Tumefungua anga kwa watalii, tumejihakikishia kwamba hawawezi kutumika kutuua kibiashara?

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
644
1,271
Hapa najaribu kwaza kwa sauti kuruhusu watalii kipindi hiki ambapo nchi nyingi bado wanaripoti visa vingi tu vya maambukizi mapya kila siku.

Hivi ikitokea nchi moja ikatuchezea mchezo, wakapandikiza watalii, wakaja na vyeti vyao viko negative, halafu wanaporudi kwao baada ya utalii wao wakaripotiwa kuwa wamepimwa na kukutwa positive ili kutafsiri kwamba wamepata maambukizi huku kwetu Tanzania.

Sakata hili haliwezi kutudidimiza zaidi? Kigwangala amejipanga juu ya hili?

Kama jirani zetu tu kila dereva aliyekuwa anapimwa wa Tz alikutwa positive, hii haiwezekani kwa hao mabeberu kutupandikizia watalii wenye lengo maalumu?

Tunapenda kweli hali irudi kawaida ila tunapojitanguliza mbele wakati hata ripoti tulikuwa hatutoi ni rahisi kufanyiwa hujuma.
 
Kibiashara ya utali,duh.
Tunamuomba Mungu tu maana ye ndie anaejua kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom