Tumekubali. Tutakukumbuka Rais wetu John P Magufuli

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
628
Toka umetutoka hayati rais wa JMT. JPM mambo yamekuwa siyo mambo. Sijuwi tuanze wapi tumalizie wapi.

Umeme ni kukatika hovyo na kila baada ya masaa fulani. Ila wanakusingizia eti ulikuwa hutaki matengenezo wala maboresho.

Pia wanadai suluhisho siyo kufukuza watu kwa uzembe au kutokuwajibika bali kubembelezana (January Makamba)! Ndio mzee usishangae karudi kwa kishindo tena anapokezana na mama kwa safari

Swala la safari kwa viongozi ni kama wamefungulia bomba la maji. Wanaponda maisha kama wanakufa kesho

Swala la huduma ya maji ndio usiseme mzee. Wanaishi kifalme. Ungekuwepo wangejiongeza kuchimba visima ila haupo wao wamerudia tena kufanya kazi kwa mazoea

Rasimali na maliasili zinavyoibiwa ndio usiseme. Pale Mererani pamoja na ukuta wao wanapitisha Tanzanite getini

Mzee yaani nchi inavyoendeshwa ni kama bora liende. Mama ni trips every other day. Hivi hajawahi panda ndege au kwenda mamtoni nini? Maana kila raia kapigwa na butaa anavyopenda safari aise!

Juzi juzi twiga walionekana wamebebwa kwenye fuso! Wanaenda wapi hatujuwi.

Mzee yale ya kutishiana wanijuwa mie ni nani au nitakupoteza yamerudi mzee.

Yaani tuliowachaguwa na kutumwa watutumikie imekuwa nongwa. Wamekuwa miungu mitu.

Hivi mzee tukimuomba mwenyewe muumba kweli hawezi kukurudisha hata kwa miaka michache urekebishe jahazi?!
 
Kuna watu ni wajinga Sana nchi hii.Nakumbuka hotuba ya mwanzo kabisa ya Samia alihoji Kuhusu kujengwa ukuta na kuweka wanajeshi juu lakini bado tanzanite zinaibwa.😂😂..

Boresha mazingira ya hiyo biashara,wizi haukuwahi kuisha toka Mwendazake zake wenu yupo na unfortunately zama za giza hakuna chombo cha kuthubutu kutoa taarifa zaidi ya pambio za mtukufu.

Kwangu Mwendazake ni moja ya Marais wa hovyo kabisa kuwahi kutokea ndio maana hakuna kitu alikamilisha zaidi kushika huku na kule .

Mgao wa umeme ni mfano wa akili fupi aliyokuwa nayo.How comes uanzishe ujenzi wa Bwawa ambalo hujui litaisha lini na hakuna backup ya umeme kwenye dharura kama ukame? Huoni amelazimisha nchi kurudi kwenye majenereta wakati alikuwa na fursa ya kuondoa hilo?

Wivu na uongo eti gas ni ya mabeberu,stupid .
 
Toka umetutoka hayati rais wa JMT. JPM mambo yamekuwa siyo mambo. Sijuwi tuanze wapi tumalizie wapi.
Umeme ni kukatika hovyo na kila baada ya masaa fulani. Ila wanakusingizia eti ulikuwa hutaki matengenezo wala maboresho! Pia wanadai suluhisho siyo kufukuza watu kwa uzembe au kutokuwajibika bali kubembelezana (January Makamba)! Ndio mzee usishangae karudi kwa kishindo tena anapokezana na mama kwa safari!
Swala la safari kwa viongozi ni kama wamefungulia bomba la maji. Wanaponda maisha kama wanakufa kesho!
Swala la huduma ya maji ndio usiseme mzee. Wanaishi kifalme. Ungekuwepo wangejiongeza kuchimba visima ila haupo wao wamerudia tena kufanya kazi kwa mazoea!
Rasimali na maliasili zinavyoibiwa ndio usiseme. Pale Mererani pamoja na ukuta wao wanapitisha Tanzanite getini!
Mzee yaani nchi inavyoendeshwa ni kama bora liende. Mama ni trips every other day. Hivi hajawahi panda ndege au kwenda mamtoni nini?! Maana kila raia kapigwa na butaa anavyopenda safari aise!
Juzi juzi twiga walionekana wamebebwa kwenye fuso! Wanaenda wapi hatujuwi!
Mzee yale ya kutishiana wanijuwa mie ni nani au nitakupoteza yamerudi mzee!
Yaani tuliowachaguwa na kutumwa watutumikie imekuwa nongwa. Wamekuwa miungu mitu!
Hivi mzee tukimuomba mwenyewe muumba kweli hawezi kukurudisha hata kwa miaka michache urekebishe jahazi?!
Kufa usifiwe ishi uchukiwe
 
