Tumejifunza nini kutoka kwa Mbowe katika mkutano wake?

Nimetoa maoni na tatizo hujaisoma thrrad nzima kama umeisoma hujaielewa. Na tatizo kubwa sana tinalo sijui ni elimu finyu ama la. Ulitakiwa kuujibu hoja na ukaweka muono wako. Ulichokifanya ni kunikosoa bila kuchangis chochote ili uonyeshe msimamo wako. Nimesema ktk thread tukubali kutokukubaliana. Kama hukubaliani na mimi basi ni weka sababu zako ulichokifanya ni kuweka maneno mdomoni mwangu maana sijakulazimisha kukubaliana na mawazo yangu.
Umejikita kwenye"Kutokuamini" so hizi ni feelings zako.
Mbowe ANAAMINI VYOMBO VYA DOLA VINAHUSIKA
 
Mimi siamini kama vyombo vya dola vinahusika lakini ninaelewa kwanini watu wanaamini hivyo sababu ya makandokando. Siyo kila mtuhumiwa anayehukumiwa kifungo katenda kosa lakini pale utetezi wako unapokua unapwaya si vigumu ikaaminika kuwa wewe ndiye mkosefu na hili ndilo linaloiponza serikali yetu. Mbowe kaainisha labda kama hukumsikia kasema Mawazo aliuawa mpaka leo tumeshamsahau. Ben Saanane kapotea hakuna kilichotokea. Lakini vyombo vyetu vipo tayari kutumia pesa zetu kuwanyanyasa raia wema wanaoenda kujitolea damu. Yaani kama wewe unatetea hata huu upuuzi basi sina la kusema. Kuniita mimi nipo upande gani hilo nitakujibu. Mimi nipo upande wowote ule ambao ninaona una haki ama ule ambao nitaona unaonewa kama uwezo wangu ni kutumia vidole vyangu kukemea basi nitakua upande huo wewe baki na mapenzi ya vyama vyenu.

Wanaonifahamu wanajua kabisa hata hapo juu nimesema kuna mambo anayoyaseka Lissu aijubaliani nayo kabisa na nimeshampinga hapa jamvini. Lakini hiyo haimaanishi kuwa hata akionewa nisiwe upande wake hiyo hulka yangu hata kama utanibatiza kuwa mimi ni chadema sijali maana najua kuna siku nikiandika kumsifu rais wako utanipongeza na ndiyo malipo yenu ya unafiki.
 
Hilo ni neno kama hawana wasiwasi basi waache vyombo huru vichunguze. Huko nyuma sikuunga mkono lakini hizi serikali za afrika ni majanga
has a jpm ni zaidi ya janga kwa tz yetu tuzidi kumwomba muumba aingilie kati
 
Kamati za ulinzi na usalama hapa Tanzania hukutana tu kama kuna mtu kamsema 'vibaya' mzee mitandaoni ili akamatwe haraka.Mikoani RC ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na DC kwa wilaya. Kwa ngazi ya nchi hatuelewi hiyo kamati ya ulinzi na usalama kama ipo na viongozi wao ni akina nani? Labda mzee na sirro wake.
 
has a jpm ni zaidi ya janga kwa tz yetu tuzidi kumwomba muumba aingilie kati
Hapo sina la kukomendi. JPM mimi namfanisha na ule msemo mgema akiaifiwa tembo hulitia maji. Kuna mambo mengi sana nayaunga mkono lakini tatizo langu kwa JPM ni pale anapotumia nguvu pasipohitajika nguvu. Lakini hapa leo mada ni kumjadili mhe Mbowe si Magufuli wakati wake ukifika tumjadili na yeye
 
Mbase1970 ,

..unaamini nani amefanya hili jambo?
Kwa bahati mbaya sana simfahamu ila bado nasisitiza serikali inalo swali gumu sana la kulijibu. Ni nani alitaka Lissu afe na kwanini. Lissu alishalalamika huko nyuma kama maisha yake yapo mashakani lakini hakuna aliyejaribu kumsikiliza na kumpatia ulinzi. Na si hivyo tu tangu Lissu apatwe na hili tatizo hatujasikia neno lolote la maana la jinsi gani vyombo husika vinavyolifanyia kazi.

Swali kwanini watu wanaombeza rais mitandaoni inakua rahisi kushikwa lakini wasiojukikana inakua vigumu? Mawazo kaacha watoto wadogo ambao hawatapata bahati ya kuona baba yao akiwasindikiza katika graduation ama katika harusi zao na mpaka leo hawajui nani alimuua baba yao. Haya matukio pekee yananifanya niilaumu serikali sababu ndiyo pekee inaweza kuwashinikiza wapelelezi wafanye kazi zao kwa uhakika. Pia ukiwalaumu mapolisi moja kwa moja na rais anahusika sababu yeye ndiye amiri jeshi wao.

Lakini nani kafanya hiki tukio sina jibu.
 
Nimejifunza kwamba issue nzima umeichukulia kiimani na ndiyo maana umejikita katika neno "Siamini" na unataka na sisi tukuamini na tusiamini wengine.
Kwa bahati nzuri ameweka wazi yale ambayo anayaamini, ambayo yanajulikana na kila mtu. kuamini kitu ni uhuru wa mtu. lakini kuamini kwa hoja fulani, hapo unaweza kukosolewa kwa hoja ulizoweka. hujaweka hoja yoyote, unamtuhumu tu kwa "kuamini". Hii ni GT forum mkuu.
 
Mimi si mfuasi wa chama chochote kile naomba nieleweke hivyo kabla sijaweka hoja fupi leo kufuatana na press conference ya Kaka yangu Mbowe.

Wengi wetu humu ndani tunamuita Mbowe ni Dj ama Mbowe ni Form four failure nk. Lakini kama kuna mtu yeyote aliyeisikikiza press conference yake jana atakubaliana na mimi kuwa ni mmoja wa wanasiasa wenye weledi wa juu katika kupanga nini cha kuongea na wakati gani kiongelewe ndiyo maana mheshimiwa huyu hapati misukusuko yeyote tangu nianze kumfuatilia ktk siasa zake.

Mbowe ni mtu mtulivu sana umpende ama usimpende huu ndio ukweli wenyewe. Hakurupuki hata kama kuna uwezekano wa kujipaisha kisiasa anayeweza kunipinga kwa hili naomba alete hapa jamvini.

Alipohutubia mkutano kule mwanza nilisema pia na nilimsifu japo wengine waliniita nyumbu. Ukifuatilia maneno yake ya jana utaona kuwa kaongea kiukweli aliweka kiki za kisiasa pembeni. Na zaidi ya yote kaiaibisha serikali maana kuna baadhi ya watu serikalini na bungeni wanataka kumchafua mh Mbowe kwasababu zao binafsi ambazo mimi binafsi sielewi zinasaidia nini katika kuuleta umoja wetu wa kitaifa ambao muanzilishi wa Taifa hili aliuhubiri sana. Kwa bahati nzuri muanzilishi huyo ndiye muasisi wa chama kilichopo madarakani.

Nilimsikia Mhe Ndugai spika wetu na pia nilimsikikiza mh Mbowe (KUB) na nikachukua muda kutafakari maelezo ya hawa wawili nimegundua kuwa siyo tu Ndugai ni mzushi bali ni mnafiki. Kwa maana kwamba pamoja na kujifanya alimtakia mema mh Tundu Lissu ambaye mimi si mshabiki wake kabisa lakini alifanya hivyo kuihadaa jamii na kumfanya Mbowe na wenzake ambao ndio waliokua mstari wa mbele kumhuduimia Lissu waonekane ni matapeli. Mimi binafsi sielewi kama huyu Mheshimiwa Ndugai anapata nini ama anajiongezea nini kisiasa zaidi ya kuweka alama ya kuuliza.

Sikukubaliana na mambo mengi ambayo Tundu Lissu aliyokua anayasema lakini hiyo ndiyo demokrasia yenyewe lakini siwezi kusema kama kupingana kwangu na mawazo yake inifanye mimi nimchukie. Lakini inaonekana kuna baadhi ya watu wanamchukia Lissu kwa msimamo wake badala ya tu ya kuelewa kuwa demokrasia ni pamoja na kukubaliana kutokukubaliana. Hii dhana ya kukubaliana kutokukubaliana ikiingia vichwani mwa watanzani hapo tu tutafikia demokrasia ya kweli.

Binafsi siamini kabisa kama serikali imetuma wasiojulikana kama waitwavyo kwenda kumdhuru Mh Tundu Lissu lakini pia siwalaumu watu wanaofikiria hivyo kutokana na viashiria fulani vinavyoendelea. Siamini kabisa kwamba kweli bunge limeshindwa kumtuma muwakilishi kwenda Nairobi kumjulia hali Lissu. Pili inawezekanaje wabunge wachangie matibabu ya mbunge mwenzao lakini pesa zisipelekwe hospitalini?????

Huko nyuma nilijitahidi sana kutojihusisha na malumbano ya hawa wasiojulikana lakini uzalendo umenishinda serikali hii ina swali kubwa na gumu sana ya kulijibu kuhusu hii assassination attempt ya Mh Lissu.

Ifike wakati tuache mapenzi kwa vyama kwa wenye vyama ukweli uelezwe kwamba Serikali ina wajibu mkubwa sana wa kuieleza jamii nini na nani alitaka Lissu afe na kwanini. Maana bila kumtafuta huyo asyejulikana basi sisi raia hatutakosea kumuunga mkono Mbowe kuwa suspect ni vyombo vyetu vya usalama ambavyo kikatiba vina kazi moja ya kutulinda sisi raia akiwepo na mheshimiwa Tundu Lissu na siyo kutudhuru.

Viashiria nilivyodokeza hapo juu ni pamoja na kuwakamata watu walioenda kujitolea damu ama waliojikusanya kufanya maombi. Serikali inayojali maisha ya raia wake haifanyi mambo kama haya tuliyoyaona wiki mbili zilizopita. Matukio kama haya yakitokea katika nchi zinazojali raia wake hata cabinet inakutana dharula kujadili lakini Tanzania viongozi wanapiga porojo.

Nilibahatika kuishi UK. Wenzetu vitukio hata vidogo kama hivi kamati ya ulinzi na usalama inakaa kujadili na inakua chini ya Prime Minister wanaiita Cobra. Hapa kwetu watu wanapigwa kama kuku ama nyati kibiti hakuna hata kitu kinachoendelea.

Pili kuhusu suala la maombi pia wao wanakutana katika open space na inakua live wanaita vigil polisi wanakua pale kuwalinda raia lakini Tanzania polisi wanaenda kusambaratisha raia. Halafu polisi wakiuawa na wananchi wakifurahia mnawalaumu kwanini mnawalaum? Nani anamuonea huruma mtu mnyanyasaji watanzania siyo Yesu aliyewaambia watesi wake hawajui walitendalo.

Mwisho ningeomba wanasiasa wa upinzani wamuige mwenyekiti wao Freeman Mbowe wakati wakiwa wanaongea na vyombo vya habari wasiongee kwa jazba zaidi bali ukweli wauweke mbele bila kutia chumvi ama kutoongea vitu ambavyo hawana uhakika navyo.

Kwetu sisi wanajamii wito ni moja tuache speculation tuwasikilize Wahusika kama kina Mbowe zaidi ya kusikikiza magazeti ya udaku kama mwanahalisi ama Uhuru na mzalendo.

Nakaribisha kukosolewa lakini siyi matusi.

Mungu mbariki Tundu Lissu mpatie unafuu auridi tulumbane kihoja na siyo kutumia bunduki.

Mbase mbase
Dj hana lolote huyo, na huyo Tundu lisu tunamuombea sote ila akipona asikae Tanzania maana ataungana na mabepari
kutuibia madini yetu na kuwatetea mabepari hao.
 
Mtoa mada umeandika sana maneno mengi lakini elewa kuwa issue ni moja tu.Chadema hawataki kabisa ushirikiano na Serikali wakiamini Serikali ndiyo iyofanya hayo kwa Tundu Lissu.
 
Hayo ndiyo maoni yako. Tundu Lissu ni raia halalibwa Tanzania tena zaidi yq Magufuli maana magufuli ni mnyambo labda ni mtu wa burundi ama Rwanda hivyo wewe huna haki ya kumuamlia wapi ahamie
 
Mtoa mada umeandika sana maneno mengi lakini elewa kuwa issue ni moja tu.Chadema hawataki kabisa ushirikiano na Serikali wakiamini Serikali ndiyo iyofanya hayo kwa Tundu Lissu.
Nakubaliana nao sababu huko nyuma hawakusaidia kipi kinakufanya uamini kama safari watakua wa msaada? Na Mbowe kalizungumza hilo jana. Labda rudia kuisikiliza ike press conference mkuu
 
Back
Top Bottom