‘Tumejivua gamba kujenga imani kwa vijana’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Tumejivua gamba kujenga imani kwa vijana’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, May 2, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIBU wa Mambo ya Nje ya Sekreatarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Januari Makamba amesema chama hicho kimejivua gamba ili kujenga imani kwa umma hasa vijana ambao ni wapiga kura.Kwa mujibu wa Makamba, CCM imefikia mahali ambako ilikuwa haiaminiki kwa umma kutokana na baadhi ya wanachama wake wakiwamo viongozi wa ngazi za juu kuhusishwa na tuhuma za rushwa na ufisadi.


  “Kujenga uaminifu kwa wananchi ni kazi kubwa ambayo tunatakiwa kuifanya, yaani wananchi watuamini kwani kama chama Serikali yetu inafanya kazi kubwa za maendeleo, lakini kama huaminiki hata kazi hizo zinaonekana kuwa ni bure,”alisema.

  Alisema katika mchakato wa kukijenga upya chama hicho, lazima idadi ya wanachama wa CCM waongezeke kutoka milioni tano wa sasa na pamoja na kujenga mfumo utakaokiwezesha chama hicho kuwa na viongozi waadilifu na weledi.

  “Miongoni mwa hatua tunazochukua ni kuhakikisha tunakuwa na viongozi wasio na madoa, pia watuhumiwa wote wa rushwa na ufisadi wajiondoe bila,”alisema Makamba.

  Makamba alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi jijini Dar es Salaam."Chama kina wasemaji wake, Mwenyekiti, Katibu Mkuu na hasa Katibu wa Itikadi na uendezi si mimi, lakini niseme dhana ya kujivua gamba nia yake ni kujenga nchi ikiwa na CCM imara, madhubuti na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania kupitia rasilimali zilizopo nchini," alisema Makamba.

  Alifafanua kuwa msingi wa kuanzishwa CCM ni kuwaletea wananchi maendeleo na kwamba ili kufanikisha hilo chama hicho kinapaswa kujivua gamba kwa lengo la kurejea katika misingi yake.

  "CCM ni 'progressive party', hivyo lazima kirudi katika msingi wake ambao ni kuleta maendeleo ya jamii kutumia rasilimali zilizopo," alisema Makamba.

  Kuhusu nafasi yake ya sasa ndani ya Sekretarieti ya CCM, Makamba alisema kinachofanyika katika idara hiyo ni kujifunza na kwamba watafanya kazi kisayansi kwa kuyachambua mambo ili majibu yawe sahihi na yaliojitosheleza.

  Alisema majukumu ya idara yake yametajwa katika Ibara ya 113 (3) ya Katiba ya CCM ambayo alisema ni mazito likiwemo la kukijenga upya chama hicho ili kipendwe, kipate wanachama wengi zaidi, viongozi weledi na waadilifu ili kishinde uchaguzi kwa urahisi bila kutumia nguvu zaidi.

  Alipotakiwa kueleza chama gani kinaonekana kuwa tishio kwa CCM, Makamba alisema mtazamo wake ni kuwa vyama vyote vya upinzani ni sawa na kwamba katika ushindani wa kisiasa jambo la msingi ni kushindana kuwa na fikra na sera bora zinazovutia wananchi na kuwaletea maendeleo badala ya kupigana vijembe.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  labda vijana wa upanga na kisutu.
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  too little to late...! NINI KUJIVUA GAMBA..? JIKATENI MKIA..!
   
 4. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit. january kapata mtindio wa ubongo. anadhani hilo la kujivua gamba litawasaidia kwa kiasi fulani. hajui kwamba hata wale waliokuwa wkikisupport ccm ndo wa kwanza kukilaumu na kukikimbia baada ya ccm kukiri wana magamba.
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Imani kwa vijana imesharudi na sasa vijana wanajipanga kuwaletea ushindi mwaka 2015 ukizingatia ajira zilizoongezeka baada ya sera za kuvuana magamba kuanza hadi kufikia 2015 hakutakuwa na kijana ambaye atakuwa hana ajira so ushindi huo unakujaaaa!!!!:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
   
 6. d

  daniel.nickson Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm haiwezi kuwa na mvuto tena kwa vijana, lakini ni lazima upinzani hasa chadema kupita kijiji baada ya kijiji na kuhakikisha chadema inatambulika kila kona ya nchi, wasilale kama walivyolala katika jimbo la newala ambapo mpaka siku za mwisho kabisa walikua hawajapata wa kusimama nafasi ya ubunge. hii inamaana kwamba kwenye hiyo wilaya wafuasi wake walikua ni wachache sana au hakuna kabisa.
   
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni wiki kadhaa (chache) zimepita tangu ccm kutoa kauli ya kujivua magamba. Ikumbukwe kuwa hiyo ni kauli tu na sio vitendo. Matokea ya vitendo vya magamba hayo hayawezi kufutwa na kauli za mdomoni. Mimi naona kuwa wapambe wa magamba na ccm hawajajua bado kina cha taabu, vifo na dhiki ambazo wamezipata wananchi, wakiwemo pia vijana. Hivyo ni dharau kubwa, au ujinga kusema kuwa imani ya vijana imesharudi baada ya kusikia hiyo kauli ya kujivua magamba. Inamaanisha kuwa vijana wa Kitanzania wana kumbukumbu fupi sana, na hata hali yao ya kimaisha inawezwa kubadilishwa na maneno ya majukwaani.

  Naamini kuwa vijana wa Kitanzania wana akili nyingi za kujua nani anawahadaa na nani anawapa matumaini. Mpaka hivi leo, 'kujivua magamba' kumebakia kauli tupu pamoja na kusogezwa kwa magamba machache katika nyadhifa zao. Mpaka hivi sasa, Tanzania imeshikiliwa na inaendeshwa na magamba, ambayo kiukweli ni kuwa kujivua kwao kwa magamba hayo ni kifo chao. Umeshawahi kumvua kobe gamba lake? Ukumvua gamba kobe, utamuua, kwa vile hataweza kuishi bila gamba lake.
  Tafakari...!
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Na hayo magamba ni yapi? mbona naona ni yaleyale tu!
   
 9. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nyoka ni nyoka tu siku zote...hawezi kubadilika kua mjusi kisa tu kajivua gamba! CCM ni chama cha waoga! walioiibia nchi hii na wanatumia nguvu nyingi kuficha maovu yao,nadhani hofu ya kuadhirika ii wazi vichwani mwao!...
   
 10. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  CCM watakapojua watanzania wanahitaji nini ndipo watapata suluhisho. Lakini hii misamiati na kufungua matawi mapya sijui Marekani hayana maana kabisa. Mbona matawi yapo kibao tu. Tafuteni watanzania wanahitaji nini kwa sasa na siyo kuongeaongea tu kwenye vyombo vya habari.
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huu wimbo wa kuvua gamba kutoka ccm haona beat na vina
  kila siku ccm wanasema wanavua gamba na kuna watu wanatuhuma za ufisadi
  lakini hakuna siku waliyotutendea haki wananchi kwa kutuambia hizo tuhuma ni zipi?
  kama ni zile za DR SLAA, ina maana wanamfukuza mwenyekiti wa chama chao?
  tunaomba ccm waucheze mziki wa DR SLAA kwa staha na kwa step,
  kama watamwacha mwenyekiti wao kupiga ngoma za huu muziki , sisi wananchi
  hatuta rudisha imani kamwe maana MKUU WA KAYA n miongozi wa wezi wa ngoma,
  naye avuliwe gamba kisha njooni kutuomba imani

   
 12. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nipewe mdahalo na huyu kijana,awaeleze watanzania mambo yafuatayo:-
  1. Akiwa mwanaccm mwaminifu, awaambie watanzania,ii wapi pesa yetu waliyiba hao anaowaita magamba kwa sasa?
  2. Akiwa kiongozi wa ccm sasa, awaambie watanzania, je kama wamevua magamba kwa tuhuma za ufisadi, wamewafikisha mahakamani ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuhujumu uchumi?
  3. Awaambie watanzania, kama ccm imeinua mikono juu kwa cdm, kwa kutekeleza matamko ya cdm ya kuwaadhibu mafisadi?
  4. Nini faida kwa watanzania, kwa kitendo chao cha kujivua hayo magamba hewa?
  5. January sio gamba changa limealo, baada ya baba yake kuitwa gamba zee lililovuliwa?
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mbona kauli ya katibu wake ni tofauti?
   
Loading...