Nimepata kumuona Rais mmoja tu tangu nizaliwe

Bila kuingiza ushambenga na mihemko ya kisiasa, aliyofanya Yale ambayo Kila mtanzania alitamani kumuona kiongozi mkuu wa nchi anayafanya,

Alitamka wazi kwamba kwenye Mambo mengi TUNAPIGWA, Jambo ambalo hakuna mtanzania anayebisha

Alienda mbali zaidi na kutuonyesha namna ambavyo wapigaji wanatupiga, Jambo ambalo ukiacha Nyerere hakuna mkuu mwingine aliyetusanua

Haijalishi kafa au yupo hai,

YEYE NDIYE RAIS WANGU WA MAISHA

Rest in piece president, let you go!! NO BODY will remain
 
Toka umetutoka hayati rais wa JMT. JPM mambo yamekuwa siyo mambo. Sijuwi tuanze wapi tumalizie wapi.
Umeme ni kukatika hovyo na kila baada ya masaa fulani. Ila wanakusingizia eti ulikuwa hutaki matengenezo wala maboresho! Pia wanadai suluhisho siyo kufukuza watu kwa uzembe au kutokuwajibika bali kubembelezana (January Makamba)! Ndio mzee usishangae karudi kwa kishindo tena anapokezana na mama kwa safari!
Swala la safari kwa viongozi ni kama wamefungulia bomba la maji. Wanaponda maisha kama wanakufa kesho!
Swala la huduma ya maji ndio usiseme mzee. Wanaishi kifalme. Ungekuwepo wangejiongeza kuchimba visima ila haupo wao wamerudia tena kufanya kazi kwa mazoea!
Rasimali na maliasili zinavyoibiwa ndio usiseme. Pale Mererani pamoja na ukuta wao wanapitisha Tanzanite getini!
Mzee yaani nchi inavyoendeshwa ni kama bora liende. Mama ni trips every other day. Hivi hajawahi panda ndege au kwenda mamtoni nini?! Maana kila raia kapigwa na butaa anavyopenda safari aise!
Juzi juzi twiga walionekana wamebebwa kwenye fuso! Wanaenda wapi hatujuwi!
Mzee yale ya kutishiana wanijuwa mie ni nani au nitakupoteza yamerudi mzee!
Yaani tuliowachaguwa na kutumwa watutumikie imekuwa nongwa. Wamekuwa miungu mitu!
Hivi mzee tukimuomba mwenyewe muumba kweli hawezi kukurudisha hata kwa miaka michache urekebishe jahazi?!
JIWE
 
Kumkumbuka mtu Kuna mazuri na mabaya.
Angeacha chukibl dhidi ya chadema angeacha sifa nzuri sana
 
Sio Magufuli mwendazake Wala Samia,CCM haistahili kuendelea kuongoza nchi.period
 
Kuna watu ni wajinga Sana nchi hii.Nakumbuka hotuba ya mwanzo kabisa ya Samia alihoji Kuhusu kujengwa ukuta na kuweka wanajeshi juu lakini bado tanzanite zinaibwa...

Boresha mazingira ya hiyo biashara,wizi haukuwahi kuisha toka Mwendazake zake wenu yupo na unfortunately zama za giza hakuna chombo cha kuthubutu kutoa taarifa zaidi ya pambio za mtukufu.

Kwangu Mwendazake ni moja ya Marais wa hovyo kabisa kuwahi kutokea ndio maana hakuna kitu alikamilisha zaidi kushika huku na kule .

Mgao wa umeme ni mfano wa akili fupi aliyokuwa nayo.How comes uanzishe ujenzi wa Bwawa ambalo hujui litaisha lini na hakuna backup ya umeme kwenye dharura kama ukame? Huoni amelazimisha nchi kurudi kwenye majenereta wakati alikuwa na fursa ya kuondoa hilo?

Wivu na uongo eti gas ni ya mabeberu,stupid .
Kwani mwendazake alimaliza mda wake hadi aliyoyaanza yakamilike? Hoja hazina mashiko kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom