Tumefika hapa kwa sababu ya Kikwete kumlea vibaya Ridhiwani kuihusisha familia yake kwenye masuala ya uongozi

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,897
Kikwete alipokuwa akitaka kugombea Urais mwaka 1995 Nyerere alimwambia kwamba wewe bado mdogo muachie Ben watu weengi waliamini hivyo ila ukweli Nyerere alimaanisha kuwa Kikwete alikuwa mdogo kwenye mambo ya kupewa kuiongoza Nchi yaani alimsoma mwenendo wa maisha yake na kugundua kuwa ni msumbufu na hafai kuwa Rais wa nchi Nyerere aliona mbali sana.

Kosa kubwa la kwanza alilolifanya Kikwete kwenye uongozi wake ni kuiruhusu familia yake kujiingiza moja kwa moja kwenye mamlaka ya Rais.

Tulishuhudia awamu ya Kikwete kijana mdogo kama Ridhiwani kujimilikisha makampuni meengi ya kilaghai na waliokuwa wasaidizi wa Ridhiwani nao kujiingiza moja kwa moja kwenye Utawala wa nchi.

Rais Mstaafu Kikwete aliporuhusu hata marafiki wake wa karibu kuingia kwenye masilahi ya Urais wake kwa njia ya utapeli hali hii imepelekea sasa kuhangaika sana wanapopata mtu ambaye hajali maslahi yao hii ni kwa sababu moja tu wanaendeleza biashara zao za kitapeli kipindi wawapo kwenye mifumo.

Ndio maana Nyerere alisema ni hatari sana kuingiza Ikulu Rais mfanyabiashara hali ikiendelea hivi kuna umuhimu sasa wa kuwa na mgombea binafsi ambaye bila huruma atakuja kuisafisha nchi.
 
Tulishuhudia awamu ya kikwete kijana mdogo kama Ridhiwani kujimilikisha makampuni meengi ya kilaghai na waliokuwa wasaidizi wa Ridhiwani nao kujiingiza moja kwa moja kwenye Utawala wa nchi
Bwashee ina maana pamoja na ile biashara ya kuuza sembe jamaa alikuwa na makampuni mengine? Aliposemaga anaishi "kimjinimjini" mi nikadhani ilikuwa ni hiyo biashara ya unga tu.
 
Bora Kikwete.

Magufuli na Nyerere wameingiza ndugu zao kwenye serikali, Nyerere alikuwa na kaka yake anaitwa Joseph Nyerere serikalini, pia alimchukua Butiku binamu yake kuwa katibu wake wa Ikulu
Magufuli alimchukua Binamu yake na kumkabidhi ubosi wa hazina

Magufuli is gone and is not coming back.

Hasara aliyotutia kwa miradi isiyokuwa na kichwa wala miguu inatosha, uonevu, siasa za kununua watu, ubambikiziaji watu kesi, uvurugaji chaguzi, kutoheshimu katiba, mambo ya magenge ya watu wasiojulikana, kutolipa stahiki halali za wafanyakazi, sheria kandamizi vyote hivi inabidi tuvireverse
 
Kikwete Urais wake ulikuwa wa ubia na familia na rafiki zake wakina 'ShKubar"!! Kama ataruhusiwa kuturudisha huko kutatokea backlash kubwa kutoka kwa wananchi na Samia hata kuwa salama na utawala wake!!
acheni kumtisha rais aisee, kwani mtamfanyaje?!...kuna mtu hapo nyuma alitugeuza mashetani na tulikuwa wadogo kama piriton leo hayupo mnajifanya kumpiga mikwara mama wa watu kisa tu mnajua anasoma mtandaoni, hvi mnadhani urais ni kama umonitor wa darasa eti..
 
Vumilieni tu sukuma gang Kama wengine walivyokuwa wanauchukia utawala wa Mungu wenu wa Chato lakini Waliuvumilia mpaka pale Mungu aliposikia kilio Chao.

Sasa ni wakati wenu wakuishi Kama mashetani .
 
Wanajaribu kumblackmail mama teh teh teh

Magufuli ndo alikuwa na Nepotism, Ukanda, Udini na Ukabila.

Mwacheni Samia achape kazi, tena namuomba sana mheshimiwa Rais atusaidie kuondoa Udini, Ukabila na Ukanda vilivojiinua sana kipindi cha mwendazake, tunataka kuona watu wa makabila yote, dini zote, kanda zote wenye vigezo wakiwemo katika serikali yake bila kulaliaa upande mmoja
 
Back
Top Bottom