily wakimtetea baba yao. Wala hatujawahi kusikia watoto hawa wa Mwalimu wakidaiwa kujihusisha na aina yoyote ya ufisadi. Hata mkewe Mama Maria hajawahi kushutumiwa na kiumbe yeyote kuyatumia madaraka ya mumewe kujitajirisha yeye na ndugu zake.

Kinachokera sana ni ile hali ya kuwa ni mwalimu huyu huyu aliyemlea Mkapa na kumbeba hadi akawa rais aliyeweka historia ya kuporomosha misingi na mema yake.

Hii inanikumbusha kisa cha fisi mmoja aitwaye Blaise Compaore kule Burkina Faso aliyelelewa nyumbani kwa shujaa Thomas Isdore Sankara, akaishia kumpindua na kumuua! Huku ni kukosa utu na shukrani. Ni aina fulani ya uhayawani unaotendwa na binadamu wenye silka za kihayawani.

Mkapa mdogo asitake kututia madole machoni. Tutajitetea. Na aambiwe na aelewe, ikiwezekana akome kudhani tunaoandika tunalipwa. Mbona hawataji wanaotuhonga kumchafulia baba yake jina, utadhani analo jina safi! Hakuna aliyechafua jina la Mkapa kama Mkapa, mkewe, marafiki na washirika wake.

Nyamaza au tafuta chuo ukaondoe huo ujinga. Busara ya leo ni maneno ya Kiingereza yasemayo: ‘Pride goes before fall and fools rush where angels fear to tread'.

nkwazigatsha@yahoo.com
 
Hivi hii serikali ipo kweli?? haya mambo mbona hata haijishughulishi kuyafatilia tujue ukweli kama jamaa anatuhumiwa afanyiwe kazi... Hao watoto nadhani ni kelele za chura hawawezi kuzuia tembo kunywa maji... Wa-tz tutasema tu...

Obasanjo aliwapa somo zuri sana kule Arusha kwenye mkutano wa Sullivan kuwa mambo ya kulea ufisadi ndio yanalostisha nchi za kiafrika na yeye akawapa mfano jinsi alivyomshughlikia IGP wake...

Sasa hapa kubebana kumezidi hata pasipobebeka mtu anabebwa tu mh!....
 
Umetuandikia Kichwa Kikubwa Hoja Chache Na Marudio Ya Wenzako Na Hasira Zako. Hii Ni Tabia Ya Ukanjanja, Kelele Nyingi Huna Data
 

Kuchora na hizi ni namba zingine, maana yake nini zaidi ya kuwa lugha ya mitaani? Au ni yale yale ya mtoto wa nyoka ni nyoka? Maana baba yake alisifika kwa kutumia salamu ya kihuni ya ‘Mambo’? .

Sikujua kama Salaamu ya "Mambo" ni uhuni.
MmmHm...Ama kweli la kuvunda halina ubani
 
Umetuandikia Kichwa Kikubwa Hoja Chache Na Marudio Ya Wenzako Na Hasira Zako. Hii Ni Tabia Ya Ukanjanja, Kelele Nyingi Huna Data

Siamini huo utumbo wa huyo FDR.Jr.!!!!!!!! Anyway, wewe usiye Kanjanja una data gani? The boy is nuts and had no needs to go public while he knows exactly what happened. wengi tuna hasira kwa taarifa yako
 
Umetuandikia Kichwa Kikubwa Hoja Chache Na Marudio Ya Wenzako Na Hasira Zako. Hii Ni Tabia Ya Ukanjanja, Kelele Nyingi Huna Data

Wataalamu wa tabia husema kuwa tabia ya mtoto mara nyingine huonyesha aina ya wazazi alio nao.

Maana yake ni moja tu, kuwa Yesu alikuwa mtoto wa Mungu na huyu mtoto ni wa rais wetu wa zamani! Na hapo juu kuna mpambe aliyekuwa anatupiwa tupiwa angalau mifupa mifupa mpaka hawezi tena ona ukweli, masikini sasa amekuwa kipofu kwa sababu tu ya mifupa ingawa hajui nyama kala nani, sasa angependa wote hapa tuwe kama yeye yaani vipofu, halafu nasikia according to the dataz huyu mpambe ni mmoja wa viongozi wakubwa sana kwenye taifa letu, I Hope hizi dataz sio za kweli!
 
