Tumejiandaa vipi kukabiliana na UVIVU, Uzembe na Kukosa uwajibikaji Serikalini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumejiandaa vipi kukabiliana na UVIVU, Uzembe na Kukosa uwajibikaji Serikalini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoto Wa Mbale, Oct 18, 2011.

 1. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nchi yetu inakabiliwa na changamoto nyingi. Uchumi wetu unaporomoka kwa kasi ya ajabu, huku lawama nyingi zikielekezwa kwa serikali. Ni haki ya watanzania kuiwajibisha serikali kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kusimamia mgawanyo bora wa utajiri wa rasilimali kwa manufaa ya watu wake.

  Lazima tuwe wakweli hapa, wengi wetu tunataka mabadiliko. Serikali ya ccm imeshindwa kusimamia uchumi wa Taifa, uporaji na wizi ni mambo ya kawaida katika serikali hii. Hata hivyo, watendaji wengi na vijana wengi walio nje ya mfumo huu wamekunywa sumu hatari ya ufisadi. Ili tuendelee hatuna budi kuiondoa sumu hiyo haraka kwani itazorotesha juhudi zetu za kuwa na Tanzania yenye neema inayoongozwa na chama mbadala.

  Tufanye nini kama taifa ili kudhibiti roho za kifisadi zisiwaingie au kuondoa zilizoingia kwa watanzania ambao lazima tutawahitaji katika kuijenga Tanzania mpya?
   
Loading...