Tumehamasishwa kujenga vyoo vya kisasa tumejenga lakini maji hakuna hili suala limekuwa kama siasa kwetu siku moja hawa wandisi tutawapa maji tunayo k

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
Tatizo la Uhaba wa Maji Katika Tarafa ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Limeendelea Kuota Mizizi Kutokana na Ukame Unaosababisha Wakazi Wake Kulazimika Kutumia Maji Machafu Ya Madimbwi.

Miongoni Mwa Wakazi Wanaolalamikia Tatizo la Uhaba wa Maji ni Pamoja na Wakazi wa Kata ya Saja Ambao Wamemtupia Lawama Mbunge Wao Alipofanya Ziara Ya Kikazi Katika Jimbo Lake la Wanging'ombe.

Clever Nywage na Golden Miho Ni Wakazi wa Saja Ambao Mbele ya Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Mhandisi Gerson Lwenge Wamepata Kuhoji ni Lini Kilio Cha Maji Kitaisha Kwani ni Kipindi Kirefu Wamekuwa Wakiomba Maji bila Mafanikio.

"kuliku na msemo unaosema usichukulie poa nyumba ni choo,sasa tumehamasishwa kujenga choo zile za kutumia maji na maji kwetu huku ni adimu na tunaahidiwa huenda ikawa 2020 hapa kati kati tutaendeshaje maisha bila maji? tulidanganywa mwanzoni kabisa kuwa maji yatakuja lakini lile wazo lilipotea kabisa sasaivi tunasema maji tutazamie hapo baadaye"walihoji wananchi

Pamoja na Ukweli Kwamba Tatizo la Maji ni La Kitaifa Lakini Wakazi Hao Akiwemo Gidion Sapy Ameendelea Kusisitiza Ahadi Ambazo Zimekuwa Hazitekeleziki Juu ya Maji Jambo Ambalo Wanadai Wamekuwa Wakinywa Maji Yanayotumiwa na Mifugo.

"siku moja hawa waandisi hawa wanao tudanganya nao tuwape maji tunaokunywa sisi watu wasaja maana sisi tunakunywa yale yale tunayo kunywa na mifugo"wananchi waliongeza

Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Mhandisi Gerson Lwenge Pamoja na Wataala wa Maji Toka Halmashauri ya Wialaya Hiyo Wanakiri Kuwapo Kwa Tatizo Hilo Huku Wakisema Serikali Bado Inaendelea Kushughulia Siku Hadi Siku.
"swala la maji hata mimi linaniumiza sasa ni jambo ambalo linanikera tumekuwa tukijitahidi kila linawezekana hata huo mradi wa milioni mia tatu tukaweka mkandarasi anafanya ukarabati wa manteki kila wakati nikaambiwa maji yanatoka kumbe yanatoka nikija mimi tu nikiondoka hakuna kitu"alisema mbunge

Mhandisi Mussa Masasi ni Meneja wa Mamlaka ya Maji Wanging'ombe WANGIWASA Ambaye Anakiri Kuwa Kwa Sasa Licha ya Kuwapo Kwa Tatizo la Upatikanaji wa Maji Lakini Limepungua na Bado Kuna Mikakati Mizuri ya Kushughulikia Tatizo Hilo.

Kila Pahala Nchini Tanzania Kumeonekana Kuwapo Kwa Malalamiko ya Uhaba wa Maji Jambo Ambalo Serikali Kupitia Bajeti Ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji Inapaswa Kulipa Uzito Suala Hilo Ili Kuondoa Kero Kubwa Kwa Watanzania.

mc.amiri/mr.mtaani

SAUTI HIZI HAPA CHINI
 

Attachments

  • MAJI.MP3
    1.5 MB · Views: 11
  • MBUNGE NA WATAALAM.MP3
    942.6 KB · Views: 6
  • MENEJA WANGIWASA.MP3
    1.3 MB · Views: 9
  • REPORT AMIRI KILAGALILA SAFIIII.mp3
    4 MB · Views: 8
  • WANANCHI SAJA.MP3
    1.1 MB · Views: 8
Back
Top Bottom