Umetuandikia Kichwa Kikubwa Hoja Chache Na Marudio Ya Wenzako Na Hasira Zako. Hii Ni Tabia Ya Ukanjanja, Kelele Nyingi Huna Data


Nakubaliana na wewe. Tatizo la watu wetu wakipenda chongo. Naheshimu uandishi wa mpayukaji lakini hapa ameandika chini ya kiwango chake. Kulikuwa na hoja nyingi za kumuumbua Steve Mkapa na maswali mengi aliyostahili kujibu. Makala imepwaya. Halafu anasifia majibu ya Ridhwan Kikwete kuwa yalikuwa mazuri. Hebu tuleteeni tena kile alichojibu mtaona tu kwamba kilichomsadia tu ni kuwa Mwandishi Charles Mulinda alilenga kumsafisha hivyo hakumuuliza maswali kwenye weak angles tofauti na Steve Mkapa ambaye mwandishi wa Nipashe alilenga kabisa kumuuliza maswali ya kumchokonoa na kumbomoa! Steve Mkapa na Ridwan Kikwete wote wamesema uwongo sawa, wameulizwa kuhusu ufisadi wote wamesema hakuna ufisadi kabisa. Wakati kila mtanzania anaujua ukweli.

FMES, unaweza kuwa na bifu lako la FDR Jr lakini katika hili, msome vizuri na ufikirie nje ya moyo wako.

Katika maandiko kama haya tunawahitaji watu wanaoweza ku-speak they minds kama mama kilango, bila kujali hoja imetoka kwa nani

PM
 
FMES, unaweza kuwa na bifu lako la FDR Jr lakini katika hili, msome vizuri na ufikirie nje ya moyo wako.

Wataalamu wa tabia husema kuwa tabia ya mtoto mara nyingine huonyesha aina ya wazazi alio nao.

Mkuu PM,

Kwa kawaida huwa ninakuona kwa mbali sana kwa sababu sijawahi kuwa impressed na huwa sikuelewi kabisaa, sasa hapa sielewi unasema nini hasa, mimi hiii quote hapo juu inanitosha sana, sihitaji zaidi na ninajua FDR kuwa ni kiongozi mkubwa wa taifa ambaye nisingetegemea kuwa na huu msimamo wa kumtetea Mkapa, sasa naomba tena nifafanulie exactly unachosema wewe ni nini?

Nimsome vizuri halafu nimfikirie moyo wangu, I hope hicho nacho ni kiswahili makini? au?
 
mathalan ingekuwa nyie msingewatetea wamzee wenu??? ... anyway .. ningekuwa mimi ningeufyata tu .. na jina nabadili kabisa

nasikia huyu kakulia ulaya atajua dagaa wanavunwa kigoma kweli ... ???
 
Mwandishi amechemka na ku-PANIC tuu hapa. Mambo madogo sana haya, hayafai kukuumiza kichwa. Angalia sana anko/anti, utapata presha hivi hivi.

Asante.
 
Sikujua kama Salaamu ya "Mambo" ni uhuni.
MmmHm...Ama kweli la kuvunda halina ubani

Yaaah...hata mimi nmeshangaa sana kusoma hilo la "mambo" kuwa ni salamu ya kihuni. Hii ni sawasawa na ile kasheshe iliyotokea jana usiku ya JMushi1 kumwita Kikwete 'mafia'....kuna watu eti walikasirishwa na Kikwete kuitwa hivyo....ilinishangaza sana kwa sababu Mkapa kaitwa majina mengi sana humu ndani lakini sikuona outrage (although by a few) kama ya jana iliyopelekea mtu kufungiwa temporarily.
 
Yaaah...hata mimi nmeshangaa sana kusoma hilo la "mambo" kuwa ni salamu ya kihuni. Hii ni sawasawa na ile kasheshe iliyotokea jana usiku ya JMushi1 kumwita Kikwete 'mafia'....kuna watu eti walikasirishwa na Kikwete kuitwa hivyo....ilinishangaza sana kwa sababu Mkapa kaitwa majina mengi sana humu ndani lakini sikuona outrage (although by a few) kama ya jana iliyopelekea mtu kufungiwa temporarily.

labda "LAIS" anatakiwa kuwasalimia wale anaowaongoza kwa salaam kama ifuatavyo, "Habari ya asubuhi/mchana NN" na siyo mambo. Wengine wanaweza kuona ni sawa na wengine wakaona kuna kasoro. Sijui huyu wa awamu ya nne anatumia salaam ipi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom