las Casas
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 575
- 711
Nilikuwa Moshi juzi kati, yaani nilizani Niko dar , jua ni Kali sanaKama hujui ni kwamba mji wa moshi kwa sasa unaongoza kwa kiwango cha joto ambalo kwa sasa limefikia nyuzi joto 36, jua ni kali ile mbaya hii yote ni matunda ya uharibifu wa mazingira.
Enzi za utawala wa Mangi Thomas Maraelle kulikuwa na sheria kali katika uhifadhi wa mazingira,watu hawakuruhusiwa kukata miti ovyo,enzi hizo kulikuwa na zaidi ya mito 20 iliyokuwa inatiririsha maji kutoka mlima Kilimanjaro,leo hali ni tete,karibu mito yote imekauka,vyanzo vya maji navyo hakuna na sasa kila kona ni kilio cha maji,hakuna maji ya uhakika kwa baadhi ya maeneo na mgao wa maji ni kama kawa japo wenyewe wanasema hakuna mgao wa maji.
Ndani ya mji wa maoshi kwa baadhi ya maeneo watu wanaamka usiku kusaka maji,hali ni mbaya mbaya kweli kweli,yote haya ni kwa sababu tumeharibu mazingira kwa kiwango cha kutisha.
Kun hatari pia ya kupugua kwa theluji ya mlima Kilimanjaro kama hatua za haraka hazitachukuliwa kukabiliana na hali hii ambayo itaendelea kuibua migogoro baina ya wakulima na wafugaji kila mmoja akitaka kunufaika na maji kwa kilimo na kwa kunywesha mifugo.
Wengi sasa wanamkumbuka Marehemu Leonidas Gama akiwa mkuu wa moa wa Kilimanjaro alisimamia vyema uhifadhi wa mazingira na kupiga marufuku ukataji miti ovyo kwa ajili ya matumizi ya mbao,kuni na mahitaji mengine na kwa hilo hakika alifanikiwa.
Baada ya kifo cha Gama watu wakavamia misitu ya asili wakafnaya yao leo ndo matunda ya uharibifu w mazingira tunayashuhudia.
Kazi kwenu watawala wa mkoa wa Kilimanjaro,msipochukua hatua leo kesho yaweza kuwa mbaya zaidi,joto litaendelea kututesa ile mbaya na maji yatakuwa bidhaa adhimu sana