rmajani
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 530
- 525
Tumekazania mno viwanda bila kujua athari ya kuleta viwanda toka nje ya nchi hasa China itakavyohatarisha ajira na uhuru wetu wa kisiasa ktk nchi yetu. Kwa sababu ya kutilia sana mkazo fedha tumefanya kosa kubwa.
Tumekazania mno viwanda kama vile tulivyosema bila fedha hakuna maendeleo ni kama twasema pia viwanda ndo maendeleo, bila viwanda hakuna maendeleo. Kosa tunalofanya ni kudhani maendeleo yetu yataanza au kukomaa kutokana na viwanda, ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha viwanda vingi vya kisasa ktk nchi yetu.hatuna pesa zinazohitajika na hatuna ufundi unaohitajika.
Haitoshi kusema kuwa tutakopa pesa na kuazima mafundi toka nje kuja kuanzisha viwanda hivyo(viwanda 200 toka China). Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia viwanda hivyo tunavyotaka.
Na pia hata kama tungeweza kupata msaada huo. Kualika msululu wa mabepari kuja nchini kuhodhi viwanda ni hatari kwa mstakabari wa ustawi wa nchi yetu na watu wake. Mfano ni makampuni ya madini wananchi wetu wanavyoangaika na wale wafanyabiashara wa kichina Kariakoo.