Tumefika hapa kwasababu ya CHADEMA, wanapaswa kuenziwa!

Haya Mkuu japo mi napatwa na shaka unaposema huna chama, na kinachonipa wasiwasi ni jinsi ulivyo na bidii katika hili jukwaa ambalo ni maalum kwa ajili ya siasa.
hii bidii ungekuwa nayo kule kwenye jukwaa la sheria ambako wengi wanahitaji msaada wako japo wa kiushauri tu ungekuwa umeitendea haki taaluma yako.

badala ya ku-balance kati ya chadema na CCM kwenye jukwaa la siasa ambayo unakiri huna chama. mi naona itakuwa vema zaidi uki-balance michango yako katika jukwaa la sheria ambapo una taaluma napo. Wasalaam

#DG
 
Kule nipo pia hadi nina mada ambayo ni Sticky
 
Ukweli lazima usemwe. Nimekuwa nikiusema ukweli bila kujali mjadala unaofuata kuhusu hoja yangu. Ni kwakuwa sina upande wowote wa kisiasa ninaouegemea. Ingawa sina uanachama au ushabiki wa chama chochote cha siasa hapa nchini au kwingineko, nimekuwa nikipewa uanachama na kuhamishwa kutoka chama kimoja hadi kingine kila mara kulingana na mada zangu. Nausimamia ukweli daima.

Kama nchi, tumefikia katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi. Vita dhidi ya madhila hayo ya kitaifa imepamba moto na inaendelea vyema chini ya uongozi wa Rais Dr. John Pombe Magufuli. Ingawa bado haijafanikiwa kwa aslimia mia moja, nia na matendo ya kupinga rushwa,ufisadi na uhujumu uchumi yanatosha kupunguza, kuwafunza adabu na 'kuwatisha' wahusika. Ni mwanzo mzuri na wenye kila aina ya matumaini.

Kama nchi, tupo katika jitihada kubwa za kulinda rasilimali zetu ili zitunufaishe. Tupo kwenye mikakati mizito kimaneno na kimatendo ya kuzilinda na kuzipigania rasilimali zetu za kitaifa kama madini, Wanyama na nyinginezo. Katika kuonyesha nia thabiti katika hilo, kuna mabadiliko mbalimbali ya kisheria yameshafanyika katika kulinda na kuzifanya rasilimali zetu zitunufaishe. Ni jambo jema na kuungwa mkono.

Kama nchi, tupo katika jitihada na mipango kabambe ya kuimarisha uchumi wetu na hata kuimarisha miundombinu. Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imejipambanua katika kuimarisha uchumi wa viwanda; uimarishaji wa miundombinu mbalimbali kama barabara, madaraja, reli na uzalishaji wa nishati ya umeme. Serikali ya awamu ya tano iko thabiti katika kuisimamia nia yake hiyo ya kiuchumi.

CHADEMA, kama chama kikuu cha upinzani nchini, kimekuwa kikipigania mambo yanayosimamiwa sasa na Serikali kwa muda mrefu. CHADEMA imekuwa ikipinga waziwazi ufisadi, wizi wa mali za umma, rushwa na uhujumu uchumi. Imekuwa ikipigania kulindwa kisheria kwa rasilimali zetu za taifa na hata kuimarishwa kwa uchumi. pamoja na kuandamwa na changamoto mbalimbali wakati eote huo, Wabunge na viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiyasimamia hayo.

Ushahidi mkubwa wa mambo hayo kutoka CHADEMA ni Hansard za Bunge zilizo na 'mapambano makali' ya kupinga ufisadi kama wa Richmond, EPA, Escrow, Buzwagi na kadhalika. Pia, Hansard za Bunge letu tukufu zina kumbukumbu adimu za Hoja mbadala na maridhawa za upinzani kuhusu uimarishwaji wa uchumi, miundombinu na uwezeshwaji wa wananchi kimapato. Katika kila Hotuba za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni za kibajeti, CHADEMA imekuwa ikishauri na kuasa kuhusu mambo mbalimbali ya kisekta ambayo kwasasa yanaing'arisha Serikali yetu.

Hakika, kwa tunachofanya na tunachokisimamia, tumefika hapa kwa sababu ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini. Wanapaswa kutetewa, kuombewa na kuenziwa.
absolutely true,kwa spirit na hulka ya magufuli angewaruhusu hawa wapinzani wakawa na fair ground ya kufanya siasa kama ilivyokuwa kw jk,angemulikiwa uozo mwingi na kw hatua anazochukua angeweka record ya pekee ktk watawala walio wahi kutokea
 
We ni mtoto wa mjini tu kama wengine. Huko unakooga ndio tulikuwa tunanawa.
Huyu sio mtoto wa mjini alikuja mjini na treni maana hauwezi kua mtoto wa mjini ukawa na akili za kindezi kama za huyu jamaa halafu nae ni mwanasheria jamaa anasikitisha sana huyu..tuambie kesi ya ufisadi ya nani imefanikiwa? Rugemalira tumeona huko mahakama ya kimataifa ikikubaliana kwamba Tanesco walipe hela? , procedural irregularity ya kujenga uwanja wa ndege wa chato?, procedural irregularities za kununua ndege?unequal treatment ya wenye vyeti feki? Wengine wakikingiwa vifua hivyo vitu vinaweka doubts nyingi sana kwenye hayo mapambano dhidi ya rushwa bila kusahau maswala ya usalama na watu kutekwa na kupotea hovyo..hata kama huyu bwana ni mnzani lazima atumie akili
 
Huo ndiyo ukweli usiyo pingika.ila kwakuwa tumehamia kusadikika, chini ya majivuno,ukweli utaitwa uongo na uongo utaitwa ukweli.
 
Lkn siyo chadema hii ya Mbowe, Tundu Lisu, Mrema &Co. labda kama kuna chadema nyingine, binafsi aliyetusaidia kufika hapa ni A.L. Mrema, huyo ndo aliyekuwa mpinzani aliyenifanya nichukie Wahindi mpaka leo hii lkn siyo hawa ma snitch chadema, angali kama huyu F.Karume hata asili yake ya Zanzibar anaikana shauri ya u snitch na kuanza kuunga mkono ushoga!
 
Bora Amber Ruth si mnafiki
 
Ukweli lazima usemwe. Nimekuwa nikiusema ukweli bila kujali mjadala unaofuata kuhusu hoja yangu. Ni kwakuwa sina upande wowote wa kisiasa ninaouegemea. Ingawa sina uanachama au ushabiki wa chama chochote cha siasa hapa nchini au kwingineko, nimekuwa nikipewa uanachama na kuhamishwa kutoka chama kimoja hadi kingine kila mara kulingana na mada zangu. Nausimamia ukweli daima.

Kama nchi, tumefikia katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi. Vita dhidi ya madhila hayo ya kitaifa imepamba moto na inaendelea vyema chini ya uongozi wa Rais Dr. John Pombe Magufuli. Ingawa bado haijafanikiwa kwa aslimia mia moja, nia na matendo ya kupinga rushwa,ufisadi na uhujumu uchumi yanatosha kupunguza, kuwafunza adabu na 'kuwatisha' wahusika. Ni mwanzo mzuri na wenye kila aina ya matumaini.

Kama nchi, tupo katika jitihada kubwa za kulinda rasilimali zetu ili zitunufaishe. Tupo kwenye mikakati mizito kimaneno na kimatendo ya kuzilinda na kuzipigania rasilimali zetu za kitaifa kama madini, Wanyama na nyinginezo. Katika kuonyesha nia thabiti katika hilo, kuna mabadiliko mbalimbali ya kisheria yameshafanyika katika kulinda na kuzifanya rasilimali zetu zitunufaishe. Ni jambo jema na kuungwa mkono.

Kama nchi, tupo katika jitihada na mipango kabambe ya kuimarisha uchumi wetu na hata kuimarisha miundombinu. Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imejipambanua katika kuimarisha uchumi wa viwanda; uimarishaji wa miundombinu mbalimbali kama barabara, madaraja, reli na uzalishaji wa nishati ya umeme. Serikali ya awamu ya tano iko thabiti katika kuisimamia nia yake hiyo ya kiuchumi.

CHADEMA, kama chama kikuu cha upinzani nchini, kimekuwa kikipigania mambo yanayosimamiwa sasa na Serikali kwa muda mrefu. CHADEMA imekuwa ikipinga waziwazi ufisadi, wizi wa mali za umma, rushwa na uhujumu uchumi. Imekuwa ikipigania kulindwa kisheria kwa rasilimali zetu za taifa na hata kuimarishwa kwa uchumi. pamoja na kuandamwa na changamoto mbalimbali wakati eote huo, Wabunge na viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiyasimamia hayo.

Ushahidi mkubwa wa mambo hayo kutoka CHADEMA ni Hansard za Bunge zilizo na 'mapambano makali' ya kupinga ufisadi kama wa Richmond, EPA, Escrow, Buzwagi na kadhalika. Pia, Hansard za Bunge letu tukufu zina kumbukumbu adimu za Hoja mbadala na maridhawa za upinzani kuhusu uimarishwaji wa uchumi, miundombinu na uwezeshwaji wa wananchi kimapato. Katika kila Hotuba za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni za kibajeti, CHADEMA imekuwa ikishauri na kuasa kuhusu mambo mbalimbali ya kisekta ambayo kwasasa yanaing'arisha Serikali yetu.

Hakika, kwa tunachofanya na tunachokisimamia, tumefika hapa kwa sababu ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini. Wanapaswa kutetewa, kuombewa na kuenziwa.
Ila inakuwaje mtu anayeomba na na ufisadi yeye anawahonga wanasiasa wa upinzani kwa pesa na vyeo ili wahamie kwake? Ufisadi unaweza kupigwa vita bila kuwepo kwa utawala wa sheria?
 
Hakika, kwa tunachofanya na tunachokisimamia, tumefika hapa kwa sababu ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini. Wanapaswa kutetewa, kuombewa na kuenziwa.
Acha kujifariji na kuendekeza mahaba
Chadema walimnadi mtu kwa miaka 8,kwamba ni fisadi lakini ndani ya dakika 30 wakampa tiketi ya kugombea urais!
Kama ni nchi za ulaya chadema wasingepata hata kiti cha udiwani
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom