Tumegundua Siri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumegundua Siri!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,448
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Tumegundua Siri!

  Hello dada Jane,

  Naamini unaendelea vizuri na mumeo James,

  Leo nimeona nikuandikie waraka kukujibu lile swali lako uliloniuliza kwamba nini hata baada ya kutimiza miaka 30 katika ndoa yetu na mume wangu John, bado tunaendelea ku-enjoy sex at maximum kuliko wakati wote katika maisha yetu, mwenzangu lazima tukueleze wazi kwani ndoa yako bado changa sana miaka 4 na sex kwa mwezi mara moja au mbili tena kwa dakika 5 tu, Pole sana!

  Kuna siri moja ambayo tumeigundua na mimi na mume wangu ni watu wa vitendo na si maneno, tuliamua kwamba kama kweli kufanya hili jambo kabla ya kuwa mwili mmoja lina maana na huleta matokeo tuliamua kufanyia kazi kwa nguvu zote.

  Tumeamini usemi kwamba:-
  “Great prayers are the way to great sex”

  Si nilikwambia tulisoma kila aina ya vitabu na kupata kila aina ya mafundisho hata hivyo tukajikuta hakuna kitu hata hivyo kwa kuomba ya pamoja kabla ya sex tumeona mabadiliko zaidi na kwa kweli tunapokuwa faragha ni kama tunapaa hewani huwa tunahisi kama tumechukuliwa na International Space shuttle kwenda anga za mbali, ni raha na inabariki sana.

  Pia tumegundua kwamba:-
  “Sex at its best is spiritual”

  Ni kweli tumegundua kwamba miili huunganika vizuri pale roho zinapounganika zaidi na njia nzuri ni maombi ya pamoja hivyo kabla ya tendo la ndoa tunaanza kwa maombi, kuombeana na pia kuomba Mungu atusaidie ili tunapopeana zawadi ya mwili kila mmoja apate raha nk.

  Sasa hivi nikimsikia mume wangu John ananiambia twende chumbani kuomba mwili mzima unanisisimka na najua sasa raha inakuja na kuridhika kumewadia acha tu…….

  Pia tumegundua kwamba kila kitendo cha kuomba pamoja (mara nyingi tukiwa tumekumbatiana) na kuwa karibu kiroho na kimwili hutusaidia kufanya discovery ya qualities za ndani na nje ambazo bila maombi tusingeweza kuziona na hivyo kupendana zaidi, ni kama kila siku namuona mume wangu ni mpya na anang'aa zaidi katika tabaia na u-handsome wake, eti naye anasema siku hizi nimekuwa mrembo ya uhakika na pia tabia yangu ni nzuri sana, naamini ni kwa sababu ya maombi.
  Hii ina maana kwamba kumbe maombi hunua hata sifa njema ambazo zimejificha na zaidi kila tunavyoendelea kuombeana ndivyo tunavyozidi kufanya discovery ya vitu vingi zaidi, quality nyingi zaidi, positive nyingi zaidi na mambo mazuri mengi zaidi na matokeo yake mume wangu ananiambia siku hizi mimi ni mzuri zaidi na mtamu zaidi wakati huohuo na mimi namuona yeye ni mzuri na mtamu zaidi.

  “Ninamuona special na yeye ananiona mimi ni special”

  Kawaida ndoa inavyozidi kuendelea uzuri wa mume na mke huanza kuchakaa na wanandoa huweza kufikia kiwango cha kuchokana, tumegundua ni maombi peke yake huweza kuendelea kuwaboresha na kuwafanya wanandoa wasichakae wala kuchuja, si unaona sisi tuna miaka 30 katika ndoa na ndoa inazidi kuwa tamu, kweli maombi ni jibu.

  Waingereza wanasema
  “Prayers at its best are great Unifiers”
  Tumeamini kwamba huu usemi ni kweli tupu.

  Hivyo dada Jane kama unataka wewe na mumeo james mambo yawe sawa usisahau hii siri ya kuomba pamoja kabla ya kuwa mwili mmoja.

  Kumbuka:-
  “Jinsi Mume na Mke wanavyoweka urafiki pamoja na Mungu kwa njia ya maombi, ndivyo Mungu anavyoidi kuimarisha urafiki kati ya mke na mume”

  Ni mimi rafiki yako
  Neema (Mrs John)

  (Ndugu msomaji James & Jane, John na Neema ni majina ambayo si ya watu ninaowafahamu ni majina yamewekwa tu kufanya ujumbe ukamilike)
   
 2. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  :rolleyes::pasante kwa maada nzuri, imenibariki sana
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Amen.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  "Prayers at its best are great Unifiers"

  Thanks is al urs bro.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Aisee sasa simnaweza mkajikuta mmeanza kufanya mambo huku mnaomba! Halafu wanapoomba huwa wamekumbatiana sasa sijui wakiwa na nguo au la
   
 6. GP

  GP JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  na wale wasio wanandoa wanaruhusiwa kuomba?
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,829
  Trophy Points: 280
  Hahaha mpwa. Bila kuomba access itakuwa denied (Sorry, off topic)
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ile jukwaa la mapenzi limejaa?
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kuchunguza sana mapenzi yapo kila sehemu,kanisani,kwenye siasa.kila mahali,ni vile tu tunatafsiri mbaya ya mapenzi.Lakini bila mapenzi dunia hakuna.
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hao hawaruhusiiwi kabisa kwa vile ni uzinzi na uasherati na Mungu hasikilizi.Vinginevyo wamuombe baba yao shetani huyo atawasikiliza.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Watu hawajui hii kitu, Omba kabla ya kumega utaona matokeo yake na mkimaliza mumshukuru mungu sio mnakoroma tuuu
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Eti wamegundua siri!

  ...'sala' ingekuwa siri basi muadhini asingenadi sala miskitini, wala kengele zisingewaita waumini makanisani...

  Kwenye mafunzo ya ndoa mw'mungu anahusishwa, kwenye ndoa anahusishwa, ...nyie wenyewe wanandoa mkishayaanza maisha mnakaribisha shetani.

  Anyway, heri yenu mliopata tena mwanga wa kumkumbuka. Wenzenu huamua kusongesha mbele kwa mbele na shetani wao!
   
 13. d

  deez New Member

  #13
  Nov 16, 2009
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mr and mrs John hayo maisha yenu nayakubali mungu aendelee kuwaweka pamoja
   
Loading...