Tumeharibu mazingira sasa maji ni shida Kilimanjaro

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Kama hujui ni kwamba mji wa moshi kwa sasa unaongoza kwa kiwango cha joto ambalo kwa sasa limefikia nyuzi joto 36, jua ni kali ile mbaya hii yote ni matunda ya uharibifu wa mazingira.

Enzi za utawala wa Mangi Thomas Maraelle kulikuwa na sheria kali katika uhifadhi wa mazingira,watu hawakuruhusiwa kukata miti ovyo,enzi hizo kulikuwa na zaidi ya mito 20 iliyokuwa inatiririsha maji kutoka mlima Kilimanjaro,leo hali ni tete,karibu mito yote imekauka,vyanzo vya maji navyo hakuna na sasa kila kona ni kilio cha maji,hakuna maji ya uhakika kwa baadhi ya maeneo na mgao wa maji ni kama kawa japo wenyewe wanasema hakuna mgao wa maji.

Ndani ya mji wa maoshi kwa baadhi ya maeneo watu wanaamka usiku kusaka maji,hali ni mbaya mbaya kweli kweli,yote haya ni kwa sababu tumeharibu mazingira kwa kiwango cha kutisha.

Kun hatari pia ya kupugua kwa theluji ya mlima Kilimanjaro kama hatua za haraka hazitachukuliwa kukabiliana na hali hii ambayo itaendelea kuibua migogoro baina ya wakulima na wafugaji kila mmoja akitaka kunufaika na maji kwa kilimo na kwa kunywesha mifugo.

Wengi sasa wanamkumbuka Marehemu Leonidas Gama akiwa mkuu wa moa wa Kilimanjaro alisimamia vyema uhifadhi wa mazingira na kupiga marufuku ukataji miti ovyo kwa ajili ya matumizi ya mbao,kuni na mahitaji mengine na kwa hilo hakika alifanikiwa.

Baada ya kifo cha Gama watu wakavamia misitu ya asili wakafnaya yao leo ndo matunda ya uharibifu w mazingira tunayashuhudia.

Kazi kwenu watawala wa mkoa wa Kilimanjaro,msipochukua hatua leo kesho yaweza kuwa mbaya zaidi,joto litaendelea kututesa ile mbaya na maji yatakuwa bidhaa adhimu sana
 
Yaani wenyeji waharibu mazingira halafu iwe hujuma dhidi ya wenyeji?,ni akili au matope?,waanoishi kuznugmza mlima Kilimanjaro ni wahamiaji au ni wenyeji?

Wanaoishi kuzngumza msitu wanusu maili ni wageni au niwneyeji?,siyo kia utmobunwekwa hapa,huo wa kwako ni utumbo na habari ya Ben sanane ina uhusiano gani ya hali ya uharibifu wa mazingira?
 
Kulinda mazingira ni jambo la msingi na muhimu sana.

Ila kuhusu joto kuwa kali hapo Moshi ni suala la kijiografia zaidi.
Miaka yote eneo la Moshi mjini huwa lina joto kuliko maeneo mengi ya Tz, kwa mwaka huu hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia ukosefu wa mvua za vuli kwa wakati.

Vilevile kuyeyuka kwa barafu ml. Kilimanjaro pia ni tatizo la kidunia linalotokana na kuongezeka kwa joto(global warming).
Kuotesha miti ni sawa ila usifikiri itazuia hii barafu kuyeyuka.

Mengine uliyoeleza ni sawa.
 
Yaani wenyeji waharibu mazingira halafu iwe hujuma dhidi ya wenyeji?,ni akili au matope?,waanoishi kuznugmza mlima Kilimanjaro ni wahamiaji au ni wenyeji?,wanaoishi kuzngumza msitu wanusu maili ni wageni au niwneyeji?,siyo kia utmobunwekwa hapa,huo wa kwako ni utumbo na habari ya Ben sanane ina uhusiano gani ya hali ya uharibifu wa mazingira?
Unakumbuka walivyomuharibia Braza Mbowe miundo mbinu ya shamba lake kwa maksudi? Watashindwaje kuwafanyia hujuma wenyeji? Sio hivyo tu hata Moshi wameifanyia mizengwe isiwe jiji!
 
Kama hujui ni kwamba mji wa moshi kwa sasa unaongoza kwa kiwango cha joto ambalo kwa sasa limefikia nyuzi joto 36, jua ni kali ile mbaya hii yote ni matunda ya uharibifu wa mazingir...
Afu wangese hawa viongozi wa dini watakuja na yao eti tufunge tuombe Mungu atupe mvua, nyoko zenu badala ya kuwafundisha waumini wenu kwa miti ndiyo miungu yenyewe inayotufadhili kwa hewa safi, dawa, chakula.

Kivuli na mema mengi yatokanayo na miti, lakini tunaikata ikiisha tunaenda kuomba Mungu asiyejulikana, hasikiki, haonekani ila tu ameandikwa kwenye vitabu vya dini eti tumuabudu, hivyo vitabu vimetoka wapi? Nani aliye compile na kuwaleta binadamu ujinga wa dini?

Haya ombeni mungu alete mvua sasa
 
Suala la Moshi kuwa Jiji wamefanyiana mizengwe weenyeji wenyewe,unafamhamu mzee Lyatuu wa YMCA?,huyu akiwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi alisambaza taarifa hadi makanisani akiwataka wananchi wa Moshi vijijini wasitoe ardhi yao ikamezwa na Moshi mjini ili iwe Jiji na mpaka leo Wauru,waold Moshi,watu wa Sango,Kibosho,Maili sita,hawako tayri ardhi yao imezwe kuwa Jiji,kama hujui hii mambo ya Jiji tuulize utapata majibu mazuri sana bro,usikurupuke bro.

issue ya Mbowe ni mambo ya kisiasa hakuna asiyejua na aliyendesha huo uharamia sote tunajua yuko wapi maana maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni mauti,Sabaya huko aliko anavuna kile alichopanda
 
Duh.... Poleni sana ndugu zetu... Sie huku bado tuna andaa mashamba msimu wa kilimo umefika..... Karibuni sana wateule....
 
Kama hujui ni kwamba mji wa moshi kwa sasa unaongoza kwa kiwango cha joto ambalo kwa sasa limefikia nyuzi joto 36, jua ni kali ile mbaya hii yote ni matunda ya uharibifu wa mazingira...
Maeneo gani Kilimanjaro wanaamka usiku kwenda kupanga foleni ili wapate maji?
 
Ni hujuma dhidi ya wenyeji kutoka serikali dhalimu ya CCM yenye chuki za kisoro.

Show us the remainings of our beloved brother Ben Saanane so that we can give him a decent burial. He deserves that!
Siku nilipomsikia mbunge Selasini kipindi hicho akieleza ujumbe aliopewa na watu wa kwao ili aufikishe bungeni juu ya Ben Saanane ilikuwa inaumiza sana. Ujumbe wake uliweza kuwaliza watu. Alisema watu wamemtuma wafanye matanga au wafanyaje mana wako njia panda. Ibilisi joka kuu hata watu wamteteeje alikuwa dhalimu.
 
Kama hujui ni kwamba mji wa moshi kwa sasa unaongoza kwa kiwango cha joto ambalo kwa sasa limefikia nyuzi joto 36, jua ni kali ile mbaya hii yote ni matunda ya uharibifu wa mazingira...
Kule mabogini, kahe, Rau forest, hali sio nzuri eh

Ile half mile strip forest at the foot of Mt.Kilimanjaro watu wanrombo wame amua kuivamia na kukata kuni ? Eh
 
Kulinda mazingira ni jambo la msingi na muhimu sana.

Ila kuhusu joto kuwa kali hapo Moshi ni suala la kijiografia zaidi.
Miaka yote eneo la Moshi mjini huwa lina joto kuliko maeneo mengi ya Tz, kwa mwaka huu hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia ukosefu wa mvua za vuli kwa wakati.

Vilevile kuyeyuka kwa barafu ml. Kilimanjaro pia ni tatizo la kidunia linalotokana na kuongezeka kwa joto(global warming).
Kuotesha miti ni sawa ila usifikiri itazuia hii barafu kuyeyuka.

Mengine uliyoeleza ni sawa.
Mleta mada ana hoja, ukataji miti na uharibifu wa misitu kiukweli umekithiri, mfano msitu wa hifadhi wa Kahe unsopakana na vijiji vya Oria, Mwangaria na vingine umeisha wootee, hata scheme ya irrigation ya Chekereni maji yamepungua sanaa..
 
Back
Top Bottom