Tumekazia hukumu ila nataka kujitoa, Nitapata haki?

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
620
1,000
Habari za Siku ndugu,

Mimi ni miongoni mwa tuliofungua kesi ya kudai kampuni,tuko watu 8,kesi imeishahukumiwa tulipwe na zaid ya miez 6 imepita na hatujalipwa,ila mwanasheria wetu kaandaa KUKAZIA HUKUMU, lakin kwa bahati mbaya kukazia hukumu kukatupiliwa mbali kwa makosa madogo ya kisheria, lakini kapewa mwongozo ili aandae KAZIA HUKUMU MPYA,

Lakini kwa upande wangu nimeona nijitoe kwenye hiyo kesi ili niende kwenye meza ya mazungumzo na kampuni yangu kwa kuanza upya kwa kuamini naweza pata haki au madai yangu mapema tofauti na hapa tulipofikia, kwamba hapa tulipofikia naweza tumia muda mrefu bila kupata madai yangu kwa wakati.

1. Naomba msaaada wa kisheria wapi ni bora kwangu kwa haraka na kwa uhakika zaidi kati ya hiyo stage tulipofikia na hayo maamzi nayotaka kuyafanya.

2. Kisheria ikitokea Mkakazia hukumu na mkapewa ushindi wa kumlazimisha mwajiri kulipa kwa lazima Je muda sahihi kisheria anaopewa kutekeleza kabla ya kukamatiwa Mali ni muda gani.

3. Naomba kupata ufafanuzi mzuri wa NGUVU YA MAAMZI YA KUKAZIA HUKUMU kisheria.
 

John Mwalingo

Member
Apr 29, 2020
11
45
Kimsingi Kama kesi iliisha na Mahakama ikaamua mlipwe fidia na Kampuni yenu baada ya siku therasini (30) za kisheria kuona Kama kuna upande haujaridhika na uamuzi huo kukata rufaa juu ya shitaka husika na uamuzi wa hukumu haujatekelezwa baada ya siku hizo kuisha mshindi au walio pewa upendeleo katika kesi hiyo moja ya jambo la msingi watakalo lifanya ili haki ipatikane ni "kukazia hukumu tu"

Note....!!

Meza ya mazungumzo katika jambo lililo amriwa na Mahakama halipo ile ni amri na amri hiyo kutekelezwa kwake ni kukazia hukumu mazungumzo yangekuwa mahala pake Kama jambo hilo lingekuwa halijafikiwa uamuzi "Hukumu"Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom