Tumejiandaa vipi kukabiliana na wimbi la "internally displaced persons"?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,911
Bomoabomoa ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni bila shaka itazilishi wimbi kubwa la watu wasio na makazi mithili ya watu wanaokimbia vita(wakimbizi), hawa wakwetu wakiwa kama ni wakimbizi dani ya nchi yao.

Kwasababu zoezi hili ni la nchi nzima na linaloashiria watu wengi kukosa makazi kutokana na bomoabomoa hiyo endapo itatekelezwa kama ilivyopangwa.

Sasa je,wananchi na serikali tumejipanga vipi kuwahudumia watu hawa?

Tumejiandaa vipi na mlipuko wa magonjwa?

Tukumbuke pia hivi sasa kuna mnvua zinaendelea na pia tulishapewa onyo la mnvua za Elnino siku za nyuma kidogo.

Ni bora kushughulika na wamabondeni kwanza kabla ya kufikiri na hao waliojenga katika maeneo mengine yasiyoruhusiwa.

Fikiri kabla ya kutenda.

Kazi kwenu wenye mamlaka maana lawama hapa hazikwepeki licha wananchi kujenga kiholela ila mkumbuke serikali nayo ilikuwepo wakati wananchi hawa wanajenga na kibaya zaidi kuna madai kuwa serikali ilikuwa ikikusanya kodi ya majengo(property tax) kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo.
 
Last edited:
Wakati wanaambiwa wahame ulikua wapi?walipewa hadi viwanja vya bure mabwe pande,wengine waliuza na wengine waligoma kutoka mjini.acha sheria zifuatwe
 
Wakati wanaambiwa wahame ulikua wapi?walipewa hadi viwanja vya bure mabwe pande,wengine waliuza na wengine waligoma kutoka mjini.acha sheria zifuatwe
Una hakika hili zoezi la sasa ambalo ni kubwa zaidi na la nchi nzima linafanywa/litafanywa sambamba na tahadhari hiyo?!

Kama hakuna fidia,watajenga na hela gani?

Wakikosa makazi,unatarajia ni nini kitatokea?
 
U
Wakati wanaambiwa wahame ulikua wapi?walipewa hadi viwanja vya bure mabwe pande,wengine waliuza na wengine waligoma kutoka mjini.acha sheria zifuatwe[/QUOT
Kabla sijatoa hoja kuhusu bandiko lako nahitaji kufahamu umri wako tafadhali
 
Hali ni mbaya, naona neno busara na hekima limekuwa ni kitendawili kwa serikali ya sasa
 
Naomba busara na hekima ichukue mkondo wake kwenye hili zoezi wananchi wanaumizwa sana kama ni kijenga mji mpya mzuri basi itafutwe busara kutafuta sehemu nyingine
 
Wakati wanaambiwa wahame ulikua wapi?walipewa hadi viwanja vya bure mabwe pande,wengine waliuza na wengine waligoma kutoka mjini.acha sheria zifuatwe
waliopewa viwanja ni wale wa jangwani, kigogo na kinondoni, vipi na wale wa mwanza, mbeya, mbezi beach pale bondeni
 
Una hakika hili zoezi la sasa ambalo ni kubwa zaidi na la nchi nzima linafanywa/litafanywa sambamba na tahadhari hiyo?!

Kama hakuna fidia,watajenga na hela gani?

Wakikosa makazi,unatarajia ni nini kitatokea?
Kwakweli ninasikitishwa sana na serikali yangu jinsi inavyofanya maamuzi yake bila kutumia hekima, viongozi wanapaswa kuomba mwenyezi Mungu awajaalie busara ya hali ya juu kwenye maamuzi yao
 
Muafrika haendi bila fimbo. Wakiendelea kuwabembeleza hamna kitu kitafanyika halafu bdae mje kulalamika serikali haijafanya kitu, wachukulie hayo kama maafuriko wakajipange upya
 
Muafrika haendi bila fimbo. Wakiendelea kuwabembeleza hamna kitu kitafanyika halafu bdae mje kulalamika serikali haijafanya kitu, wachukulie hayo kama maafuriko wakajipange upya
Ingekuwa babako alijenga pale na labda ndio amestaafu hamna pa kukimbilia maana aliotumikia serikali na viwanja wakaviuza kwa 15000 kwa square meters je ungeongea haya unayoongea???? Najaribu kifikiria tu
 
W
Muafrika haendi bila fimbo. Wakiendelea kuwabembeleza hamna kitu kitafanyika halafu bdae mje kulalamika serikali haijafanya kitu, wachukulie hayo kama maafuriko wakajipange upya
Najaribu kuwaza kama watu wote tungekuwa tunawaza kinamna hiyo sijui unataka wakajipange wakiwa wapi????
 
Ingekuwa babako alijenga pale na labda ndio amestaafu hamna pa kukimbilia maana aliotumikia serikali na viwanja wakaviuza kwa 15000 kwa square meters je ungeongea haya unayoongea???? Najaribu kifikiria tu

Ningemwambia dingi ulizingua kujenga sehemu isiyo halali bila hata kupewa hati ya nyumba, huo ni simply uvamizi. Sasa tujipange upya tuchukulie kama nyumba imesombwa na maji au imeungua Hakuna namna. Muafrika haendi bila fimbo
 
Serikali pamoja na kutekeleza zoezi la bomoabomoa ingkuwa busara kama hawa wahanga watengewe maeneo, wale waliopewa kabla wasihusike ila wapya wapewe ili wenye kuhama kwa hiari wafanye hivyo ila sio namna hii mambo yanavyopelekwa
 
Ningemwambia dingi ulizingua kujenga sehemu isiyo halali bila hata kupewa hati ya nyumba, huo ni simply uvamizi. Sasa tujipange upya tuchukulie kama nyumba imesombwa na maji au imeungua Hakuna namna. Muafrika haendi bila fimbo
Wewe ni mwafrika au mzungu au yellow??
 
waliopewa viwanja ni wale wa jangwani, kigogo na kinondoni, vipi na wale wa mwanza, mbeya, mbezi beach pale bondeni
Tena walikuwa na bahati kupewa viwanja.ujenge kwenye mto upewe kiwanja cha bure?hakuna popote upuuzi huu
 
Nd
Muafrika mgumu mweusi hadi rohoni
io maana unaamini mwafrika haendi bila kuchapwa fimbo sababu hata babako alikufundisha kwa kukupiga kama mbuzi, poleni waafrika kama ndio akili zenu haziendi bila kupelekwa kama punda, nimekuelewa nimejua naongea na mtu mwenye mentality ya aina gani, nafunga mjadala!!!
 
Fimbo ni lugha ya picha. Unafikiria ka mtoto wa std2 jiongeze
 
Zoezi ni zuri lakini madhara ni makubwa sana kwa watu wa uchumi wa chini. Gharama za kujenga ni kubwa sana so ni kama kuwarudisha nguma watu kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom